Wabunge wa CCM kuonesha kutokuwa na imani na serikali lazima kuwe na matokeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kuonesha kutokuwa na imani na serikali lazima kuwe na matokeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 24, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Wabunge wa CCM wanagongana na serikali yao. Wanainyanyasa na kuimbua mbele za watanzania. Nimewahi kuandika huko nyuma kuwa ni jukumu la upinzani kudhoofisha serikali iliyoko madarakani ili ianguke na hata ikibidi ilazimike kuitisha uchaguzi mapema (early election). Nikasema wakati ule kuwa siyo jukumu la upinzani kuisaidia CCM kutawala. Sasa kinyume cha hilo nacho ni kweli. Jukumu la wabunge wa CCM ni kukitetea chama chao na hasa serikali yao isije kuanguka.

  Kwa miezi ya karibuni sasa wabunge wa CCM wanaonekana kuwa na mgongano na serikali yao. Maneno yao makali na hata misimamo mikali dhidi ya mawaziri wa serikali hiyo ni mashambulizi ya wazi, dhahiri na yaliyopangwa. Upande mmoja ni wazi wapo ambao wanafanya hivyo kama sehemu ya political triangulation lakini wapo pia wanaofanya hivyo kama sehemu ya tofauti ya msingi kati yao na chama chao. Ni hawa wa kundi la pili ndio ambao hasa nawazungumzia kwani wale wengine wanafanya kwa ajili ya kugeresha wapinzani na kuwahadaa watanzania ili CCM izidi kutawala.

  Hata hivyo kwa kundi hilo la pili ambalo kweli lina tofauti za msingi na serikali yao na wameonekana kuwa na uadui wa wazi na baadhi ya watendaji wa serikali (open hostilitiy) hawawezi kuwa hivyo bila kuwa na matokeo. Nina maana ya kwamba wabunge wa chama tawala wanapoamua kugongana na serikali yao kwa kuonesha kutokuwa na imani nayo basi lazima wawe tayari kuishi na matokeo ya msimamo huo.

  a. Walipoamua kukataa bajeti ya Wizara ya nishati na Madini kwa maneno makali hadi kulazimisha serikali kuiondoa walionesha kutokuwa na imani na serikali. Kwamba, hawakuamini serikali ingeweza kuleta bajeti nzuri na yenye manufaa kwa wananchi na jinsi walivyomshambulia Ngeleja - mteuliwa wa RAis - walijionesha wazi kuwa wana matatizo na Kikwete mwenyewe.

  b. Ilipokuja bajeti ya Uchukuzi navyo ilikuwa hivyo hivyo; walizungumza kwa ukali sana na wengine tulishangaza na kauli za baadhi ya wabunge hao wa CCM ambazo zilionesha wazi kuwa walikwua na tatizo na wizara hiyo na hata Waziri wake Bw. Omar Nundu.

  c. Likaja suala la David Jairo - ambalo ukiangalia sana unaweza kuona kabisa kuwa linashambulia sehemu zote mbili; kwanza linashambulia upande wa wizara na pili upande wa Ikulu. Sasa maendeleo ya leo Bungeni yanatudhihirishia kuwa wapo wabunge wa CCM ambao kweli wanatofauti na serikali. Ni lazima iwe ni tofauti na serikali kwani naogopa kusema kuwa ni personal.

  CAG aliitwa kufanya uchunguzi akafanya na akatoa ripoti yake kuwa hakuna utaratibu uliokiukwa na Ikulu kwa kutegemea taarifa ya CAG wakaamua kutangaza wanamrudisha Jairo kazini. Hili likanikumbusha jinsi CAG alivyoisafisha benki kuu kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kwenye ujenzi wa nyumba za magavana. Kwa wanaokumbuka pamoja na uzito wa jambo lenyewe CAG aliaminiwa kutoa taarifa na aliposema kuwa "value for money standard" na kuwa "hakuna taratibu iliyokiukwa" tukaambiwa tukubali kwani ulikuwa ni uchunguzi huru. Sasa CAG huyu huyu ameisaifisha serikali watu hawataki!

