Waafrika ndivyo tulivyo?

Mzee Es,

Unapokuwa ktk Taasisi zenye sheria kali na system madhubuti utafanya kama inavyotakiwa. lakini ukienda nchi ambayo kila kitu ni RUKSA basi mjomba rahisi nawe kuyafanya maovu.
Tanzania loop holes kibao na binadamu tumeumbwa na tamaa kiasi kwamba inahitaji moyo kweli kweli kujiepusha.

Ukiwa mkristu huwezi kuona sababu wala haja ya kuoa mke wa pili. Ingia Uislaam utaona ruksa hivyo inavyowachanganya watu na hata wengine ku abuse sheria! Kwa hiyo inawezekana kuwa Balali ndiye alopotea kinachohitajika ni kuwepo uchunguzi tu kuondoa rabsha zote!.. yaleyale ya Zitto, wanazidi kukataa uchunguzi ndio wanajenga imani kwamba kuna jambo baya limetendeka.
 
Mzee Bob,

Shukrani mkuu, mimi ninaamini hiyo ni point ndogo lakini kubwa sana katika kuchangia mtataizo yetu ya uchumi Afrika, maana haiwezekani kuwa tuna viongozi wengi ambao ni ex-World bank, na IMF leaders, lakini wakisharudi Afrika tu basi wanabadilika na kuwa kama the locals,

Halafu na sisi wa-Afrika tumezidi sana siasa mpaka kwenye uchumi, nafikir hiyo ndio hasa one ishu ya downside ya Mwalimu, na mpkak leo hatuja-recover bado!
 
Mtukwao,
Yaani umeongea kumbe sisi kuendelea kwa kutegemea AID ni ndoto!
Mimi ningeshauri kutumia nguvu kwa wananchi wetu in 10-15 years! Na wafadhili tungewapa ujenzi tu wa barabara na miundombinu for the period of 10 years baada ya hapo ningewaomba waondoke- tubaki wenyewe!
It is a big shame that we are so proud of hand outs na kuongeza utegemezi toka 39-42% ktk bubget this year! Misaaada inaleta utegemezi- ndo maana viongozi hawataki kukuna vichwa! Hawana changamoto!
We need a bold decision kusema misaada- ni basi! Ila tuwape kama 10 years ili wamalizie na projects tulizowekeana mikataba!
 
Mzee Es,
Hii ulosema kuwa ni point ndogo sana lakini jua kwamba inabeba uzito wa matokeo kwa asilimia 99.
kama vile wanavyosema ktk relationship ya mwanaume na mwanamke, sex ni asilimia ndogo sana ya mapenzi lakini hiyo asilimia ndogo inabeba uzito mkubwa sana wa mapenzi yote.
Hawa viongozi wetu wametoka kweli Ulaya na elimu kubwa ya utendea kazi lakini wanapokuja ktk mazingira tofauti ambayo kwanza yana lack information ovesight, Transparency, compliance na economic freedom, huwezi kulaumu asili ya watu hawa. Sii kweli kwamba Nyerere ndiye aliyetuwekea Siasa ktk Uchumi bali ulikuwa ni muundo wa Chumi zote duniani. Sii Marekani Urusi, Uchina wala Uingereza zote zilifanya biashara zao kwa kutanguliza msimamo wa Siasa zao mbele ya uchumi.
Isipokuwa tofauti imekuja kwamba sisi tumeshindwa kabisa kujiingiza ktk dunia ya Utandazwzi kwa sababu hatukuwa na phase za kujiandaa kama nchi zingine za kijamaa.
ndio kama nilivyosema akina Balali walipokuja wamekuja na Umma na visu vyao kuvitumia hapa nyumbani ambako kila mtu anatumia mkono na kuwataka wananchi wabadilike ktk usiku mmoja na umuhimu haupo ktk umma na visu bali ni maandalizi ya mapishi yao.
Mjomba hata Vietman wamebadilisha uchumi wao hali hawa watu waliutangaza ujamaa kama vile dini na chuki waliyokuwa nayo na Marekani sidhani kama wangefikia hapa walipo leo. Wameweza vipi wajamaa wenzetu na sisi tumebaki ktk shimo la chewa?...unless unataka kunambia kwamba hadi leo hii Watanzania bado wanafikiria kuwa uchumi wa duniani unaendeshwa kwa misingi ya Kijamaa na Kibepari kiasi kwamba tulipo amua kuwa Mabepari basi tunafuata misingi ya Ubepari kulingana na vitabu vya miaka hiyoo ya 70 ambayo ndio viongozi wetu walikuwa shule kwa mara ya mwisho!
 
