Wabunge wataka wahitimu wakopeshwe kwa vyeti vyao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kutumia vyeti vya wahitimu wa vyuo vikuu nchini kama dhamana ya kuwapa mikopo mbalimbali ya kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, aliyasema hayo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, akibainisha Serikali ina mifuko zaidi ya 45 inayohusika na mikopo mbali na mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri inayotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Latifa Juakali, alitaka kujua mpango wa Serikali kuanzisha bodi ya mitaji kwa wahitimu wa elimu ya juu kama ilivyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Akijibu swali la msingi, Naibu Waziri alisema Serikali imeupokea ushauri wa mbunge na kwamba imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana kupitia halmashauri kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani, huku akiwashauri wahitimu hao kutumia fursa hiyo kupata mitaji.

“Tunaangalia namna gani wahitimu watatumia vyeti vyao kupata mikopo tutaifanya tathmini na kufanya uamuzi, hili ni jambo mtambuka, linahusu wizara nyingine. Tunachukua ushauri ili tuone kama vyeti vinaweza kutumika kamdhamini mhitimu," alisema.

Naibu Waziri Kipanga pia alisema halmashauri zinatenga asilimi 10 ya mapato ya ndani ya kwa ajili ya kutoa mikopo kwa mgawanyo wa asilimia nne vijana, asilimia nne wanawake na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu.

“Mwanzoni ilikuwa lazima vijana 10 wawe kwenye kikundi na wawe na shughuli ya kufanya, kwa sasa masharti yamelegezwa hata wakiwa watano katika kikundi wanapewa mikopo ya kukidhi mahitaji yao ili waweze kurejesha na kujiajiri,” alifafanua.

Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya, alihoji ni lini wizara hiyo itatenga fungu maalum kusaidia vijana kama wanavyotoa mikopo ya elimu ya juu, huku akitolea mfano wa Wizara ya Kilimo inayotoa motisha kwa vijana wanaojiunga na kufanya shughuli za kilimo mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Akijibu swali hilo, Waziri Kipanga alisema jukumu la wizara ni kuratibu utoaji wa elimu nchini na wakishahitimu siyo jukumu lao pekee, bali la Serikali kwa ujumla, lakini kwa kuwa mbunge huyo anazungumzia motisha ili wajiajiri, Serikali inapokea ushauri huo.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ritha Kabati, alitaka kauli ya serikali kuhusu wahitimu wa vyuo vikuu kukatwa fedha zaidi licha ya kumaliza mikopo yao.

Waziri Kapinga alisema bodi imeanzisha dawati la malalamiko na kuwataka wahitimu walioendelea kukatwa fedha kupeleka hoja zao na itakapobainika walikatwa kimakosa watarejeshewa fedha zao.

Alisema mfumo wa mikopo hiyo unaonyesha nani kakopeshwa, karejesha kiasi gani na kimebaki kiasi gani, jambo linalowawezesha wanufaika kuona mwenendo wa deni lao.
 
Kwahiyo wakishindwa kulipa wanang'ang'ania cheti..😂

Ubovu sio wote wanauwezo wa money management!,hili neno lioneni hivihivi tu lakini ni gumu kuliishi acha tu!.
 
Unamkopesha ,tuseme milioni kumi, akishindwa kulipa kwa sababu yoyote ile, hicho cheti unakiuza au unakifanyia nini.
vitatelekezwa sana. Wabongo wengi hawaheshimu mikataba.
 
80% ya wahitimu wanadaiwa na HESLB halafu bado unawaongezea mzigo wa deni kwa kuwapa mikopo kwann wasiwape Ruzuku kwa wale watakao andika andiko zuri la mradi
 
Back
Top Bottom