Wabunge wa CCM kuonesha kutokuwa na imani na serikali lazima kuwe na matokeo

Mwanakijiji umeonesha Umbumbu mkubwa kwa kutofahamu kazi za Mbunge! Katiba ya JM wa Tanzania haijaonesha kazi ya Mbunge wa Upinzani ni ipi na ya Chama kinachotawala ni ipi!? Kazi ya Bunge na Mbunge ni kuibana serikali!

watu kama wewe sijui kwa nini hampot*i? Ila hamwezi kuzuia hii nguvu ya wananchi

Mwanakijiji umeonesha Umbumbu mkubwa kwa kutofahamu kazi za Mbunge! Katiba ya JM wa Tanzania haijaonesha kazi ya Mbunge wa Upinzani ni ipi na ya Chama kinachotawala ni ipi!? Kazi ya Bunge na Mbunge ni kuibana serikali!

Naomba nitofautiane na wewe kwa ulichoandika, kwa kuwa pamoja na kuelezwa kazi za mbunge
ni zipi lakini haifanyiki kivitendo bali ipo kinadharia kwa kuwa wabunge wote wa CCM wana matarajio
kuwa wao ni mawaziri watarajiwa, wanashindwa kuibana serikali ya chama chao kwa kutarajia fadhila
za bwana mkubwa. Nadhani unaingia kwenye mkumbo uleule wa kuendeleza siasa katika mambo nyeti...

Pinda hawezi kujiuzulu na Bunge la chama chake likabakua . Akijiuzulu LAZIMA Kikwete avunje na bunge ili wote waanze upya.

I do not see the connection MKJJ -Pamoja na kuwa siamini kuwa Pinda anaweza kujiuzulu; lakini sioni kwanini Pinda akijiuzulu ni lazima JK avunje bunge? Ninachojua ni kuwa anapaswa kuvunja baraza la mawaziri tu. Hii ilitokea wakati Lowasa alipojiuzulu, ni baraza la mawaziri tu lililovujwa na si bunge. Iweje sasa hivi iwe tofauti?

Kwa jinsi mkuu wa nchi anavyoipeleka nchi kwa sasa kila kitu kipo shaghalabaghala. Pinda kweli kwa yale yaliyotokea kuhusu suala la Jahiro anapaswa kujiuzulu kilinda heshima yake. Na hata kama baraza lake la mawaziri litavunjika kwa jinsi ilivyo kuwa kwa Lowasa, sioni sababu ya mtu makini na atakaependa kuwatumikia watanzania hata baada ya miaka minne ya jk, kukubali uteuzi wa nafasi ya uwaziri. Kukubali nafasi hiyo ya kuteuliwa katika kipindi hiki cha jk ni kukataa kuaminiwa na watanzania kwa nafasi yoyote ya kisiasa baada ya kipindi cha uraisi wake.
Hivyo sidhani kama kuna kiongozi makini anaependa kuteuliwa kushika wadhifa ndani ya serikali kwa sasa ila wale wenye tamaa na lengo la liwalo na liwe.

Mawanakijiji, kwanza huwa unapenda kuandika maneno meeeeengi kwa kuandika vitu vichache ambavyo ungekuwa makini katika kuandika kwako visingezidi mistari mitatu. Ni ukosefu wa ya kufanya au kupenda kuyakuza mambo ndio unaokupelekea kufanya hivyo? au ndio tabia mbaya tu ya majungu na ufataani?

Wabunge wa CCM hawako pale bungeni kwa kuchaguliwa na au kuitetea Serikali kama ufikiriavyo au unavyotaka ieleweke. Wabunge wapo pale kwa kuchaguliwa na wananchi wao na si vinginevyo.

Serikali itapokuwa haitendi watakavyo wananchi. mbunge anakuwa hana chama pale. Kwani hata ukichaguliwa na wanachama wa chama fulani lakini ukifika pale unakuwa ni Mbunge wa wananchi wote wa Bungeni kwako, wa chama kilichokuchagua na wasio wachama chako na wasio na vyama kabisa.

Kuna wananchi wengi tu ambao ni wanachama wa chama fulani lakini ikifika uchaguzi huwa wanamchaguwa mbunge kama mbunge na bila kujali anatokea chama kipi.

Usitake ujaze watu ujinga kwa muono wako finyu kuwa mradi mbunge ni wa CCM basi waliomchaguwa ni wana CCM tu au anawawakilisha wana CCM tu. Huo ni muono finyu saaana na usiokuwa na mantiki.