Ebwana Bob mifano yako hai huwa naizimia kichizi! Huo wa sinia la pilau siku ya Maulidi kali..!!

Eniwei...huu mjadala hauwezi kuisha. Every now and then lazima mtu aunzishe...

Hii ya microwave kuvumbuliwa na mbongo mi sijaisikia....umeto wapi hiyo?

Hapo atakuwa amechapia, hii teknolojia ya mikrowevu waliigundua waingereza katikati ya vita kuu ya pili ya dunia. Wakati huo hata nchi inayoitwa Tanzania ilikuwa haipo kwenye ramani ya dunia
 
Mzee Bob,

Shukrani mkuu, mimi ninaamini hiyo ni point ndogo lakini kubwa sana katika kuchangia mtataizo yetu ya uchumi Afrika, maana haiwezekani kuwa tuna viongozi wengi ambao ni ex-World bank, na IMF leaders, lakini wakisharudi Afrika tu basi wanabadilika na kuwa kama the locals,

Halafu na sisi wa-Afrika tumezidi sana siasa mpaka kwenye uchumi, nafikir hiyo ndio hasa one ishu ya downside ya Mwalimu, na mpkak leo hatuja-recover bado!

Mimi Naona Mwalimu alijitahidi, maana alianzisha MECCO, NBC, TIB, THB, TIRDO, TISCO , STS (BIT), lakini lebaration struggles na Vita Baridi ndizo ziliangusha uchumi wa Tz kwa wakati ule.
Ukiangalia hata sasa hivi, Mengi na wenge wengi wana advocate kusamini vitu vya nyumbani, hata Msuya juzi juzi aliongelea ubaya wa whole sale privatisation na serekali kujiondoa ktk uwekezaji.
Sasa hiyo vita baridi kati ya western countries (capitalist economy) na Eastern Bloc na Wajamaa kama sisi uliadhiri uchumi wetu kwa Propaganda za hizo nchi dhidi ya nchi yetu, pili liberation struggle, kwa kupeleka resource nyingi huko ( tatizo hakutaka kukubali kushindwa hata kama alijua hicho kitu kitakuwa na economic consequencies kwa nchi) maana alikuwa kama mtu alikwisha ya vulia maji nguo shurti uya oge.
Sasa couple na internal dis-satisfaction ya watu na viongozi wenzake alishindwa kusimamia mapambano yote, especially internally licha ya kuwepo institution za kupingana na Rushwa na uzembe mwingine. Ndio likaanza tatizo la ku-recycle baadhi ya watendaji, na pia kwa wakati ule hakuwa na options nyingi, wazee wenzake wengi aliopigania uhuru walisha anza kuwa nje ya System, akawa ni Vijana waliosoma wakati ule ambao hawakuwa wengi, Ndio akina Gibbons wa Bima, Nsekela, Mwapachu, nk, na Bahati mbaya Moringe alitutoka ambaye Mwl alitegemea kumwachia mambo Uchumi wa ndani na watendaji wengine, wakati yeye yupo kwenye liberation struggle na Non Alignment Countries and other international politics.
 
Mzee August,

Unaamini kweli Marehemu alikuwa na strong skills za uchumi ambazo zingeweza kutusaidia as a nation, leo kutukomboa kiuchumi?

