Wabunge matajiri wafanyabiashara, wanasimamia Maslahi ya akina nani bungeni?

Nchi hii ni ya watu wote sio ya wakulima ba wafanyakazi tu ni ya wote wakiwemo wafanyabishara ambao ndio walipa kodi wakubwa kuliko hao wakulima na wafanyakazi Hao ndio wenye TRA hasa.Mkulima anachangia shilingi ngapi kwenye kodi ya taifa ? Au mfanyakaxi wa serikali ana mchango gani wa maana TRA sababu hata mshahara wake tu anategemea serikali ikusanye kodi kwa wafanyabiashara ndio alipwe .Niwafa kupe tu.mnyonyaji wa kodi za wafanyabiashara

Mleta mada unatakaje hutaki walipa kodi wakubwa wawepo bungeni wajae wala kodi kodi?

Wapi kwa maslahi ya kodi zao wanalupa na maslahi ya kusimamia kodi wanalipa huko bungeni na pia kusimamia maslahi ya wafanyabiashara wenzao na wananchi wao
 
Tuangalie akili na wenye Nia ya kututumikia.
Si ccm wala huko kwingine, sasa hivi wote wapo kulinda matumbo yao. Nani alitegemea Halima Mdee siku moja angeisaliti chadema!

Kuna padri mmoja Dar miaka ya nyuma kidogo alisema sasa hivi ni ngumu sana kumpata mtanzania mwaminifu.
 
Tuongeze UKWELI,

Halima Mdee haikuwa Kwa hiari yake, nguvu iliyotumika kuwaingiza wamama wale CCM Si pesa pekee,

Uliwahi kuwekewa shingoni Ile CHUMA ya baridi?

Muulize Wenje kilichomkuta pale Jiji.

Tupambanie Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote,tuondoke kuwategemea WANADAMU wanaobadilika.
 
Salaam,Shalom!!

Zamani, mwalimu wa Shule ya msingi, alikuwa na uwezo wa kuchukua fomu na kugombea ubunge na akashinda, sasa hivi akijaribu, atakutana na kikumbo Cha tajiri au .toto wa kiongozi mkubwa serikalini na kutupwa mbali.

Kuwa tajiri Kwa halali Si DHAMBI, Hilo liwekwe wazi. Na mada Haina Chuki na matajiri wa halali wenye uchungu na Umaskini wa wananchi.

Wananchi tunajiuluza hivi ;

1. Mfanyabiashara tajiri mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anagombea ubunge na kuacha kusimamia biashara zake Ili akae bungeni na kulipwa 80,000 Kwa siku, ni ana mapenzi na wananchi au Kuna nini nyuma yake?

2. Mmiliki wa mabasi zaidi ya 50 Nchi nzima, anafuata nini bungeni? Na ikiwa anatetea maslah ya Wananchi, mbona nauli hazishuki?

3. Tukitafuta wauza magenerator wakubwa nchini, hutawakosa bungeni, tunajiuluza, bungeni Huwa wanakwenda kutetea Maslahi ya nani? Na ikiwa wanatetea maslah ya biashara zao, mgao wa UMEME utakuja kuisha Kweli?

4. Tukichunguza Kwa makini, waagizaji wakubwa wa MAFUTA, SUKARI nk nk wamo bungeni, najiuliza ipo siku SUKARI itashuka Bei, au MAFUTA yatakuja kushuka Bei Kweli? Tufanye nini Ili kupata watetezi wa Maslahi ya wananchi wa Kweli?

5. Kitu Gani Hasa kinawavuta matajiri kutaka nafasi za udiwani na Ubunge ambazo kimsingi posho zake ni kiduchu kulinganisha na mapato ya biashara zao?

Ikiwa wabunge wanaomiliki vituo vya mafuta Nchi nzima Wana mapenzi ya dhati, kwanini wasishirikiane kujipunguzia faida kidogo Ili mafuta yashuke Bei Ili sie wapiga kura tufurahie?

