Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
ndoto nyingine nguvu kusadikika
Pinda hawezi kujuuzuru magamba kwa kujikausha usipime
Pinda hawezi kujuuzuru magamba kwa kujikausha usipime
Nitakuwa wa kwanza kushangaa kama Pinda hata jiuzulu kutetea na kulinda hadhi yake
Na. M. M. Mwanakijiji
Wabunge wa CCM wanagongana na serikali yao. Wanainyanyasa na kuimbua mbele za watanzania. Nimewahi kuandika huko nyuma kuwa ni jukumu la upinzani kudhoofisha serikali iliyoko madarakani ili ianguke na hata ikibidi ilazimike kuitisha uchaguzi mapema (early election). Nikasema wakati ule kuwa siyo jukumu la upinzani kuisaidia CCM kutawala. Sasa kinyume cha hilo nacho ni kweli. Jukumu la wabunge wa CCM ni kukitetea chama chao na hasa serikali yao isije kuanguka.
Kwa miezi ya karibuni sasa wabunge wa CCM wanaonekana kuwa na mgongano na serikali yao. Maneno yao makali na hata misimamo mikali dhidi ya mawaziri wa serikali hiyo ni mashambulizi ya wazi, dhahiri na yaliyopangwa. Upande mmoja ni wazi wapo ambao wanafanya hivyo kama sehemu ya political triangulation lakini wapo pia wanaofanya hivyo kama sehemu ya tofauti ya msingi kati yao na chama chao. Ni hawa wa kundi la pili ndio ambao hasa nawazungumzia kwani wale wengine wanafanya kwa ajili ya kugeresha wapinzani na kuwahadaa watanzania ili CCM izidi kutawala.
Hata hivyo kwa kundi hilo la pili ambalo kweli lina tofauti za msingi na serikali yao na wameonekana kuwa na uadui wa wazi na baadhi ya watendaji wa serikali (open hostilitiy) hawawezi kuwa hivyo bila kuwa na matokeo. Nina maana ya kwamba wabunge wa chama tawala wanapoamua kugongana na serikali yao kwa kuonesha kutokuwa na imani nayo basi lazima wawe tayari kuishi na matokeo ya msimamo huo.
a. Walipoamua kukataa bajeti ya Wizara ya nishati na Madini kwa maneno makali hadi kulazimisha serikali kuiondoa walionesha kutokuwa na imani na serikali. Kwamba, hawakuamini serikali ingeweza kuleta bajeti nzuri na yenye manufaa kwa wananchi na jinsi walivyomshambulia Ngeleja - mteuliwa wa RAis - walijionesha wazi kuwa wana matatizo na Kikwete mwenyewe.
b. Ilipokuja bajeti ya Uchukuzi navyo ilikuwa hivyo hivyo; walizungumza kwa ukali sana na wengine tulishangaza na kauli za baadhi ya wabunge hao wa CCM ambazo zilionesha wazi kuwa walikwua na tatizo na wizara hiyo na hata Waziri wake Bw. Omar Nundu.
c. Likaja suala la David Jairo - ambalo ukiangalia sana unaweza kuona kabisa kuwa linashambulia sehemu zote mbili; kwanza linashambulia upande wa wizara na pili upande wa Ikulu. Sasa maendeleo ya leo Bungeni yanatudhihirishia kuwa wapo wabunge wa CCM ambao kweli wanatofauti na serikali. Ni lazima iwe ni tofauti na serikali kwani naogopa kusema kuwa ni personal.
CAG aliitwa kufanya uchunguzi akafanya na akatoa ripoti yake kuwa hakuna utaratibu uliokiukwa na Ikulu kwa kutegemea taarifa ya CAG wakaamua kutangaza wanamrudisha Jairo kazini. Hili likanikumbusha jinsi CAG alivyoisafisha benki kuu kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kwenye ujenzi wa nyumba za magavana. Kwa wanaokumbuka pamoja na uzito wa jambo lenyewe CAG aliaminiwa kutoa taarifa na aliposema kuwa "value for money standard" na kuwa "hakuna taratibu iliyokiukwa" tukaambiwa tukubali kwani ulikuwa ni uchunguzi huru. Sasa CAG huyu huyu ameisaifisha serikali watu hawataki!
