Wabunge wa CCM wapigwa Mkwara

Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
256
Kuna Tetesi kwamba Wabunge wa CCM wamepigwa Mkwara na Chama chao kutokutaka Ushahidi toka kwa Wabunge wa Upinzani pale wanapowasilisha madai yao dhidi ya Serikali.

Kwani kwa kutaka ushahidi kumepelekea Wabunge hao wa Upinzani kuleta Ushahidi ambao umekuwa ukiumbua Serikali na Viongozi wake kama ule wa Lema na Waziri Mkuu, ule wa Kafulila, ule wa Zitto na hata ule wa Tundu Lissu n.k.

Hii imepelekea hata jana Mh. Mnyika alipotamka kuwa anaushahidi kuwa kuna viongozi wa dola waliohongwa na Wafanyabiashara ya Mafuta hakuna Mbunge yeyote wa CCM aliyetaka Mh. Mnyika alete Ushahidi.

Nawasilisha.
 
if the rumor is true, i can see their logic simply bcoz they like power and they r not willing to expose their true colors
 
Nakubaliana na wewe mkuu, coz Mnyika alirudia statement yake kama mara tatu hivi ili kuwatega. Lakini hakuna hata mmoja aliyeomba uthibitisho, hata NS alikuwa kimya.
Lukuvi, Mary Nagu, Kigwangalla, Mwigulu Nchemba na Samwel Sitta hawakuwepo bungeni nini?
 
Ni afadhali umetujuza, asante sana, ifuatayo ni mbinu mbadala: wabunge wa upinzani wanapoibua tuhuma/hoja zenye ushahidi, wasisubiri ushahidi uombwe na wabunge wa CCM, mfano anaweza kutoa hoja Lema na zitto au Regia kwa niaba ya bunge awashawishi wabunge mtoa hoja alete ushahidi.

CCM wakipinga ushahidi usiletwe tafsiri ya moja kwa moja tuhuma zinajithibitisha, wakiunga mkono unapelekwa ushahidi mzito kwa msisitizo wa kutakiwa usomwe bungeni wapiga kura wamjue mkweli ni nani. Hawawezi kuusimamisha wakati!!
 
Hakuna Ushahidi mzuri kama ukiletwa kwa Wananchi, sisi ndio tutakaoamua na kutoa hukumu. Mnyika lete ushahidi kwa Wananchi na pia peleka kwenye vyombo vya habari viiumbue Serikali legelege ya chama legelege.

Kwani hata akitoa ushahidi bungeni utawekwa kapuni na Spika wa Magamba. Mi naona Wabunge wa Upinzani wakiambiwa wapeleka ushahidi Bungeni na ushahidi mwengine tuletewe na sisi wananchi
 
Ni kweli kabisa hawa vilaza wa CCM wamepigwa mkwara.
Kama kuna mtu anabisha aseme nitoe USHAHIDI.
 
Mwishdo wa CCM nauona hauna zaidi ya mwaka mkere lazima atajiuzulu
 
Yaani hadi vichekesho sasa.
Nadhani sasa mbunge wa upinzani anapoweka wazi udhalimu fulani ni vizuri akawauliza wabunge 'mnahitaji ushahidi' nadhani Wabunge wa CCM kwa haraka haraka watajibu 'Hapana hatuhitaji'.

Mkuu Ndibalema hapo kwenye nyekundu umenichekesha sana. Naunga mkono wabunge wa upinzani sasa wabadili namna ya kuwatega wawaulize kama ulivyopendekeza. Na wakijibu hatuhitaji itaashiria nini mkuu?
 
Kuna Tetesi kwamba Wabunge wa CCM wamepigwa Mkwara na Chama chao kutokutaka Ushahidi toka kwa Wabunge wa Upinzani pale wanapowasilisha madai yao dhidi ya Serikali, kwani kwa kutaka ushahidi kumepelekea Wabunge hao wa Upinzani kuleta Ushahidi ambao umekuwa ukiiumbua Serikali na Viongozi wake kama ule wa Lema na Waziri Mkuu, ule wa Kafulila, ule wa Zitto na hata ule wa Tundu Lissu n.k.

Hii imepelekea hata jana Mh. Mnyika alipotamka kuwa anaushahidi kuwa kuna viongozi wa dola waliohongwa na Wafanyabiashara ya Mafuta hakuna Mbunge yeyote wa CCM aliyetaka Mh. Mnyika alete Ushahidi

Nawasilisha.
Waache wachimbane mikwara tuu......... Kuna namna nyingine ya kufanya.............. kwa mfano... Mnyika anaongea halafu Lisu anaomba ushahidi........AU ........... Mnyika anaongea.... Kafulila anaomba ushahidi......... INAKUWA KWISHNEIIII....
 
Back
Top Bottom