  Well, haiwezekani wakatae na wakabakia. Hivyo lazima kuna matokeo na matokeo lazima yawe mazito vile vile.

  a. Pinda kwa upande wake ameachiwa uamuzi mmoja tu. Kama alimshauri Rais Kikwete kuwa Jairo afukuzwe na kama aliamini kabisa kuwa - kutokana na taarifa alizokuwa nazo - kuwa Jairo hakupaswa kuendelea basi hawezi kubakia Waziri Mkuu tena. Nyerere aliweka standard kwenye sakatala la Tanganyika, Mwinyi na Mzee Malecela. Alisema Waziri Mkuu huwezi kumshauri Rais kitu naye akakataa halafu ukarudi na kumshauri kitu kingine juu ya jambo lile lile tena kwenye mambo ya msingi. Akasema Waziri Mkuu ukimshauri Rais jambo na amekataa na unajua uko sahihi unatakiwa kujiuzulu ili Waziri Mkuu mwingine aje na kutoa ule ushauri mwingine. Pinda, NI LAZIMA AJIUZULU kama aliamini msimamo wake wa awali kuhusu Jairo ulikuwa sahihi - na bila ya shaka akijiuzulu na baraza la mawaziri litavunjika.

  b. Kikwete anaachiwa uchaguzi mmoja tu. Tayari Bunge limeonesha kutokuwa na imani na teuzi zake na maamuzi yake. Sina tatizo na wabunge wa upinzani kuonesha kutokuwa na imani huko lakini wabunge wa chama chake mwenyewe wanapofanya hivyo ni lazima arudishe nidhamu au awape matokeo. Nyerere tena alionesha kiwango; wakati fulani Bunge lilipomkatalia kupitisha mswada wake aliwaambia wazi kuwa ni jukumu lao kufanya hivyo lakini wakifanya hivyo basi atavunja Bunge waweze kurudi kwa wananchi. Ninaamini, wakati umefika kwa Kikwete kuwaambia wabunge wake kuwa yuko tayari kuvunja Bunge kama wabunge wake hawawezi kufanya kazi na serikali yake ili warudi kwa wananchi.

  Bila ya shakahilo ni gumu kwani kwa kuvunja Bunge na yeye mwenyewe atatakiwa kurudi kugombea tena; swali litakuwa ni nani atarudi Bungeni au Ikulu. kama kweli wabunge wa CCM wanaamini serikali ina matatizo na hawana imani hivyo nayo basi wawe tayari kukutana na matokeo ya msimamo wao huo. Wawe tayari kurudi kwa wananchi. Hivyo Kikwete alitake Bunge kupiga kura ya kuwa na imani na waziri Mkuu au la. VEry simple. Kama wabunge wa CCM hawana imani na serikali yake watampigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na hivyo Waziri Mkuu atatakiwa kujiuzulu; na Waziri Mkuu akijiuzulu Kikwete atangaze kuvunja Bunge kwani hawezi kuchagua baraza kutoka kwa wabunge wale wale na hivyo kama wanataka kuanza upya yuko tayari kuanza upya kabisa na uchaguzi mpya.

  Ninachosema ni kuwa lazima kuwe na matokeo!!
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Nitakuwa wa kwanza kushangaa kama Pinda hata jiuzulu kutetea na kulinda hadhi yake
   
 3. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nadhani ni wakati mwafaka kwa pinda kulinda imani yake kwa wananchi kwa kujiuzulu maana hawezi kutetea jambo ambalo ni gumu kwake
   
 4. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Isingekuwa Tanzania ningeshangaa!Na sitashangaa kuona watu hawashangai maana hakuna cha kushangaa kwene nchi ya mazoea!
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii vita ya magamba tu.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  MM, Things Fall Apart.......

