Kifupi ZITO ni mzungumzaji mzuri na anajua kujenga hoja. Sasa kwa nini maswala ya umeme, maji na usafiri ambavyo ni shida kweli KIGOMA haongei, hajengi hoja hata sisi tukaona. kama serikali itatekeleza au la ni swala jingine.
Sikufichi ndugu yangu, kwanza kauri yake kwenye utetezi wa Downs binafsi imenikera sana. Anasema ooooh, nchi itakuwa gizani, ebo, Kigoma tuko gizani kila siku mbona haji kutuhamasisha tukaandamana kuonyesha hasira zetu.
.
Sasa kigoma sisi hatuna umeme siku nyingi 2, sasa kukuosa kwetu umeme si ni moja ya kutojengwa viwanda kweli.
Hali ya kigoma ni hali ambayo wangeweza kuungana wabunge wa kule na kutoa tamko au msimamo flani lakini, kimyaaaaaaaa.
Naomba nipate michango yenu wanajamii, kutokana na mimi binafsi kutowaelewa Vizuri wabunge wa KIGOMA
Sijui niseme wanauzalendo sana kwa mambo ya kitaifa au ni vipi, wanashadadia sana mambo mengine lakini MATATIZO ya wana KIGOMA hata hawayaoni.
Angalia mifano.
Mh ZIto na mawaswala ya kitaifa na sehemu nyingine kama mambo ya Downs, BUZWAGI, KIWIRA,
Mh Shelukamba yeye amejikita kwenye utetezi wa mafisadi wote mnajua.
Bwana Msambya ya yeye ni UDINI, yakija mambo ya OIC na Mahakama ya Kadhi, Bungeni panajimbika.
SASA wanajamii, mbon matatizo makubwa ya wanaKIGOMA kama Usafiri, Maji na UMEME wala hayawasumbui wako kimyaaaaaaaaaaa, nini TATIZO lao.
Hivi ndugu zangu kuna mtu asiyefahamu kuwa wana KIGOMA ndio waathirika wakubwa wa usafiri wa Reli ya KATI, mbona wabunge wetu hawakomalii issue za hawa mafisadi wa kihindi walioko pale kwelye shirika la Reli badala yake wanakomalia vitu vingine kabisa?
Hivi Mh Zito hajui kuwa kigoma wapo GIZA kila siku, mbona hilo halimsumbui badala yake anakomalia mitambo ya Downs ambayo najua kabisa haitawapatia wanakigoma umeme.Kigoma siku zote iko giza, hakuna mbunge wa kigoma anayeinua mdomo kulisema.
Wanajamii, utashangaa, pamoja na Kigoma kuwa na Ziwa, lakini mji ule hauna maji. Hilo wala halimsumbui ndugu yetu Serukamba, yeye kutwa, kuchwa michango yake ni utetezi wa mafisadi bungeni. Ataongea mpaka utamuonea huruma kwa mishipa na mate kumtoka, nini Tatizo la wabunge wetu? Au ni kwa kwa kuwa wao wenyewe hawaishi kule, au ndio kutaka sifa tu au nini.
Nisaidieni wanajamii, niko kwenye TUTA.
Kujaribu kumbebesha Zitto lawama ya kutoendelea Kigoma au kutochangamkiwa Kigoma ni kujaribu kukwepa ukweli. Matatizo ya Kigoma hayatokani na Zitto kupiga kelele au kutopiga kelele! Matatizo ya Kigogoma yamefungamana kwa miaka karibu 50 na utawala wa Chama cha Mapinduzi.
Ni chama cha Mapinduzi chenye serikali na chenye sera za sehemu mbalimbali na miradi mbalimbali. Wakati wenzenu Dar wanazungumzia kujengewa Flyovers nyinyi Kigoma hata reli ya kati haijatengemaa! Sasa hivi kutoka Arusha kwenda Mbeya ni karibu kwa masaa kuliko toka Dar hadi Kigoma ingawa kijiografia Kigoma ni karibu na Dar kuliko Mbeya na Arusha!!!
Jinsi unavyozungumza ni kana kwamba Zitto hajawahi kuzungumzia masuala ya Kigoma au wapiga kura wake Bungeni. Naomba utuletee rekodi ya Zitto Bungeni kuhusu masuala haya maana inawezekana wakati anayazungumza hukuyasikia.
Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.
CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!
2006-03-26 09:01:54
By Simon Kivamwo
The Member of Parliament for Kigoma North, Kabwe Zubeiry Zitto, has welcomed the recent pledge by President Jakaya Kikwete that his government was determined to build economic infrastructure in regions styled as forgotten.
