Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
10,952
23,095
Moja kwa moja.

Inakera sana unakuta upo kibanda umiza mnaangalia mechi mtu anaanza kushangilia goli kabla ya mpira kuingia wavuni au mtu anahadithia tukio la mbele kabla kutokea wakati mechi inaendelea.

Watu wa namna hii nashinda kuwatafsiri kichwani mwao kupo vipi, natamani niwatandike makofi kabisa. Kama wanapenda kusikiliza mpira redioni bora wangekuwa wanabaki makwao kuliko kuwaharibia ladha ya mpira wenzao.
 
Wanakera sana ila kuna mabanda wanakua strict kabisa na hiyo issue. Hairuhusiwi kusikiliza radio kwa loudspeaker. Na ukiamua kusikiliza kwa earphones basi usiwe na kiherehere cha kutoa updates.

Hawa ni aina ya watu wanaopenda kuonekana wao ndo wa kwanza kupata habari fulani. Ni aina fulani ya insecurity
 
Ata uwanjani wapo ambao wanakuwepo ila wanasikiliza radioni
Uwanjani haina impact kwasababu redio inakuwa inaenda sawa na kile kinachoonekana uwanjani

Ila kama una stream au kuangalia kwenye TV, redio hua mbele ya muda kuzidi TV.

Mabanda umiza ya kitaa mengi yamepiga marufuku kusikiliza redio ukumbuni
 
Kuna jamaa tulikuwa naye uwanjani sijui alikuwa anasikiliza redio gani ile...yani alikuwa anashangilia kabla ya goli, na kweli huku nyavu zinatikisika
 
Back
Top Bottom