  Kuna mambo ambayo hayapo sawa huko serikalini na sasa wabunge wamegundua kuwa kuendelea kuitetea serikali yao ni kujimaliza mbele ya umma na wao wanapaswa kuamua ama kuwa wabunge kwa kipindi cha mwisho kwa kuendelea kuitetea serikali ama kuwa kinyume nayo ili waweze kuaminika kwa wananchi.

  Kuna Mbunge mmoja wa CCM aliwahi kuniambia kuwa kuwa CCM ni mzigo sana haswa pale wanapopangiwa nini wakisema na nini wasikiseme na kwa hili niliwahi kuona nyaraka waliyopewa wabunge wa CCM jinsi ya kuchangia bajeti na inaitwa mwongozo wa kucahngia bajeti.....

  Hili la Jairo, ni wazi kuwa Pinda anapaswa kuamua kama alishatoa hukumu ndani ya buinge leo anaambiwa kuwa hukumu yake haikuwa na mantiki je? ataweza kumpa maagizo Jairo tena? Je? Jairo atakuwa tayari kupokea maagizo ya waziri mkuu aliyekwisha mhukumu bila hata kumsikiliza ?

  Hii inapeleka ujumbe gani kwa watumishi wa umma ,je?ni kuwa waziri mkuu anakurupuka katika kutoa maamuzi juu ya masuala magumu mbalimbali?
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Pinda ajiuzulu tu.maana atakuwa haaminiki tena.Haya ni maneno.ila uamuzi ni wake
   
 8. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  pinda akijiuzuru na mimi najiuzuru kuwa ntu
   
 9. u

  utantambua JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Utashangaa Hili nalo litapita kama mengine yalivyopita na maisha bado yakaendelea chini ya magamba
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  asante Mwanakijiji kwa makala safi.
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Any way tunaweza kujaribu kujenga hoja nzuri hapa kuwa PM ajiuzulu sawa, lakini lakini tujiulize kila anacho shauri PM lazima Rais akifuate?
  Si mtetei PM kama mtu safi lakini siioni pia hoja nzito ya kumfanya ajiuzulu ati kwasabubu rais hajafata ushauri wake.
  Najua tunapenda kuchukua maneno ya Hayati Nyerere kama msaafu, lakini yeye alifuata kila ushauri aliopewa na ma PM wake?
  Kuna mambo mengi mno Rais anayoshauriana na PM wake na wasahauri wengine, tena wakati mwingine yanakuwa ya kuvutana hoja lakini mwisho wa siku lazima waje na kitu kimoja.
  La JK sina tatizo nalo anapaswa kujipima
   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Moja ya shughuli kuu mara tu baada ya wabunge kuanza kikao cha kwanza katika mwaka wa kwanza kati ya mitano ni Serikali ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kuwadhamini ili waweze kuchukua mikopo mikubwa inayolingan na misha hara na posho zao za miaka mitano. Na wengi wao wamechukua achilia mbali mikopo ya magari ambayo mlazima wailipe kwa maika mitano. Huu huwa ni mkakati maalum wa kuwabana wabunge washindwe kutofautiana na serikali iliyoko madarakani. Jeuuri wanayoonyesha akina Luhanjo inatokana na ukweli huu, wanajua wabunge hawako tayari kupiga kura ya kutokuwa na imani ili rais avunje bunge na mabenki walikochukua mikopo yakamate magari na nyumba zao. Hivyo hizi ni blah blah kama zile Spika Sitta alivyozima mjadla wa Richmond alipoona nafasi yake ya uspika iko hatarini.
   
 13. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ana hadhi gani ya kutetea?
   