Well, haiwezekani wakatae na wakabakia. Hivyo lazima kuna matokeo na matokeo lazima yawe mazito vile vile.
a. Pinda kwa upande wake ameachiwa uamuzi mmoja tu. Kama alimshauri Rais Kikwete kuwa Jairo afukuzwe na kama aliamini kabisa kuwa - kutokana na taarifa alizokuwa nazo - kuwa Jairo hakupaswa kuendelea basi hawezi kubakia Waziri Mkuu tena. Nyerere aliweka standard kwenye sakatala la Tanganyika, Mwinyi na Mzee Malecela. Alisema Waziri Mkuu huwezi kumshauri Rais kitu naye akakataa halafu ukarudi na kumshauri kitu kingine juu ya jambo lile lile tena kwenye mambo ya msingi. Akasema Waziri Mkuu ukimshauri Rais jambo na amekataa na unajua uko sahihi unatakiwa kujiuzulu ili Waziri Mkuu mwingine aje na kutoa ule ushauri mwingine. Pinda, NI LAZIMA AJIUZULU kama aliamini msimamo wake wa awali kuhusu Jairo ulikuwa sahihi - na bila ya shaka akijiuzulu na baraza la mawaziri litavunjika.
b. Kikwete anaachiwa uchaguzi mmoja tu. Tayari Bunge limeonesha kutokuwa na imani na teuzi zake na maamuzi yake. Sina tatizo na wabunge wa upinzani kuonesha kutokuwa na imani huko lakini wabunge wa chama chake mwenyewe wanapofanya hivyo ni lazima arudishe nidhamu au awape matokeo. Nyerere tena alionesha kiwango; wakati fulani Bunge lilipomkatalia kupitisha mswada wake aliwaambia wazi kuwa ni jukumu lao kufanya hivyo lakini wakifanya hivyo basi atavunja Bunge waweze kurudi kwa wananchi. Ninaamini, wakati umefika kwa Kikwete kuwaambia wabunge wake kuwa yuko tayari kuvunja Bunge kama wabunge wake hawawezi kufanya kazi na serikali yake ili warudi kwa wananchi.
Bila ya shakahilo ni gumu kwani kwa kuvunja Bunge na yeye mwenyewe atatakiwa kurudi kugombea tena; swali litakuwa ni nani atarudi Bungeni au Ikulu. kama kweli wabunge wa CCM wanaamini serikali ina matatizo na hawana imani hivyo nayo basi wawe tayari kukutana na matokeo ya msimamo wao huo. Wawe tayari kurudi kwa wananchi. Hivyo Kikwete alitake Bunge kupiga kura ya kuwa na imani na waziri Mkuu au la. VEry simple. Kama wabunge wa CCM hawana imani na serikali yake watampigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na hivyo Waziri Mkuu atatakiwa kujiuzulu; na Waziri Mkuu akijiuzulu Kikwete atangaze kuvunja Bunge kwani hawezi kuchagua baraza kutoka kwa wabunge wale wale na hivyo kama wanataka kuanza upya yuko tayari kuanza upya kabisa na uchaguzi mpya.
Ninachosema ni kuwa lazima kuwe na matokeo!!
Pinda hawezi kujiuzulu na Bunge la chama chake likabakua . Akijiuzulu LAZIMA Kikwete avunje na bunge ili wote waanze upya.
Nilitaka kuuliza hivi piaMbona alipojiuzulu Lowassa Rais hakuvunja Bunge?
Lakni JK mwenyewe aliwaaambia katikahotuba yakemja hataki wabunge wa ndio mzeee . Kama mamneno yale aliyasema kutoka moyoni basi naye atakuwa anafurahi.......
Nadahni kwa sasa comedy ya wabunge inazidi rating hata ile the comedy ya kina joti .
Nitakuwa wa kwanza kushangaa kama Pinda hata jiuzulu kutetea na kulinda hadhi yake
<br />Nitakuwa wa kwanza kushangaa kama Pinda hata jiuzulu kutetea na kulinda hadhi yake