Naomba darasa kidogo bro if you do not mind!
 
Mzee Es,
Mwalimu skills za uchumi- yeye kwanza hakuwa mwanauchumi.
Ila uwezo wake kuwaweka watu pamoja- kama taifa (Nation Building) is unqustionable-makabila 122, wakristo na waislam! Nadhani wakati ule we needed Mwal. ila alihitaji Waziri Mkuu Mchumi. Kwa uwezo wake ndo maana mambo kama ukabila, udini Tz ni kidogo ukilinganisha na nchi zingine. Angalia Kenya Kenyata alijenga kweli uchumi- ila hakufaulu sana kujenga utaifa kama Tz. Pia Nyerere uwezo wake kuweka watu pamoja siyo tu kwa Tanzania, hata EA, na SADC na hata South South!
Sasa ilibidi hawa wengine baada ya Nyerere wajenge uchumi- maana tushakuwa wamoja by 1985!
 
Mzee Es,
Mwalimu skills za uchumi- yeye kwanza hakuwa mwanauchumi.
Ila uwezo wake kuwaweka watu pamoja- kama taifa (Nation Building) is unqustionable-makabila 122, wakristo na waislam! Nadhani wakati ule we needed Mwal. ila alihitaji Waziri Mkuu Mchumi. Kwa uwezo wake ndo maana mambo kama ukabila, udini Tz ni kidogo ukilinganisha na nchi zingine. Angalia Kenya Kenyata alijenga kweli uchumi- ila hakufaulu sana kujenga utaifa kama Tz. Pia Nyerere uwezo wake kuweka watu pamoja siyo tu kwa Tanzania, hata EA, na SADC na hata South South!
Sasa ilibidi hawa wengine baada ya Nyerere wajenge uchumi- maana tushakuwa wamoja by 1985!

NAkubaliana nawewe kuhusu hawa wa sasa especially Nkapa na Kikwete, unfortunately kwangu mimi Nkapa huu mtihani ulimshinda, aka institutionalise Rushwa na Uzembe mwingine, sasa Kikwete , nafikiri arudi kwenye drawing board aangalie matatizo yetu na namna ya kuyatatua, sio kisiasa, bali kiufundi, na kurekebisha matatizo alio achaa Nkapa, nayo si kisiasa, akichukua njia hii basi ndio atakapo haribu sehemu zingine, au kusababisha matatizo yetu kuwa donda ndugu labda mpaka Manabii wapya waje
 
Mzee Mzalendo,

Mwalimu was the greatest katika Afrika kwa skills za uongozi wa kisiasa, lakini at the same token hakuwa na skills za kiuchumi na hakutaka kukubali ushauri wa magwiji wa uchumi kina marehemu Professor Rweyemamu, mpaka leo bado hatuja-recover hiyo weakness moja kubwa ya Mwalimu kwenye uchumi as a nation, ndiyo point yangu,

Mkapa alikuwa on the way kuwa the greatest wa uchumi kwa nchi yetu, simply kwa sababu aliweza kukusanya wachumi wenye skills wa kumsaidia, lakini akaanza tamaa za kukusanya mali kwa haraka haraka baada ya Mwalimu kufariki, na akaishia kuharibu kila kitu na kuturudisha nyuma maili 20 zaidi ya Mwinyi na kundi lake!
 
