Waandishi wa habari wa Tanzania, Hoja kuu ya Mkapa ilikuwa nini?

Unawazungumzia Waandishi wepi? Wakina Pascal Mayalla, Jackton Manyerere, Sam Mahela au wepi?
Hakuna watu wa Hovyo kama Waandishi wa Tanzania. Na Ndiyo maana sikilizi Taarifa za Habari za Tanzania wala magazeti Maana wanaandika kama Hata shule hawajaenda. Hawana Msaada kwa Jamii ya Tanzania.
Nilowapuuuza Kabisa na Kuwaona hopeless pale Waliposhindwa Kusimamia Msimamo wao kwa Kumgomea Nyamitako badala yake wao ndiyo wakaanza kujipendekeza. Waandishi wa Tanzania Makanjaja tu labda Mzee Ulingwe pekee.

Inawezekana kweli makanjanja. Ila hoja yako ndo ya mtu kanjanja Originale. Unataja watu. Ambao una hisia nao hasi so kama waandishi watamtukana na kumgomea usiyempenda Basi ndo wanatoka ukanjanja. Basi Kasome Tanzania Daima. Lina wasomi huwatakao.
 
Inawezekana kweli makanjanja. Ila hoja yako ndo ya mtu kanjanja Originale. Unataja watu. Ambao una hisia nao hasi so kama waandishi watamtukana na kumgomea usiyempenda Basi ndo wanatoka ukanjanja. Basi Kasome Tanzania Daima. Lina wasomi huwatakao.
Hujaelewa hata nilichoandika ni vema ukakaa Kimya tu.
 
Wasalaam,

Kuna tatizo la kimsingi la waandishi wetu wa habari, huenda ni kwa utashi, au uoga au muono pofu.

Hoja ya Bwana Mkapa Jana imesulubishwa na kijihoja Cha kutakiwa kuuwawa kwa bwana mmoja! Nadhani waandishi walitakiwa ku -capitalize kwenye hoja za mleta hoja lakini wengi wao wameacha hoja za msingi wamehamia kwenye habari za sumu! Kwa mtazamo wangu mpewa sumu na hasira zake na %ya uvumilivu wake nahisi mtoasumu huenda angekuwa ameletewa kifaru kipite juu yake! Just a joke!

Waandishi wameacha hoja zilizoletwa kuhusu jinsi gani New CCM wanashindwa kujua kuwa kwasasa kuna vyama vya kushindana navyo kwa hoja, wanadhani kuna koroni sugu linalotakiwa kung'olewa kwa mtutu, kiasi cha kuingiza vyombo vya usalama kukilinda!

Waandishi wameshindwa hata kupembua hoja nono kama je kwanini wajeshi wakapewaa teuzi za kisiasa katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi ambapo mtangulizi wa Raisi aliyepo alishatutoa huko tayari, je hawana datakuwa kuna wanajeshi na mapolisi wamepewa teuzi za kisiasa kama uDC au uRC au nyingine zinazofungamana na hizo?

Wanaelewa maudhui ya Bwana Mkapa kama ilikuwa ni wakeup call, kuliamsha taifa kurekebisha mapungufu badala yake kwa ukichwa panzi!
Hata wakati wa BWM kulikuwa na wanajeshi walihudumu katika utumishi wa umma/ siasa. Kwa mfano Col. Simbakalia, Brig Gen. Luhanga, Col.Tarimo wakiwa kam Ma-RCs.
 
Hata wakati wa BWM kulikuwa na wanajeshi walihudumu katika utumishi wa umma/ siasa. Kwa mfano Col. Simbakalia, Brig Gen. Luhanga, Col.Tarimo wakiwa kam Ma-RCs.
Hujasoma vizuri, ninani mtangulizi wa huyu? Nimeandika JK alijitahidi kutekebisha hilo, maana Kwa uRC au uDC unakuwa unafanya siasa as per CCM constitution maana unakuwa automatically Mjumbe wa kamati ya Siasa ya either mkoa au wilaya.

JK aliliona na akawatoa wote!
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Back
Top Bottom