Wabongo waishio majuu kwa sifa!!?

Wabongo waishio majuu kwa sifa!!?

MillionHairs

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
803
Reaction score
406
Jamani tuache utani baadhi ya Wabongo (waTanzania) waishio nje ya nchi wanamisifa usipime.

Yaani kama umebahatika kutembelea nchi za UK na USA au nchi zinazofanana na hizo nchi basi utanielewa ninachotaka kuongelea hapa…wakiwa wabongo kwa wabongo wanapenda sana kuzu ngumza kiswahili na sana sana wakikutana na mtu wa nyumbani (Tanzania) ambaye amekwenda au umekwenda kwa shughuli zako maramoja basi ndiyo kabisaaa yaani wakikuona tu wanapenda
sana kuzungumza au kuongea kiswahili na wewe.

Ila cha ajabu na kushangaza mtu huyo huyo au watu hao hao warudipo bongo kuja kusalimia ndugu au kwa majukumu fulani fulani basi hawataki au hataki kabisa kuzungumza kiswahili na badala yake anaongea ung'eng'e kuanzia mwanzo hadi mwisho au maneno 10 ung'eng'e na mawili kiswahili.

Sasa mimi najiuliza inakuwaje unapokuwa nchi za ung'eng'e unapenda kuongea lugha ya nyumbani kwenu Tanzania alafu ukirudi Bongo kwa mapumziko ya wiki mbili au mwezi hutaki kuongea kiswahili.

Ukienda shopperz plaza unajifanya yes no,mlimani city yes no,kwenye daladala yes no ukikutana na washikaji zako wa kitambo yes no nk nk nk.

Sasa hii yote ni nini? ni ushamba au ndiyo unataka tujue kuwa unatoka USA au Ulaya?

Ama kweli baadhi ya wabongo waishio majuu kwa misifa!!?
 
Kule hawawezi kuongea kiengereza chao hicho cha Yes, no kwasabubu ndio kwa wenyewe kwhyo bora wajivunie lugha yao tu, ila wakiwa hapa kwa vipofu wenzao akina sis dah! Tabu kweli si unajua chongo ndio kiongozi kwenye nchi ya vipofu, ila kuna wabongo wanaongea kiengereza utafkiri wamemeza kitoto cha kizungu
 
Ingawa unachosema ni kweli, mimi nasema si wabeba maboksi wote ambao wako hivyo.

Na nisiende mbali. Mimi hapa prezdaa wa wabeba maboksi nikijaga vekesheni bongo huwa sipendi kabisa hata kuongea hicho Kiswahili. Kizungu ndo huwa nakitupa kule.

Kisukuma ndo huwa nakitumia sana na zaidi. Najua mwaweza msiniamini lakini ukweli ndo huo. Ni Kisukuma mwanzo mwisho tena kile cha Ntuzu kabisa.

Lekagi gete ugunigushela unene Nzagamba Ng'wanagingili u Ikungulyabashashi.
 
Good Morning prezdaaa.
 
Jamani tuache utani baadhi ya Wabongo (waTanzania) waishio nje ya nchi wanamisifa usipime.

Yaani kama umebahatika kutembelea nchi za UK na USA au nchi zinazofanana na hizo nchi basi
utanielewa ninachotaka kuongelea hapa…wakiwa wabongo kwa wabongo wanapenda sana kuzu
ngumza kiswahili na sana sana wakikutana na mtu wa nyumbani (Tanzania) ambaye amekwenda
au umekwenda kwa shughuli zako maramoja basi ndiyo kabisaaa yaani wakikuona tu wanapenda
sana kuzungumza au kuongea kiswahili na wewe.

Ila cha ajabu na kushangaza mtu huyo huyo au watu hao hao warudipo bongo kuja kusalimia ndugu
au kwa majukumu fulani fulani basi hawataki au hataki kabisa kuzungumza kiswahili na badala yake
anaongea ung'eng'e kuanzia mwanzo hadi mwisho au maneno 10 ung'eng'e na mawili kiswahili.
Sasa mimi najiuliza inakuwaje unapokuwa nchi za ung'eng'e unapenda kuongea lugha ya nyumbani
kwenu Tanzania alafu ukirudi Bongo kwa mapumziko ya wiki mbili au mwezi hutaki kuongea kiswahili.