Lakini kwa upande mwingine sisi sote hatuna utaalamu wa kila kitu so kiongozi bora sio lazima awe na skills za ki-uchumi, kama Mwl hakuwa na hizo skills hata Kenyata Sifikiri kwamba alikuwa Mchumi. Tatizo la Nyerere alizidiwa na Mapambano, he had to many things to fight for at that time, na kiu yake kubwa ilikuwa liberation struggles so hata hao wachumi wakimwambia usipeleke huko asinge wasikiliza , ndio hapo ubishi wake ulianza, maana to him liberation struggle ndio ilikuwa his first priority at that time, pili sabotage kama wayo fanyiwa cuba na Amerika ktk uchumi, Na Nyerere hakutaka kugeuka jiwe, au kumpigia Magoti mtu, hasa wa Magharibi. So Nyerere uchumi ulivyo yumba alijua, so immidiate solution ilikuwa ni wote kuchangia ktk hizo deficit, ambazo wengine hawa kukubaliana nae, ndipo ilipozuka Rushwa kubwa na madhila mengine kwa walio kuwa na nafasi.
Aliamini Msuya kwa kuwa alisomea uchumi ange kuwa waziri mkuu Bora, kwa hiyo sioni kwamba alikuwa anawabeza wachumi au kukata ushauri wao
 
Lakini kwa upande mwingine sisi sote hatuna utaalamu wa kila kitu so kiongozi bora sio lazima awe na skills za ki-uchumi, kama Mwl hakuwa na hizo skills hata Kenyata Sifikiri kwamba alikuwa Mchumi. Tatizo la Nyerere alizidiwa na Mapambano, he had to many things to fight for at that time, na kiu yake kubwa ilikuwa liberation struggles so hata hao wachumi wakimwambia usipeleke huko asinge wasikiliza , ndio hapo ubishi wake ulianza, maana to him liberation struggle ndio ilikuwa his first priority at that time, pili sabotage kama wayo fanyiwa cuba na Amerika ktk uchumi, Na Nyerere hakutaka kugeuka jiwe, au kumpigia Magoti mtu, hasa wa Magharibi. So Nyerere uchumi ulivyo yumba alijua, so immidiate solution ilikuwa ni wote kuchangia ktk hizo deficit, ambazo wengine hawa kukubaliana nae, ndipo ilipozuka Rushwa kubwa na madhila mengine kwa walio kuwa na nafasi.
Aliamini Msuya kwa kuwa alisomea uchumi ange kuwa waziri mkuu Bora, kwa hiyo sioni kwamba alikuwa anawabeza wachumi au kukata ushauri wao

August,
Sasa sisi tulichofaidi katika Liberation Struggle ni nini? Ni heshima? Ni kama kuwa baba yeye anasifika kutatua migogoro ya watu- ana anashindwa home kwake- watoto wana njaa- 'sisi tunataka chakula baba- hatujali kama ndo umetoka kwa jirani kutatua kesi!'
Ila Kweli Mwalimu alipanda mbegu ya Umoja hata walianzisha EAC, na SADC na OUA.
Ilibidi hawa wengine waendeleze! Ila Nyerere naye hakukubali ushauri wa wachumi mapema Mtei alimwambia tangu mwanzo sera za kibepari na mikopo akakataa- hadi hali ilipokuwa mbaya wakati wa Mwinyi ndo tukawakumbatia!
 
August,

Hivi unajua mkuu kuwa uchumi wetu hautakuja kuwafikia baadhi ya tuliowakomboa? Kama Msumbiji, South Afrika, au Namibia, leave alone Uganda tuliowatolea Idd Amin?

ninaona unajaribu kwa apologist wa Mwalimu, kitu ambacho sio dhambi, wote wananchi tunampenda, lakini ili tutatue matatizo tuliyonayo kiuchumi sasa, ni lazima tuangalie foundation yetu, tena kiroho mbaya! tumefikaje hapa tulipo na huu uchumi ambao ni a joke?

Msuya, kabla ya kuwa waziri mkuuu alikuwa waziri wa fedha, alifanya nini cha kuwa promoted kuwa PM, kama sio zile hela alizokuwa akizitolea mlango wa nyuma kule hazina kwa ajili ya ku-cover mikutano ya CCM Dodoma? uiletgemea Msuya aurekebishe uchumi wetu kweli? baada ya kutuambia kuwa kila mtu atabeba mzigo wake kiuchumi bongo?
 
