Waafrika tunashindana wenyewe, tunaogopa maendeleo ya mwafrika mwengine, tunaridhika tukiwa juu ya mwafrika mwenzetu bila ari ya kushindana kimataifa.

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
1707075890608.png



Ubinafsi umekuwa ni tatizo kubwa sana kwetu Africa kuzidi umoja wa uafrika wetu hasa katika Loyalty ya ukabila / ukoo / mru binafsi,

Mwafrika yupo tayari kumnyima nafasi mwafrika mwenye uwezo kwa sababu za ubinafsi aidha hayupo kwenye kabila / ukoo wake, anahofia akimpa atamzidi maendeleo, anataka na hio nafasi iwe yake (ulafi)..mwafrika yupo tayari kumsagia kunguni mwafrika mwenzake furaha yake wasote wote, mwafrika yupo tayari wakose wote ili mwafrika aliepiga hatua akose zaidi, PURE HATERDNESS TO ITS CORE.

Waafrika hatupendwi na matabaka mengine lakini sisi hatupendani zaidi, huko Marekani wamarekani weusi ndio wanaongoza kwa kuua wenzao mara kibao kuzidi hata polisi, Huku Afrika kuna maandamano kibao kupinga waafrika kuhamia nchi za waafrika wengine ilhali nchi hizo zina wahamiaji wachina, wahindi, wazungu, n.k. Yani mwafrika hataki kabisa kugawana na mwafrika mwenzake.

Waafrika wakiwa juu ya wenzao huona kazi imemalizika hawana morali ya kushindana na wazungu, wahindi, wachina, waarabu, n.k. Mwafrika kufika kileleni ni kumshinda mwafrika mwenzake na atapiga sana kelele ama kufanya chochote ili waafrika wenzake wajue licha ya kwamba yeye mwenyewe ndani ya nchi yake anakimbizwa na waarabu, wahindi, wazungu, wachuna , n.k. wala haoni tabu endapo akiwa juu ya waafrika wenzake.
 
Back
Top Bottom