Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,361
- 11,246
Katika hali inayoonekana kuongezeka kwa maandamano ya kuiunga mkono Hamas na kuilaani Israel huko chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani,waandamanaji hao wameteka moja ya jengo la chuo kikuu hicho.
Utekaji huo ulifanyika muda mfupi kabla ya onyo lililotolewa na kuondoka kwenye mahema yaliyojengwa na waandamanaji chuoni hapo na kutangazwa moja kwa moja na redio ya FM ya inayorusha matangazo kutoka chuoni hapo.
Waandamanaji hao mara baada ya kulikalia jengo hilo walipanda juu na kuunganisha mikono yao huku wakipeperusha bendera za Palestina na hijabu ambayo ni ishara illiyovaliwa na muasisi wa harakati za Palestina,jmarehemu Yasser Arafat.
Jengo linaloshikiliwa na waandamanaji hao ni kitovu cha upinzani uliofanywa chuoni hapo mwaka 1968 kupinga vita vya Vietnama na ukombozi wa haki za kiraia.