Mzee Es,

Ohhh yeah! mwalimu alikuwa na timu nzuri sana ktk Uchumi na mambo mengi ya kutuendeleza. tatizo lilikuwa SIASA yetu na sio mwalimu mwenyewe unless tunataka kutumia hilo neo - Hakutaka kusikiliza wachumi wetu. Lakini mimi namfahamu vizuri upeo wa mtazamo wake kwakuzingatia hali halisi ya wakati wake.
Kulikuwepo na mifumo mwili tu yaani wewe Bepari ama Mjamaa!..kwa hiyo kulingana na moyo wake hili la Ubepari lilikuwa nje kabisa. na elimu kama unavyofahamu inazidi kupanuka kila siku. Enzi zile ukimwambia hata Professor wa Uchumi toka chuo maarufu kwa nini kusiwepo na Utandawazi nadhani angekucheka sana na kusema 'una wazimu.' haya mambo ya macroeconomic ni maswala mapya kabisa ktk Ulimwengu wao na pengine Nyerere na Elimu yake ilibidi akae upya darasani na kujikuta kisha chelewa!

Nyeyere pamoja na kufungua miradi mingi ebu tazama vitu vidogo vidogo kama Usafiri Dar (UDA) hii ni mbinu ambayo sidhani kama nchi za kiafrika walikuwa nayo zaidi ya Tanzania tena enzi hizo za 70. Ni yeye na Kaunda Africa nzima ambao wameweza jenga reli ya mizigo na abiria ndani ya Uhuru achana na hayo mashirika muhimu ya Usafiri wa anga. mawasiliano. na ukitazama hili la mawasiliano Tanzania tulikuwa na chombo cha kisasa kuliko nchi zote za kiafrika, madudu ya mwenge hayakuwa ya kawaida enzi hizo na ndio maana hadi leo reception ya Bongo ni bomba kishenzi pamoja na kwamba line zimezidi kupita kiasi, hata Ukerewe kwetu unazungumza na mtu kama vile yupo mji mkuu. Nakumbuka pia tulikuwa tukitoa walimu kwa nchi kama Botswana na Zimbabwe.

Na kitu gani hasa kinachonifanya niwe na imani na Rais Nyerere! ni yale maendeleo mafupi ya kati ya miaka ya 70 ambayo tuliweza kufikia asilimia 10 kwa miaka mitano mfululizo, Tuafikia hata kuanza kuwacheka Kenya tunapoona maskini wao ktk vibanda vya plastic.
Lakini Pale ngoma ilipoanza kubadilika na mfumo wa siasa yako kuwa ndio registration ya biashara pale ndipo mzee wetu alipopotea!.. na siwezi kusema alipovurunda kwa sababu ati hana elimu ya Uchumi bali IMANI ile ya kutothamini UMOJA nalile swala la kila mtu na mzigo wake ndio havikuweza kumwingia akilini kabisa. Kama imani ya dini mwalimu alikataa kabisa kubadilisha dini yake kwa sababu ya shida!... Kamwe hatakubali kugeuka jiwe!
Na laukama tungeweza kutumia mbinu za mwalimu wakati huu wa Utandawazi nadhani tanzania tungekuwa mbali sana kwani nchi kama China na hizo Economic Zones wamefanya kama sisi tulivyo operate zile district Cooperatives - Mwadeco na kadhalika.
Nakumbuka kwetu huko Ukerewe tulianzishiwa kiwanda cha matunda na kituo cha Uvuvi!..ambapo nyavu na mashine za boti zilikuwa zikipatikana RTC. KIla mkoa mwalimu alijaribu kutambua vipaji vyao na kusisitiza wananchi kuweka nguvu zao ktk kilimo, Ufugaji ama Uvuvi na nyenzo zilipatikana kulingana na uwezo wetu. Sio leo hii na hizo Saccos ambazo fedha ndio msingi wa kuondoa Umaskini unaofanywa na kina Gate, Clinton Bono na hata WB.
Na huwezi kuamini majumbani mwetu tulikuwa tukitumia majiko ya Gas miaka ya 70 tena Ukerewe! hizo nyumba za NHC zilikuwa zimejengwa kileo, Living room, two bedroom, store na vyoo vya kuvuta, maji 24/7 ktk bomba. Hakuna mtu aliyekuwa akilalamika hata kidogo kuhusu usafiri pamoja na kwamba barabara zetu hazikuwa nzuri. Tumesoma bure na hospital bure chini ya serikali yenye njaa ambayo haikuwa na soko nje zaidi ya wananchi wake.
Where can you get A President like him Afrika ya leo hii!...transition tu ya kutoka huko na kuutazama Utandawazi ndipo tulipovurunda kila kitu!...Hilo jengo la benki kuu peke yake tumeibiwa fedha za kuweza kufanyia Ukarabati reli yetu yote ya kati!..
Hizo nchi ambazo tulizikomboa wameanza na NOTHING! achana na kutawaliwa ambako ni kubaya kuliko Utawala wa Mwalimu lakini vipi wao wameweza ku rebound.. chukulia Uganda jinsi Idd Amin na Obote walivyoimaliza tena majuzi tu. Vipi wao wameweza kufanikiwa nje ya fikra za Idd Amin na Obote!
 