Pinda kadhalilishwa na serikali. Tutamkumbuka ndani ya nafsi zetu pale atakapofanya maamuzi magumu ya kujiuzulu

Ninachomaanisha ni kwamba, je wabunge wa ccm wako tayari kulioa gharama ya kuiumbua na kuichachafya serikali yao? Au wako tayari kyonekana,wanaichachafya tu? Pinda anaweza kutusaidia hapo kesho jwa kutoa hojakuwa Bunge limpigie kura ya roll call ya kuwa ba imani naye. Wasio na imani naye wakuwa wengi atajiuzulu. Wajati huohuo Kikwete awaambie wabunge wa ccm kuwa wakioiga kura ya kutokuwa na imani na pinda, atavunja bunge. Tuone ni kina nani ccm kweli wanataka mabadikiko.

Ninachomaanisha ni kwamba, je wabunge wa ccm wako tayari kulioa gharama ya kuiumbua na kuichachafya serikali yao? Au wako tayari kyonekana,wanaichachafya tu? Pinda anaweza kutusaidia hapo kesho jwa kutoa hojakuwa Bunge limpigie kura ya roll call ya kuwa ba imani naye. Wasio na imani naye wakuwa wengi atajiuzulu. Wajati huohuo Kikwete awaambie wabunge wa ccm kuwa wakioiga kura ya kutokuwa na imani na pinda, atavunja bunge. Tuone ni kina nani ccm kweli wanataka mabadikiko.

MKJJ, kuna hoja iliwahi kutolewa humu kuwa Pinda alipotoa kauli ya mwanzo pale bungeni alikuwa na document ile aliyoionyesha Mama Shelukindo lakini baada ya kuonyeshwa nyingine na hivyo kuweka shaka ya ukweli wa ipi ni halali basi akapoa na hivyo alipokuja kutoa maelezo mara ya pili akawa mpole na akasema amepokea maelekezo mengine. Sasa kwa hali hii tunategemea ajiuzulu au hata kuwa athubutu kuomba hiyo kura ya kutokuwa na imani naye?

Jamani enough of the talking, complaining etc!
Mimi nataka kulianzisha;

Mkinihakikishia yafuatayo:-
1: Kupigania Reform (maandamano n migomo)
2: Mtanitunzia mwanangu na mama yangu

NIJIUNGUZA MOTO pale askari monument!
Nasubiri response!

Any way tunaweza kujaribu kujenga hoja nzuri hapa kuwa PM ajiuzulu sawa, lakini lakini tujiulize kila anacho shauri PM lazima Rais akifuate?

Si mtetei PM kama mtu safi lakini siioni pia hoja nzito ya kumfanya ajiuzulu ati kwasabubu rais hajafata ushauri wake.

Najua tunapenda kuchukua maneno ya Hayati Nyerere kama msaafu, lakini yeye alifuata kila ushauri aliopewa na ma PM wake?

Kuna mambo mengi mno Rais anayoshauriana na PM wake na wasahauri wengine, tena wakati mwingine yanakuwa ya kuvutana hoja lakini mwisho wa siku lazima waje na kitu kimoja.

La JK sina tatizo nalo anapaswa kujipima

Hatukatai Pm kutofautiana na rais,ila si kwa hili la Pm kujiridhisha na kutoa tamko zito la hukumu tena bungen kisha ikulu-raisi anamsafisha na kupingana na Pm minister wake.

nahisi leo usiku mkewe ana kazi ya kumnyamazisha....atalia huyo.......

Dr Slaa wa ukweli alizungumza kule Arusha
kuwa Pinda ni bingwa wa kusema uongo
na wao CHADEMA watamfundisha kusema ukweli.

Naona Mungu ameleta mazingira hayo na huu
ndo wakati mwafaka wa kumpa fundisho.

NaAJUE ANAPODANGANYA BUNGENI KWA KUDHANI
ANAMFURAHISHA ****** AJUE WAZI ******
NI KIGEU GEU ATAPOTEZA MASHARIKI NA MAGHARIBI.

Jamani enough of the talking, complaining etc!
Mimi nataka kulianzisha;

Mkinihakikishia yafuatayo:-
1: Kupigania Reform (maandamano n migomo)
2: Mtanitunzia mwanangu na mama yangu

NIJIUNGUZA MOTO pale askari monument!
Nasubiri response!

mmefika wawili ...safi sana ni pm tafadhali......tunahiji njia ya mkato ili kufanikisha mambo ...hivi hivi hatuwezi.ni pm tafadhali namba ako a simu tu inahitajika

It may be a winding path; it may be longer, though its mysteries make it much more interesting.

Back
Top Bottom