Ukienda shopperz plaza unajifanya yes no,mlimani city yes no,kwenye daladala yes no ukikutana na
washikaji zako wa kitambo yes no nk nk nk.

Sasa hii yote ni nini? ni ushamba au ndiyo unataka tujue kuwa unatoka USA au Ulaya?

Ama kweli baadhi ya wabongo waishio majuu kwa misifa!!?

SIFA? wewe unatatizo lako. Jua mtu ukiishi miaka mingi nchi za nje unasaau lugha yako kwa kiasi fulani.
Hivo ukiongea kiswahili lazma uchanganye na lugha ingine, lugha ya ile nchi unayoishi.

Hata maneno ya kijapani au kirusi unaweza kuingiza ktk kiswahili, sio kingereza tu. Kwa mfano mimi najua kijerumani, kidenish, kingereza na kiswahili, nikiwa dar naweza kusikia waswahili akichanganya kishwahii na kijerumani, au kidenish, mimi nawaelewa wanachomaanisha ila waswahili wanakua hawaelewi. Na wale wanajisau kama wapo bongo hivo wanasau kuongea kiswahili sahihi.

Na sio wa majuu tu, mfano
wapare wanachanganya kipare na kiswahili, wamakonde wanaongea kimakonde na kiswahili, na hawa wanapenda sifa pia eti kuonesha wanatoka msumbiji? Au wamasai wanaongea kimasai wakichanganya na kiswahili na hawapia wanapenda sifa au kuonesha wanatoka kenya.

Kuna wengine wanafanya makusudi na kuna wengine wanakua washa zoea kuongea hivo.
 
Lakini, hilo la kutotaka kuongea Kiswahili au la kuchanganya Kiingereza na Kiswahili, kama ni tatizo, basi si tatizo la Wabongo waishio majuu tu.

Kuna wabongo wengi tu ambao hata majuu hawajawahi kufika lakini kila mara hawaishi kuchanganya lugha, hususan wale wasomi wasomi au wale wanaojiona wamesoma soma au wale wanaojiona wako matawi flani kimaisha au wale wanaoiona hiyo lugha ya Kiingereza kuwa ni lugha yenye hadhi ya juu kuliko Kiswahili.

Nani anabisha hilo?
 
Ingawa unachosema ni kweli, mimi nasema si wabeba maboksi wote ambao wako hivyo.

Na nisiende mbali. Mimi hapa prezdaa wa wabeba maboksi nikijaga vekesheni bongo huwa sipendi kabisa hata kuongea hicho Kiswahili. Kizungu ndo huwa nakitupa kule.

Kisukuma ndo huwa nakitumia sana na zaidi. Najua mwaweza msiniamini lakini ukweli ndo huo. Ni Kisukuma mwanzo mwisho tena kile cha Ntuzu kabisa.

Lekagi gete ugunigushela unene Nzagamba Ng'wanagingili u Ikungulyabashashi.

Sio ikungulyandili au ikungulipu?
 
Lakini, hilo la kutotaka kuongea Kiswahili au la kuchanganya Kiingereza na Kiswahili, kama ni tatizo, basi si tatizo la Wabongo waishio majuu tu.

Kuna wabongo wengi tu ambao hata majuu hawajawahi kufika lakini kila mara hawaishi kuchanganya lugha, hususan wale wasomi wasomi au wale wanaojiona wamesoma soma au wale wanaojiona wako matawi flani kimaisha au wale wanaoiona hiyo lugha ya Kiingereza kuwa ni lugha yenye hadhi ya juu kuliko Kiswahili.

Nani anabisha hilo?

Umeua mzee na.kuna ambao wanajua kabisa kuwa watu hawajui kiingereza ila anatumia maneno ya kigeni na kutafsiri yeye mwenyewe;

I mean...its like...sasa unabaki unajiuliza huyu anataka nini hasa
 
Back
Top Bottom