Wabunge wa CCM wapigwa Mkwara

Yaani hadi vichekesho sasa.
Nadhani sasa mbunge wa upinzani anapoweka wazi udhalimu fulani ni vizuri akawauliza wabunge 'mnahitaji ushahidi' nadhani Wabunge wa CCM kwa haraka haraka watajibu 'Hapana hatuhitaji'.

Karibu ningecheka mwenyewe. Hii imekaa vizuri sana Ndibalema.
 
Kuna Tetesi kwamba Wabunge wa CCM wamepigwa Mkwara na Chama chao kutokutaka Ushahidi toka kwa Wabunge wa Upinzani pale wanapowasilisha madai yao dhidi ya Serikali.

Kwani kwa kutaka ushahidi kumepelekea Wabunge hao wa Upinzani kuleta Ushahidi ambao umekuwa ukiumbua Serikali na Viongozi wake kama ule wa Lema na Waziri Mkuu, ule wa Kafulila, ule wa Zitto na hata ule wa Tundu Lissu n.k.

Hii imepelekea hata jana Mh. Mnyika alipotamka kuwa anaushahidi kuwa kuna viongozi wa dola waliohongwa na Wafanyabiashara ya Mafuta hakuna Mbunge yeyote wa CCM aliyetaka Mh. Mnyika alete Ushahidi.

Nawasilisha.

mkuu mbona unasema tetesi? we sio mmojawapo wa hao mafarisayo? tuambie mmeambiwaje na chama chenu
 
kama ulikwepo akilin kwangu mzee, ndo nishaandaa nitume mkuu. bahati nzuri umeniwahi, hapo kweli kwishnnei.
Waache wachimbane mikwara tuu......... Kuna namna nyingine ya kufanya.............. kwa mfano... Mnyika anaongea halafu Lisu anaomba ushahidi........AU ........... Mnyika anaongea.... Kafulila anaomba ushahidi......... INAKUWA KWISHNEIIII....
 
Ni afadhali umetujuza, asante sana, ifuatayo ni mbinu mbadala: wabunge wa upinzani wanapoibua tuhuma/hoja zenye ushahidi, wasisubiri ushahidi uombwe na wabunge wa CCM, mfano anaweza kutoa hoja Lema na zitto au Regia kwa niaba ya bunge awashawishi wabunge mtoa hoja alete ushahidi.

CCM wakipinga ushahidi usiletwe tafsiri ya moja kwa moja tuhuma zinajithibitisha, wakiunga mkono unapelekwa ushahidi mzito kwa msisitizo wa kutakiwa usomwe bungeni wapiga kura wamjue mkweli ni nani. Hawawezi kuusimamisha wakati!!
Nimeipenda hii, itakuwa mbinu mbadala na ya kisayansi zaidi. Naam,Tundu akimwaga vitu kuhusu uchafu wa serikali na kiongozi Sugu anang'aka kutaka ushahidi na anakomaa kwelikweli sijui watatokea wapi.
 
Yaani hadi vichekesho sasa.
Nadhani sasa mbunge wa upinzani anapoweka wazi udhalimu fulani ni vizuri akawauliza wabunge 'mnahitaji ushahidi' nadhani Wabunge wa CCM kwa haraka haraka watajibu 'Hapana hatuhitaji'.

Inachekesha, japo kwa uchungu! Nilitegemea hata mimi jana Mnyika kutakiwa kutoa ushahidi, hakutakiwa. Sasa wakianza kuuliza kuwa mnataka ushahidi, ama hawatajibu au watasema HAPANA na jibu lolote litakuwa MOTO...!
 
sasa kama kuna dhana ya kutokuomba ushahidi basi mtoa tuhuma anaweza toa tuhuma na ushaidi nusu kimitego kusudi wajifanye kuomba zaidi hapo ndipo amwage data za kutosha ili waumbuke
 
waliumbuka sana kwa kutaka ushahidi, wakijua labda kwa vile Lissu, Lema, ni wageni kwenye bungeni wasingekuwa na vidhibiti..wakaumbuka, so wakapeana semina na kukubaliana hakuna tena kuomba ushahidi..! imekul akwoa, coz wananchi tumeshang'amua janja ya magamba..2015 mwisho wao, ikiwezekana hata kabla !tunataka nchi tufaidi wote na sio wachache!
 
