Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
 
Kwa hali ilivyo sasa kutoboa Marekani ni vigumu sana. Haki za mfanyakazi ni ndogo na pia mfumo wa bima ya afya ni mbovu. Ujerumani ni nchi nzuri sana lakini mpaka uje ujiseti inabidi upate cheti cha huku huku na ujue lugha. Huku malipo yako poa na mfanyakazi unalindwa sana.

Kwa kumalizia mimi naona ukishafanya kazi kwa miaka mitano ukawa na experience ya kutosha kwenye field yako Bora urudi Bongo. Maana kama una mtaji unaweza hata ukaanzisha biashara yako.
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Wamekuudhi mkuu, umeamua kuwachamba
Ila hata mimi uwa sishobokei nchi zenye waafrika wengi kwani zinakuwa na kshifa nyingi kutuhusu
Wizi, fujo, uuzaji wa madawa na utaperi
Tunakuwa hatuaminiki, na hata ukimsogelea mzungu anahisi unataka kumuibia
Hapo uwa napakumbuka sana afrika nauwaza uhuru wangu na hakuna wa kunibagua au kuninyanganya haki yangu na ninakuwa na sauti imara tofauti na kuomba haki
Naipenda afrika shida maendeleo tu, ambayo yameshikwa na viongozi wetu
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Hakuna sehemu yenye maisha rahisi. Narudia tena hakuna sehemu rahisi yenye maisha rahisi... Labda ubaki Bongo uwe chawa wa mama Samia ila ujue nako kuna ugumu wake. Inabidi uwe mpiga kelele kweli kweli na ujitoe akili zako.
 
Wamekuudhi mkuu, umeamua kuwachamba
Ila hata mimi uwa sishobokei nchi zenye waafrika wengi kwani zinakuwa na kshifa nyingi kutuhusu
Wizi, fujo, uuzaji wa madawa na utaperi
Tunakuwa hatuaminiki, na hata ukimsogelea mzungu anahisi unataka kumuibia
Hapo uwa napakumbuka sana afrika nauwaza uhuru wangu na hakuna wa kunibagua au kuninyanganya haki yangu na ninakuwa na sauti imara tofauti na kuomba haki
Naipenda afrika shida maendeleo tu, ambayo yameshikwa na viongozi wetu
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!
 
Back
Top Bottom