 15. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji thanks kwa makala nzuri, ila nchi yetu ilipofikia ni pagum kwa kweli, kuhusu Pinda nadhani anatakiwa tu kujiondoa hapo kwenye serikali hii inayotetea mafisi ili kuzidi kujenga heshima yake na uaminifu ktk kazi alonayo, lakini kwa bongo hii sijui maana Pinda aliekuwa analia zamani bungeni sio huyu wa sasa keshaharibiwa na magamba wenzake (ameshakuwa mwanasiasa)
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lakni JK mwenyewe aliwaaambia katika hotuba yake moja hataki wabunge wa ndio mzeee . Kama maneno yale aliyasema kutoka moyoni basi naye atakuwa anafurahi.......

  Nadahni kwa sasa comedy ya wabunge inazidi rating hata ile the comedy ya kina joti .
   
 17. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama siku ile alilia pale alipoambiwa ajiuzulu kwa kutamka kuwa auwae Albino na yeye auwawe, itakuwa hii kujiuzulu bila shinikizo! Alikuwa Mtoto wa Mkulima, alipoona utamu wa madaraka akatangaza sekta rasmi mpya ya Ombaomba pale Bungeni. Mtu kama huyu ambaye ni Opportunist unategemea atajiuzulu kwa kulinda hadhi yake!
  Siku akijiuzulu tu mimi nitachukuwa maamuzi magumu kwa kujiita Mbunge wa CCM pale mtaani bila kuogopa kuchekwa na wenye akili zao.
   
 18. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...
  Hakuna Serikali 'huko'...ni 'mkusanyiko wa wajaza nafasi' au kwa uwazi zaidi ni kuwa viongozi wa serikali ni mithili 'vizibo vyo madebe yaliyo matupu, yaani yaliyojaa utupu -'ombwe'...hivyo debe halitaacha kutwika..., ila mifuniko itaning'inia tu kuziba uwazi, na sio kufanya debe liwe na ujazo 'content' yoyote kwani wao wenyewe wameziba chochote kisiingie, au hata 'utupu' uliopo usiwe na wa kuujaza...!

  Kwa hiyo PM ni kinara wa 'utupu' wenyewe na ndio kizibo kikuu, hivyo kuondoka kwake hakupo ktk picha maana hakuna wa kuona lolote la yeye kumhitaji aondoke, maana mwenyewe 'haoni' tena. Amebaki 'mtoto wa mkulima ombwe!'

  Tuna kazi sana...tumngoje 'malaika wa bwana' atashuka siku sii nyingi kuondoa utupu hii....

  'Shaloom....Amani iwe kwenu'
   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu Paulss,
  Naomba nitofautiane kidogo tu na wewe. Kuna vitu viwili umechanganya pamoja.
  Kwanza kuna majadiliano kati ya PM na president. There you can argue with each other. Mtabishana hata masaa kumi halafu mwisho mnakubaliana jambo hilo.
  Hata ktk baraza la mawaziri kuna kudebate issues na kufikia mwafaka. Mnapokuja public your always one thing. One government with the same vision- There is collective responsibility.
  On the other hand, when you show the difference in public, ni kitu kingine kabisa. Kwa sababu mnatazamwa na watu wa uelewa tofauti kabisa. Mnaondoa kabisa public confidance. Mnaondoa heshima yenu. In this case, lazima Pinda atapoteza heshima yake bungeni na serikalini na mbaya zaidi atapoteza imani yake kwa wananchi.
   
 20. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu MKJJ, hakuna ubishi kwamba LAZIMA KUWE NA MATOKEO!

  LAZIMA pia kuwe na matokeo yanayohusu MADUDU lukuki yaliyotendwa na SERIKALI iliyopo madarakani. Hapa ndipo napata kigugumizi. Watu wamesheheni zigo kubwa tu la ufukara na yatokanayo na hilo. Kila kukicha wanakumbana na MADUDU MAPYA. Order of the day. Watu wengi wanajua hilo. MATOKEO yanayohitajika yanafahamika. Sio siri hata kidogo. Matokeo hayajileti yenyewe. Kazi kwelikweli hapo.
   
Loading...