Mzee Bob,

Ninajua wewe na Mwalimu, siasa hazikuwa zetu bali za Mwalimu mwenyewe peke yake, akitulazimisha tuzikubali bila ya ridhaa zetu, ndio maana sisi wengine tukaenda kutafuta meli, maana tulijua kuwa ni take it or leave it,

Hakutaka kuwasikiliza washauri wa uchumi ambao mkapa aliwasikiliza sana, mpaka alipoanza tamaa ya mali, anyway, Mwalimu sasa hayupo je kinatushinda nini kurekebisha uchumi?
 
Wazee naomba kuuliza swali, hawa kina Balali na mkewe walikuwa kwenye mashirika ya pesa ya kimataifa na waka-perfom perfectly na hatujkusikia negativity, sasa wakishaingia tu serikalini bongo basi tunaanza kusikia noma, je nayo ni low IQ au elimu ndogo?

Just curious?

Umeshasema mashirika ya fedha ya kimataifa which means they are run most likely na hao hao wadhungu. Mwafrika hawezi kuendesha kitu peke yake. Wengi wanaofanikiwa katika hayo mashirika wako under supersvision ya hao watu na wakirudi bongo ndio maana unaona wanaboronga.
Na kuhusu suala la IQ...hii haina maana weusi au waafrika wote wana IQ ndogo. No kuna ambao wana IQ kubwa tu lakini si wengi kiasi cha wao kuleta mabadiliko yoyote.

Kuna mtu mwingine hapo juu kasema necessity is the mother of all inventions/ ingenuity. If there's any place in the world where this maxim would be more apt then that place is Africa. Most Africans lack the basic necessities of life. So if necessity was the mother of all inventions/ ingenuity then how come...............
 
Mzee Es,

Nakubaliana na wewe kuhusu Mkapa alipoingia madarakani na hasa miaka ya mwanzo, kwani nakumbuka kabla ya uchaguzi wake wa Pili mwalimu alituambia kuwa hategemei kabisa kuwa Mkapa ataweza kupita uchaguzi unaofuata!..Alijua alichokisema na Mkapa hakufanya makosa!... akaweka bao.
Na kwa mdomo wake Nyerere alituambia kwamba Tanzania hata tukipata mafuta hatuwezi kuendelea!...sababu kubwa ni kuwa infrastructure ya nchi ni mbovu kupita kiasi.... bado leo tunaambiwa tunapaaa!