Yaani saiz sukari inauzwa 5000, kwanini wabunge matajiri wasipambane kuhakikisha tunanunua SUKARI Kwa Bei ya 2,000 per kg ikiwa Kweli wanasimamia Maslahi ya maskini?

Karibuni 🙏
Bila KODI hakuna serikali na bila WAFANYABIASHARA hakuna KODI kwa hiyo WAFANYABIASHARA ndio serikali.

Bunge ni chombo cha uwakilishi kinapaswa kiwe na kila aina ya mtu katika jamii.

Kama unadhani sifa yako ya vidigrii ndiyo pekee yake inatakiwa ili uende bungeni imekula kwako- jiunge na group la whtsapp
ACHA WIVU, ROHO MBAYA NA AKILI MBOVU
 
Mwalimu ana hela ya kufanya kampeni?
Halafu huyo mwalimu mlipa kodi mdogo sana anaenda kufuata nini bungeni .Kikodi chenyewe anacholipa kidogo.Kamshahara kake tu kanategemea hela ya walipa kodi wakubwa walipe ndipo yeye apate mishahara
Bunge haliwezekani wajazwe wala kodi tu

Kwanza inabidi serikali itumie taarifa za TRA kuamua nani agombele. BUNGE Kujaa maskini kuliletea nursing taifa.Ziangaliwe ripoti za TRA halafu mlipa kodi mkubwa ndie apewe nafasi ya kugombea.Tuachane na kujaza malofa bungeni waishia tu kupiga makofi na vigelegele
 
Bila KODI hakuna serikali na bila WAFANYABIASHARA hakuna KODI kwa hiyo WAFANYABIASHARA ndio serikali.

Bunge ni chombo cha uwakilishi kinapswa kiwe na kila aina ya mtu katika jamii
ACHA WIVU, ROHO MBAYA NA AKILI MBOVU
Hujajibu swali,

Mtu mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anafuata nini bungeni?

Ikiwa anawapenda wananchi, mbona hapendekezi Kodi ishuke Ili mafuta yawe chini, na Yeye apunguze Bei Ili kunufaisha waliompigia kura?

Jibu hayo kwanza.
 
Halafu mlipa kodi mdogo sana anaenda kufuata nini bungeni .Kikodi chenyewe anacholipa kidogo.Kamshahara kale tu kanegemea hela ya walipa kodi wakubwa walipe ndipo yeye apate mishahara
Bunge haliwezekani wajazwe wala kodi tu

Kwanza inabidi serikali itumie taarifa za TRA kuamua nani agombele. BUNGE Kujaa maskini kuliletea nursing taifa.Ziangaliwe ripoti za TRA halafu mlipa kodi mkubwa ndie apewe nafasi ya kugombea.Tuachane na kujaza malofa bungeni waishia tu kupiga makofi na vigelegele
Nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi,

Tukitajirika, tutajirike pamoja.
 
Hujajibu swali,

Mtu mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anafuata nini bungeni?

Ikiwa anawapenda wananchi, mbona hapendekezi Kodi ishuke Ili mafuta yawe chini, na Yeye apunguze Bei Ili kunufaisha waliompigia kura?

Jibu hayo kwanza.
siwezi kujibu swali la kijinga kama hilo; na kimsingi mtu yeyote akikujibu mshukuru mungu wako.
Kama unadhani sifa yako ya vidigrii ndiyo pekee yake inatakiwa ili uende bungeni imekula kwako- jiunge na group la whtsapp na wenye digrii wenzako
 
Pesa anatakiwa apate Kutoka michango ya wanachama chamani!!

Utaratibu wa kutumia pesa yake kufanya compaign, atazirudishaje?

