Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Kwa kuwa msigwa ni waziri wa elimu wa serikali ya ccm chini ya magufuli basi ondoa shaka hiyo shule itapata walimu
unazijua kazi za mbunge? hilo lipo ndani ya uwezo wake na ni matokeo ya yeye kutowajibika kama mwakilishi wa wananchi katika ngazi ya halmshauri. over five years shule ipo jimboni mwake ina walimu wanne tu. Tena kufanya uhamisho ndani ya manispaa hauna gharama yeyote ni yeye kama mwakilishi wa wananchi kwenda kuongea na mkurugenzi au afisa elimu wa wilaya na kuhamisha baadhi ya walimu waliojazana kwenye shule zingine ndani ya manispaa.
 
unazijua kazi za mbunge? hilo lipo ndani ya uwezo wake na ni matokeo ya yeye kutowajibika kama mwakilishi wa wananchi katika ngazi ya halmshauri. over five years shule ipo jimboni mwake ina walimu wanne tu. Tena kufanya uhamisho ndani ya manispaa hauna gharama yeyote ni yeye kama mwakilishi wa wananchi kwenda kuongea na mkurugenzi au afisa elimu wa wilaya na kuhamisha baadhi ya walimu waliojazana kwenye shule zingine ndani ya manispaa.
Huyo ni msigwa mbunge wa chama cha upinzani cdm,sawa sasa iangalie hii shule ipo jimboni mwa mbunge wa ccm tena ni waziri
1461238339149.jpg
 
Magufuli na huyo dada naibu spika full komedy!Inakuwaje urudishe hela wakati wabunge kibao wanadai mishahara ya miezi minne?!Yote hiyo kutaka sifa kwenye vyombo vya habari!Serikali ya wasanii hii...
hakuna kazi wabunge wanayofanya hata hiyo mishahara bora wasilipwe tu...
 
Yaani Msigwa anaona raha hela zitumike kwa safari yake ya kwenda kuzurura nje kuliko kuwapa madawati watoto wanaokaa chini na kukalia mawe na matofali.

Ona hapo Msigwa akiwa kazini kwenye jengo la ubalozi wa Tanzania marekani.Hapo pichani ndio anaonekana kachachama anakagua jengo hilo la ubalozi kujua kama value for money ya hilo jengo iko sawa.


_DSC8604.JPG
msigwa ni kituko anataka kwenda nje kufanya starehe tu hana lolote
 
Wabunge wanataka kwenda nje kukagua nyumba?
Msigwa mpigaji tu eti kuangalia nyumba za ubalozi kwani mabalozi hawawezi kwenda kuziona na kuzitolea taarifa? Mwingine anasema anapinga kwa kuwa amesafiri kwa shida wakati wa mizunguko ya kamati,kwani wananchi tunavyohangaika haoni? Au ndo yale mawazo kwamba anataka aishi ni kama hayupo Tanzania ilihali wananchi tuna shida?
 
Huyo msigwa ni injinia wa majengo? Kwa hiyo akienda kukodolea macho jengo anajua kama ukarabati limetumia milioni kadhaa ni sahihi au sio sahihi kwa tu kukodolea macho?

HIYO VALUE FOR MONEY INAPIMWA KWA KUKODOLEA MACHO NA KUPIGA PICHA MBELE YA JENGO?

Wanaenda tu kutalii.Wasiende pesa za safari zao zipelekwe kwenye madawati.
Wacha kuwa na akili za kiwavi,kwa mawazo yako wabunge walizaliwa kuwa wabunge tu?bungeni kuna watu wenye professional zao ikwemo hiyo ya civil engineering, wacha kujiondoa ufahamu kisa kutetea ccm na kumponda mbunge kisa anatoka upinzani
 
Tena mi ningependa watuletee maoni huku mitaani wananchi tupige kura kama kuna haja wabunge waendelee kupewa posho ya siku wakati wana mshahara.
 