Ni kweli Siasa za Nyerere zilikuwa za lazima, chukua ama sivyo hama sisi wengine ndio hivyo tulichukua muda wetu kupigwa msasa na leo hii nadhani naweza kuzitazama dunia zote mbili kwa urahisi zaidi.
tena umenikumbusha maswala ya meli maanake sisi wengine ndio tulikuwa tukilaani wazazi wetu kwa kutuzaa Afrika wakati ujanja wa meli hatuna, lakini pamoja na Ujamaa huo huo tuliweza kuponyoka na kuingia Ma south na mwishowe Europe na huku duniani. lakini pamoja na njaa zetu za Ujamaa tumeweza kuishi nchi hizi kama Mabepari na pengine vizuri kuliko baadhi wazawa wa hapa... WHY? kwa sababu nchi hizi ni land of Opportunity tofauti kabisa na Bongo ambako watu wenyewe ndio Opportunist!..
 
Kwa maoni yangu, pamoja na mapungufu katika mipango ya uchumi ya Nyerere, alifanya mambo mengi sana kuendeleza nchi kiuchumi katika mazingira aliyokuwa nayo. Ni imani yangu kuwa angekuwa katika mazingira ya siku hizi angefanya vizuri zaidi. Tanzania iliyoongozwa na Nyerere ilikabiliwa sana na mivutano wa vita baridi iliyokuwa inaingilia kabisa jinsi alivyotoa maamuzi yake. Kwa mfano, baada ya mapinduzi ya zanzibar, serikali ya mpinduzi ilikuwa imeiarika East Germany kuwasaidia miradi fulani fulani kule Zanzibar, wakati West Germany nao walikuwa wanaisadia Tanganyika miradi fulani mmjawapo ukiwa ni ukarabati wa hosptiali ya Ocean road na ujenzi wa barabara fulani jijini dar es salaam. Baada ya Muungano mwaka 1964, West German wakampa pressure Nyerere kuwa afukuze East Germany ama sivyo waondoa misaada yao. Hayo yalikuwa ni matusi sana kwa uhuru wetu, jambo ambalo Nyerere kwa ushujaa alilikataa na kuwaambia wajerumani kuwa hatafanya hivyo na wakitaka wachukue hata sindano yao; ni kweli walibomoa barabara walizokuwa wamejenga na kuchukua kila kitu walichokuwa wameweka kwenye hospitalia ya Ocean Road. Kama tungekuwa na uongozi wa aina tuliyoona siku za hivi karibuni nadhani tunejikuta tunayumbishwa sana. Kuna mambo mengi sana ya kutukana utaifa wetu yaliyofanywa na nchi za Magharibu katika kipindi cha kufikia mwaka 1966 ambayo Nyerere hakukubalina nayo ndipo akafikia kuhalalisha siasa ya Ujamaa na "KUJITEGEMEA" kupitia lile Azimio la Arusha. Kipengere cha kujitegemea ndicho kilichoona tunajenga viwanda vyetu vingi sana kuepuka kutegemea nchi za nje. Unedeshaji katika baadhi ya viwanda hivi haukuwa mzuri kutokana na sabau kadhaa mojawapo ikiwa kukosekana kwa usimamizi madhubuti ambapo mameneja walikuwa wakitumia raslimali za viwanda hivyo kwa faida zao binafsi. Baada ya vita baridi kuisha, hatukutakiwa kuuza viwanda vyetu vile kwa nchi za nje ila tungeweza kuvibinafsisha kwa watanzania wenyewe kama ambavyo Japan ilifanya kwa viwanda vingi vilivyokuwa vya serikali kama NEC, JR, ANA na kadhalika. Tatizo lililofanywa na waliomfuata Nyerere ni pale walipojikita kuviuza kwa bei ya bure kabisa kwa "wawekezaji" kutoka nchi za nje kama kwamba wawekzaji hao ndio wakombozi. Kama serikali ingekuwa serious kutaka kumilikisha viandwa na mashirika hayo kwa wanachi isingeshindwa kabisa lakini ile mentality ya kuamini kuwa mzungu ndiye mwenyewe nadhani ndiyo iliyotufanya tugawe nchi yetu kwa wageni tena kama walivyofanya mababu zetu kwa Carl Peters.

