Quran haijapangwa na wanadamu? Uthman hakupanga Quran yake? Mohamed aliacha printed edition? Kwanini Uthman alichoma Quran zingine ili ibakie yake tu?
Hii ya Misri ya mwaka 1924 mnayotumia leo haikupangwa kwa amri ya mfalme Fuad? Wasomi Wa Al Azhar university hakuzipa majina sura za Quran? Kuna sehemu yeyote Allah alihusika? Hiyo ndiyo Quran ambayo asilimia 90 waislamu mnaikairiri,una uhakika gani ndiyo Quran aliyoshusha Allah?
Swali: Je, Qur’ani “ilipangwa na wanadamu”?
Majibu :
Ndiyo,
ilikusanywa (compiled) na wanadamu —
lakini haikuandikwa au kutungwa na wanadamu.
Tofauti muhimu sana ambayo Mkristo anachanganya:
Uandishi / Wahyi ≠
Ukusanyaji / Mpangilio
Qur’ani:
Wahyi: kutoka kwa Allah ulikwenda kwa Mtume Muhammad ﷺ
Ukusanyaji: wanadamu walikusanya
kilekile kilichokuwa kimeshashushwa
Biblia (hasa Zabur):
Uandishi: wanadamu wengi, nyakati tofauti, baadhi hawajulikani
Uhariri: kuchagua, kuunganisha, kurekebisha maandiko
Qur’ani haidai kuwa Allah aliikusanya kwa kurasa; inadai kuwa
maneno yake ni kutoka kwa Allah.
Swali ; Je, Uthman (r.a.) “alipanga Qur’ani yake”?
Majibu :HAPANA.
Uthman hakutunga Qur’ani mpya, wala hakuchagua aya.
Alichofanya ni:
1: Kuunganisha
Qur’ani ileile iliyokusanywa zamani na Abu Bakr (r.a.)
2:Kuiandika kwa
lahaja ya Quraysh ili kuzuia migogoro ya matamshi
3.Kuzuia
nakala binafsi zilizokuwa na:tafsiri pembeni, , maelezo ya walimu ,na lahaja zisizo rasmi
Muhimu ni kuwa kulikuwa Hakuna aya mpya iliongezwa na pia kulikuwaHakuna aya iliondolewa
Swali : Kwa nini Uthman alichoma Qur’ani zingine?”
Hili ni swali muliliuliza sana na nimewapa majibu , lakini nyinyi mna akili za kuku , lakini lnimelijibu wazi kihistoria.
Zilichomwa
sio kwa sababu zilikuwa Qur’ani tofauti, bali: Zilikuwa:
1. notsi za wanafunzi
2.nakala binafsi
3.maandishi yenye maelezo ya pembeni
Kama vile leo Ukichoma
draft za mwanafunzi si sawa na kuharibu kitabu cha asili
Lengo lilikuwa ni
Kulinda umoja wa maandishi, si kuficha tofauti.
Swali : “Mtume Muhammad aliacha printed edition?”
Majibu : ni HAPANA, na hakukuhitajika. : Kwa nini? Ni kwa sababu , Waarabu walikuwa
wanahifadhi kwa nguvu sana kwa kukariri na pia Qur’ani ilisimuliwa na
maelfu kwa wakati mmoja
Qur’ani Ilihifadhiwa kwa maandishi na kukariri (tawatur)
Tuje kwa Biblia:
Biblia Haikuwa na mfumo wa
kukariri kama ibada , pia Ilihifadhiwa kwa maandishi ya waandishi wachache
Umeandika Kuhusu Mushaf wa Misri 1924 (Mfalme Fuad)
Hapa pia kuna thread mlileta ya hili na nimejibu sana tu , hata hivyo
Mushaf wa 1924:
Siyo Qur’ani mpya , HAIKUBADILISHA maneno
Lililofanywa ni :
1: kuweka alama za vokali
2 viwango vya uchapishaji
3 kuondoa tofauti ndogo za tahajia
Hiyo Ni sawa na:
Kuchapisha Kamusi sanifu, si kuunda lugha mpya
Qur’ani ya leo ni ileile Qur’ani ya karne ya 7 kwa maneno.
Swali : “Wasomi wa Al-Azhar walizipa majina sura?”
Majibu ni HAPANA.
Majina ya sura: mengi yalitajwa na Mtume ﷺ mwenyewe , yalijulikana kabla ya Al-Azhar kuwepo
Hata kama jina lingepewa baadaye:
Jina si sawa na wahyi
Maudhui (aya) ni sawa na wahyi
Swali : Allah alihusika wapi?”
Majibu : Allah alihusika katika
wahyi, si katika karatasi , wino, au mashine ya kuchapisha
Qur’ani inasema:
“Hakika Sisi tumeiteremsha Qur’ani, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda.”
(Al-Hijr 15:9)
Ulinzi huu: ulifanyika kupitia:
1. kukariri kwa wingi (tawatur)
2. maandishi mengi
3 umoja wa umma
Swali“Una uhakika gani hii ndiyo Qur’ani ya Allah?”
MAJIBU . Ndiyo, kwa sababu:
Tawatur maelfu waliirithi bila kukatika
Maandishi ya kale manuskripti (Birmingham, Sana’a) zinafanana kwa maneno
Hakuna matoleo tofauti ya maudhui tofauti ni
qira’at, si Qur’ani tofauti
Tukija kwa Biblia:
ina: vitabu viliongezwa/kuondolewa , matoleo tofauti (Catholic, Protestant, Orthodox) , Zabur tofauti kwa idadi