Huyo msigwa ni injinia wa majengo? Kwa hiyo akienda kukodolea macho jengo anajua kama ukarabati limetumia milioni kadhaa ni sahihi au sio sahihi kwa tu kukodolea macho?

HIYO VALUE FOR MONEY INAPIMWA KWA KUKODOLEA MACHO NA KUPIGA PICHA MBELE YA JENGO?

Wanaenda tu kutalii.Wasiende pesa za safari zao zipelekwe kwenye madawati.
TATIZO HUJASOMA POST YANGU MPAKA MWISHO AU UMENIELEWA VIBAYA. KAMATI ZA BUNGE ZINAKAGUA MIRADI MBALIMBALI INAYOFANYWA NA SERIKALI. KWA DHANA YAKO KWAMBA LAZIMA MBUNGE AWE INJINIA NDIO AKAKAGUE MAJENGO BASI KAMATI ZOTE ZIFUTWE MAANA HAZINA MAANA KWANI WANACHAGUA WABUNGE KWENYE HIZO KAMATI NA SIO PROFESSIONALS. WAPO MADAKTARI WA BINADAMU KWENYE KAMATI YA MIUNDOMBINU SO ILO LA MSIGWA LISIKUPE SHIDA KUNA SEMINA WANAPATIWA
 
Kwa hiyo kila wakati lazima waende kukagua hayo majengo? kwenda kuthibitisha kuwa yapo au kuwa yana magurudumu yatakuwa yameondoka kwenda sehemu nyingine?
HIZO NI KAZI ZAO NA UTARATIBU WALIOJIWEKEA KAMA BUNGE, TATIZO LAWEZA KUWA KWENYE RATIBA YA BUNGE IPO ILA BUNGE IKATOKEA HAINA PESA. JAMANI TUWE OBJECTIVE TUSILITAZAME LA KWENDA KUKAGUA BALOZI KAMA KIGEZO TU CHUKULIA KAMATI YA AFYA NA YA ELIMU HATA YA MIUNDOMBINU ISHINDWE KWENDA KUKAGUA ENEO KUNA MLIPUKO WA EBOLA AU HUDUMA MBAYA ZA AFYA, AU HUDUMA DUNI ZA BARABARA KISA BUNGE HALINA HELA WAKATI PESA WAMERUDISHA SERIKALINI. ISSUE NI MAMBO MBALIMBALI YA BUNGE KUKWAMA ILA LA KUKAGUA BALOZI LIKIWA MOJAWAPO
 
HIZO NI KAZI ZAO NA UTARATIBU WALIOJIWEKEA KAMA BUNGE,

Wasiposafiri kama nchi tutakuwa tumepata hasara gani? Au wamejiwekea tu utaratibu kuwa kila mwezi fulani tukale kuku london,mwezi mwingine marekani,mwingine Japan!!!!!!!!
Wasipoenda kama taifa tutakuwa tumepoteza nini.

Na ni lazima wasafiri sasa? hawawezi safiri baada ya bunge la bajeti hili kumalizika? Kuna uharaka gani?
 
pic+mps.jpg


WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.


Chanzo: Nipashe
Msigwa nae hizo kamati toka zimeanza kusafiri ni kipi kilichobadilika au kipi kimeleta tija au bado anataka safari alizokuwa anatumbua akisafiri na Nyalandu na akina Lembeli,safari zao hazisaidii chochote,hizi ni zama za IT watumie Skype.
 
Mnapoteza wakati wenu bure...hazirudi. Binafsi naona jambo la maana kununua madawati na kuondoa aibu iliyopo. Zingeachiwa Bunge tusingeziona tena na wala tusingejua zimekwenda wapi. Sana sana wangezitumia katika hivyo hivyo walivyokuwa wakitumia siku zote. Bilioni 6 ni pesa nyingi sana.
 
Walizoea pesa za kumwaga kwenda kutembea ulaya bila misingi wataisoma namba tu
 
Back
Top Bottom