Jambo jingine ni kuwa Nyerere alitumia reaslimali nyingi sana kwa kukomboa nchi nyingine. Hata hivyo ukweli kuwa hatuwezi kuwafikia wenzetu tuliowakomboa hauna maana kuwa siasa ya nyerere ilikuwa mbaya. Uganda wameanza kujenga uchumi wao mwaka 1986 baada ya mseveni kuingia madarakani, wakati hiuo mwalimu alikuwa keshaondoka madarakani. To the very least tungekuwa na uchumi kama wa Uganda licha ya kuwa hawana bandari. Msumbiji wameanza kujenga uchumi wao mwaka 1992 tu baada kufikia makubaliano kati ya Frelimo na Renamo wakati nyerere keshaondoka madarakani karibu miaka 7; maendeleo ya Msumbiji kichumi zaidi yetu hayana uhusiano na siasa za Nyerere.

Mkandara: Nilisoma uvumbuzi wa microwaves ukasema ulifanywa na mtanzania wa Kagera. Historia ya microwaves ni ndefu sana ikianzia miaka mingi kabla hatujapata uhuru, na hakuna record nzuri za kuonyesha kuwa tulikuwa na wataalamu wa physics au electrical engineering wa kiwango cha juu kiasi hicho. Najua historia zinazoonyesha wataalamu wa uganga zaidi ya physics na engineering. Ninadhani mvumbuzi wa kitanzania mwenye asili ya Kagera aliyefanya maajabu lakini akazimwa wala hasikiki kabisa katika dunia hii ni Dr. Hezekiah Kamuzora aliyetoa vitu vyake nadhani mwaka 1980 hivi. Huyu aligundua mambo fulani kuhusiana na afya ya damu ya biandamu lakini uvumbuzi wake nadhani ulifinywa kabisa na huenda aliyechukua krediti ni mtu mwingine kabisa.
 
Mzee Kichuguu,

Misimamo ya kiiitikadi, bila ya kuwa na alternative ndio vilimponza Mwalimu na sasa sisi wananchi tunaungua pole pole bila ya kwenda jehanamu, huuu ndio ujeuri wa Hamas kule Palestina kukataa kuitambua Israel, huku wa-Palestina wanakufa njaa maana sasa US hawapeleki pesa tena, na Israel imefunga mpaka wake kwa hiy wa-Palestina hawawezi kwenda kufanya kazi na kpata hela kidogo, matokeo yake msimamo wa kiitikadi ni imara kwa Hamas lakini wananchi wanakufa kwa rate ya wananchi 100 kwa siku hasa huko Gaza, kwa risasi na njaaa, ikiwa ni pamoja na kukosa dawa za magonjwa, Je tuwapongeze Hamas kwa kuwa na msimamo imara kiitikadi?

Kenya wao wakati sisi tuna hizo itikadi za Mwalimu, wao hawakuwa nazo, je are we better than Kenyans leo kiuchumi na kisiasa? Mimi naona wao wameamuka zaidi mpaka kuwatoa KANU the CCM likes?

Mzee wangu ni hizo itikadi ndio zinatufanya mpaka leo tuwape kura CCM, na kuchezewa na hawa viongozi wetu ambao ukiwaangalia kwa makini matendo na maneno yao ni kwamba wanatuchukulia for granted, na hawaamini iko siku upinzani watashinda uchaguzi!
 
Lakini sasa Mzee ES, chukulia kuwa Nyerere alipoondoka madarakani mwaka 1985, tungeanza transformation za kufanya zile investment za Nyerere zifanye kwa faida ya watanzania, je leo baada ya miaka 22 tangu atoke madarakani tungekuwa wapi? Yeye aliiacha nchi na viwanda vya kutosha kutupeleka mbele ingawa vilikuwa vinakosa working capital na usimamizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom