A
Anonymous
Guest
Wahitimu wa kozi za Afya ngazi ya Diploma nchini zilizopo chini ya Baraza la Elimu na Mafunzo ya Ufundi(NACTVET) tunawasilisha malalamiko kuwa tumemaliza chuo tangu mwezi Septemba 2023 na matokeo yalitoka tangu mwezi Oktoba, lakini cha kushangaza hadi leo hatujapata vyeti vyetu.
Zaidi ya miezi Sita imepita na hakuna taarifa yoyote rasmi ya kusema tutapewa lini vyeti hivyo, na muda unazidi kwenda hali ambayo inazidi kutukatisha tamaa na kututia unyonge sababu hakuna kitu chochote tunaweza kufanya na taaluma zetu bila ya uwepo wa hivyo vyeti
Hatuwezi kuomba ajira hata ya kujitolea sababu hatuna utambulisho wa kuwa tumehitimu zaidi ya hivyo vyeti.!
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti juu ya hili na ikiwezekana mtuulizie kwa wahusika ni lini tutapata hivyo vyeti ili tuweze kuendelea na shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo kuomba ajira ili kujikwamua kimaisha.!
Aidha natanguliza shukrani zangu za dhati naamiin ombi langu litafanyiwa kazi.
Ahsante.!