The regions are Kigoma, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Rukwa and Tabora.
The MP from the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) told the Sunday Observer this week that, being the secretary general of the Kigoma-based MPs, he would urge his team to rally behind the President in fulfilling the pledge.
'On behalf of the MPs from Kigoma Region, I promise wholehearted co-operation to the President to make sure that the pledge bears fruit.'
He said Kigoma could not have been in its present state of poverty if previous governments had not neglected it.
Kujaribu kumbebesha Zitto lawama ya kutoendelea Kigoma au kutochangamkiwa Kigoma ni kujaribu kukwepa ukweli. Matatizo ya Kigoma hayatokani na Zitto kupiga kelele au kutopiga kelele! Matatizo ya Kigogoma yamefungamana kwa miaka karibu 50 na utawala wa Chama cha Mapinduzi.
Ni chama cha Mapinduzi chenye serikali na chenye sera za sehemu mbalimbali na miradi mbalimbali. Wakati wenzenu Dar wanazungumzia kujengewa Flyovers nyinyi Kigoma hata reli ya kati haijatengemaa! Sasa hivi kutoka Arusha kwenda Mbeya ni karibu kwa masaa kuliko toka Dar hadi Kigoma ingawa kijiografia Kigoma ni karibu na Dar kuliko Mbeya na Arusha!!!
Jinsi unavyozungumza ni kana kwamba Zitto hajawahi kuzungumzia masuala ya Kigoma au wapiga kura wake Bungeni. Naomba utuletee rekodi ya Zitto Bungeni kuhusu masuala haya maana inawezekana wakati anayazungumza hukuyasikia.
Lakini zaidi ni kuwa, kama Kigoma wakitaka mabadiliko ya kweli ni wao wachukue hatua za kurudisha kadi za CCM!! na kuifuta CCM kwenye utawala wa mkoa wao na kuchagua chama ambacho kitakuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia raslimali zenu na chenye kuweza kupiga "kelele" bungeni. Vinginevyo, lawama kwa mtu mmoja kwa matatizo ya mkoa mzima ni kukwepa ukweli kuwa wenye wajibu na wenye kustahili lawama ya kudumaa kwa Kigoma (kama ilivyo Mtwara, Lindi, Tabora n.k) ni serikali ya CCM tu.
CCM ndiyo sababu, Zitto ni kisinigizio!
...ni hoja inayofaa kujibiwa na wabunge wote wa Kigoma, hata kama kuna wasemaji wao humu ndani ya JF. Naamini mh.Zitto Kabwe jana ulipokuwa online, ulichungulia pia mada hii, na ni hiari yako kujibu kwa wakati muafaka ili kuwaondoshea duku duku wana Kigoma wanao oppose na wanao propose maendeleo ya Mkoa huo, au ku "pass", ...binafsi nilitegemea utasema lolote, anyway; 'subra yavuta kheri'Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!
... anyway; 'subra yavuta kheri'
Sio kigoma tu, ni sehemu zote ambazi waarabu waliharibu hali ya hewa, yaani walileta harufu mbaya ya kuuza na kupitisha watumwa, ni kama kumelaaniwa, na hakutakuja kuendelee. mtu mwingine angefikiri kuwa sehemu ya East african long distance route(Bagamoyo,Mpwapwa and kondoa irangi,Tabora,Kigoma to Ujiji),...wanaopenda kucheza bao saa sita mchana wakisubiri azana wakaswali. maeneo yamekuwa makame kabisa na ndo yanaongoza kwa umasikini na kukosa chakula kila mwaka
Mheshimiwa Spika, naomba niwasilishe hali ya umasikini kiwilaya kwa wananchi kwa kigezo cha idadi ya wananchi walio katika Umaskini wa kutupwa (% of households below basic needs poverty line)
Wilaya masikini Zaidi
Bunda 68%
Musoma 64%
Geita(vijijini) 62%
Mbarari 13%
Serengeti 61%
Singida(vijijini) 56%
Namtumbo 55%
Meatu 53%
Kisarawe 51%
Babati 50%
Wilaya zenye Ahueni
Bukoba Mjini 11%
Arusha Mjini 12%
Mbeye Mjini 12%
Morogoro Mjini 14%
Kinondoni 14%
Nyamagana 15%
Lushoto 16%
Ilala MC 16%
Tanga Mjini 17%
source; http://www.bunge.go.tz/bunge/docs/mipango.pdf