Prof Janabi wa JF
Senior Member
- Jul 7, 2023
- 142
- 417
Faridi Kubanda amejijengea heshima kubwa kwenye muziki wa HipHop Tanzania. Ni mmoja kati ya watu waliowa-influence wadau wengi wa muziki huo.
Mimi napenda muziki ila nasikiliza zaidi hiphop. Na baadhi ya masihi ya Fid Q yalifanya nione wabongo wanaoishi nje ya bongo hawathaminiani kabisa.
Ngoma ya kwanza ambayo Fid Q alionesha kuwa wabongo hawapendani ni ile ngoma ya Wandugu wapenzi, ipo kwenye album Shule ya Xplastaz iliyotoka 2012. Hiyo ngoma ya Wandugu wapenzi ambayo ni ya Xplastaz, Fid Q ft JCB, Fid amechana stanza ya kwanza ambapo amesema
"Wale wanaojifanya wakweli, ndio huwa waongo ile mbaya.
Hawana mchongo washafeli, kama wabongo wa Ulaya"
Hapo ni wazi Fid Q alituambia wabongo wa majuu wamefeli. Tukafurahia mistari maisha yakaendelea. Kwenye ngoma nyingine ya Fid Q ya Sumu, Fid akaongea tena kuhusu wabongo wa majuu kwenye outro ambapo amesema
"Wabongo wa majuu hamna upendo mnajigawa,
Uongo hauna miguu lakini skendo zina mabawa"
Sikiliza hapa
View: https://youtu.be/gR08ZzMZnQE?t=165
Hiyo ni mara ya pili Fid Q anajaribu kuonesha kuwa wabongo wa majuu sio chochote. Nawaza wabongo wa majuu wamemfanya nini Fid Q.
Je, alienda Majuu bila kujua kwa kufikia wana wakamkataa, maana wana wanasaidia kwa kiwango wanachoweza sio kama tunavyoishi bongo.
Mimi najitokeza kusema Fid ameweka chuki zisizo na mpango, wabongo wa majuu wanasapoti sana, kokote mnapokutana mnapiga stori za Tz na mnakuwa ndugu kabisa. Mtu ukikwama jambo wenzako wanasapoti, wanakutafutia michongo nk.
Fid atoke hadharani kusema alikuwa na shida gani na wabongo wa majuu. Nilisikiliza story ya Rama Dee jinsi alivyo na Mr Paul unaona kabisa wana wanasapotiana na kuna roho fulani ya kusapoti sana.
Natamani kuona waandishi wa michezo wanamuhoji Fid Q kwamba ana shida gani na wabongo wa majuu