Bungeni Kuna biashara Gani?
Unadhani kampeni inafanywa kwa maneno? Mkuu ukiona mtu yuko bungeni ujue si chini 300,000, 000/= tshs zimeenda. ni Tanzania kura inapigwa ama kwa fedha au kwa chuki iala chuki nayo inatengenezwa na fedha
 
siwezi kujibu swali la kijinga kama hilo; na kimsingi mtu yeyote akikujibu mshukuru mungu wako.
Kama unadhani sifa yako ya vidigrii ndiyo pekee yake inatakiwa ili uende bungeni imekula kwako- jiunge na group la whtsapp na wenye digrii wenzako
Ndugu comte hakuna swali la kijinga, Kuna jibu la kijinga.

Nimekuuliza, mtu mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anayemiliki migodi, bungeni anaenda kufanya nini?
 
Ikiwa hili ndilo jibu,

Umma wa wananchi Walio wengi wakulima na wafanyakazi, wamchague viongozi watakaokwenda kupigana Maslahi ya wananchi ,Si maslah binafsi.

Tuwe macho uchaguzi ujao 2024&2025.
Binafsi naona kwa huu ulimwengu wa kidigitali kazi ya ubunge haina maana yoyote kwa mwananchi zaidi ya kuongeza mzigo kwa walipakodi. Wanatuwakilisha kwenye kula keki ya taifa na sio vinginevyo.
 
Ndugu comte hakuna swali la kijinga, Kuna jibu la kijinga.

Nimekuuliza, mtu mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anayemiliki migodi, bungeni anaenda kufanya nini?
Bunge ni sehemu ya kutoa mawazo, ushauri na kuwalisha watu bila kujali hali ya huyo mtu
 
Unadhani kampeni inafanywa kwa maneno? Mkuu ukiona mtu yuko bungeni ujue si chini 300,000, 000/= tshs zimeenda. ni Tanzania kura inapigwa ama kwa fedha au kwa chuki iala chuki nayo inatengenezwa na fedha
Sasa mfanyabiashara ni LAZIMA alinganishe faida na HASARA.

Alitumia b2 kwenye kampeni, atafanya biashara Gani bungeni Ili kurudisha HASARA hiyo ikiwa posho za bungeni ni ndogo?

Matajiri na wafanyabiashara wakubwa, bungeni wanakimbilia nini Hasa?
 
Utaona,

Ni Rahisi hayo Kutokea ikiwa wanagombea kupitia upinzani.

Chama tawala kutoboa labda uwe mtoto wa kiongozi mkubwa.
upinzani hela zinatoka ujerumani na kwa waathirika kama Lowassa
 
Sasa mfanyabiashara ni LAZIMA alinganishe faida na HASARA.

Alitumia b2 kwenye kampeni, atafanya biashara Gani bungeni Ili kurudisha HASARA hiyo ikiwa posho za bungeni ni ndogo?

Matajiri na wafanyabiashara wakubwa, bungeni wanakimbilia nini Hasa?
Hakuna faida kama haiba, hadhi, na utukufu- VISA anaipata haraka sana
 
Bunge ni sehemu ya kutoa mawazo, ushauri na kuwalisha watu bila kujali hali ya huyo mtu
Sasa kama ni sehemu isiyo na faida,

Kwanini utumie ml 300 kwenye mkutano wa kuomba kura?

Unamaanisha watu hao hawana akili, au wanatupenda sana wananchi?
 
upinzani hela zinatoka ujerumani na kwa waathirika kama Lowassa
Na za CCM zinatoka mfukoni upi?

Mimi sijataja chama, naongelea wabunge matajiri na wafanyabiashara wakubwa.

Karibu.
 
Na za CCM zinatoka mfukoni upi?

Mimi sijataka chama, naongelea wabunge matajiri na wafanyabiashara wakubwa.

Karibu.
Hakuna mgombe nchi hii anapewa hela ya kampeni na chama chake.
Nchi hii huwezi kupata kura bila kutoa hela hata kanisani
Kuwashobokea matajiri ni akili ya hovyo na ubaguzi- kosa lao ni lipi?
 
Back
Top Bottom