Kuna Tetesi kwamba Wabunge wa CCM wamepigwa Mkwara na Chama chao kutokutaka Ushahidi toka kwa Wabunge wa Upinzani pale wanapowasilisha madai yao dhidi ya Serikali.

Kwani kwa kutaka ushahidi kumepelekea Wabunge hao wa Upinzani kuleta Ushahidi ambao umekuwa ukiumbua Serikali na Viongozi wake kama ule wa Lema na Waziri Mkuu, ule wa Kafulila, ule wa Zitto na hata ule wa Tundu Lissu n.k.

Hii imepelekea hata jana Mh. Mnyika alipotamka kuwa anaushahidi kuwa kuna viongozi wa dola waliohongwa na Wafanyabiashara ya Mafuta hakuna Mbunge yeyote wa CCM aliyetaka Mh. Mnyika alete Ushahidi.

Nawasilisha.

Nawaomba wabunge wa upinzani wakishusha hoja iwe inaambatana na ushaihidi wa nguvu ili wawe wamemaliza kabisa business yaani kwenda mpaka kwenye ushahidi ambao CCM wanauogopa!!
 
Wacha wapigane mkwara- wataumbuka sana safari hii. Bado hata mwaka mmoja haujaisha. Kila ninapoona Mnyika anawaumbua mimi nakumbuka mikesha ya karibu siku 3 kulinda kura zake. Halafu najipongeza mwenyewe.
mkuu asnteni sana kulinda kura za Mnyika maana kichwa kama hiki kingechakachuliwa...daah sasa wagombea wangapi wa cdm wazuri kama Mnyika wamechakachuliwa? serikali itaumbuka very soon....
 
Yaani hadi vichekesho sasa.
Nadhani sasa mbunge wa upinzani anapoweka wazi udhalimu fulani ni vizuri akawauliza wabunge 'mnahitaji ushahidi' nadhani Wabunge wa CCM kwa haraka haraka watajibu 'Hapana hatuhitaji'.

Mkuu mimi naona kwa faida ya Watanzania kujua ufisadi na udhalimu mkubwa wa hawa magamba kila tuhuma dhidi ya chama hicho na ushahidi wake uanikwe hadharani badala ya kusubiri magamba waombe ushahidi. Hii itasaiadia zaidi katika kuzidi kukisambaratisha chama hicho cha magamba. Kama ushahidi utawekwa hadharani na magamba na Serikali wakiamua kukaa kimya, Watanzania tutawauliza magamba na Setrikali yao legelege kulikoni!?
 
Nimeipenda hii, itakuwa mbinu mbadala na ya kisayansi zaidi. Naam,Tundu akimwaga vitu kuhusu uchafu wa serikali na kiongozi Sugu anang'aka kutaka ushahidi na anakomaa kwelikweli sijui watatokea wapi.
<br />
<br />
Kwamsisitizo wanaliambia bunge nia ya kuufikisha ushahidi huo kwa wananchi kupitia mikutano na maandamano!!
 
Mimi nashauri kama wamekuwa wajanja basi hapa ndio pa kuwabana, itabidi CHADEMA wajiandae na mbinu za kimkakati, kwa mfano Wenje akitoa tuhuma basi inatakiwa Lema asimame kuomba muongozo wa spika ili kumtaka Wenje athibitishie Bunge kama anasema ukweli au uongo.
Hii ndio njia ya kula sahani moja na Magamba. hii style inaitwa man to man.
 
Weep not child,
Weep not my darling,
The ravening clouds shall not be victorious
They shall no longer posses the sky.....

Clouds were colonies then
it is ccm now, it shall no longer posses the parliament, no longer victorious ,loosing evrything so fast...
Even the confidence,

walifikiri ngugi alisemea wakoloni tu, magamba ni zaidi ya wakoloni, they knw their days are numberd,magamba have blinded them all.
 
nakubaliana na ww nilishanga sana nanilisema lazima magamba waombe muongozo kuhusu ushahidi lakini ikawa G itakuwa ni kweli
 
Walikuwa wanafikiri ushahidi utawaumbua wapinzani ikawa vice versa.!

Kwani mbunge wa upinzani hata akiwa wa chama kimoja ana haki kamili ya kuomba mwongozo.
sasa angesimama mbunge mwingine wa Chadema kuomba mwongozo. Kwani hawakufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom