Waafrika ndivyo tulivyo?

jamani mweee mmerudisha ubishi ule uleeee!..
Guys hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa maskini! Umaskini huleta NJAA ya akili na tumbo. Nitarudia kusema kwamba Umaskini wetu ni Ugonjwa!.. unahutaji tiba basi, zaidi ya yapo hakuna! kwa sababu hao hao Waafrika wanapoishi nchi hizi za Ulaya mbona wanafanikiwa sana? tena wengi wamefanikiwa ktk muda mfupi sana kuliko hata wazawa wazungu ktk nchi zao. Je, mnajua kwamba microwave ilivumbuliwa na Mtanzania ambaye kaishi ktk mazingira tofauti. Kuna mifano mingi sana ktk mazingira mazuri na utawala mzuri hata hao wazungu huko Romania na nchi za east Europe wamechoka ile mbaya!.. taratibu wenzetu wameanza kuikubali dawa ya Umaskini sio sisi.

Kama nilivyowahi kusema ktk mjadala mmoja lokuwa ukifanana na huu. mali tulizokuwa nazo sisi ni sawa na sahani la pilau siku ya maulidi!...likishuka chini tu sahani ni tupu kwa sababu hapo mjomba ni Darwin na ujanja kupata sio kuwahi tena. Hivyo basi hata utawala wetu unakuwa hauna mpangilio mzuri utadhani siku ya maulidi na hadi wananchi tumesha adopt concept hiyo. Hii ndio system ya nchi zetu tofauti na wenzetu ambao hawana harka, hula kwa visu na Umma huku wamekaa mezani na kila mtu ana plate yake!.. hiyo ndio sikukuuu ya mzungu.
 
Ebwana Bob mifano yako hai huwa naizimia kichizi! Huo wa sinia la pilau siku ya Maulidi kali..!!

Eniwei...huu mjadala hauwezi kuisha. Every now and then lazima mtu aunzishe...

Hii ya microwave kuvumbuliwa na mbongo mi sijaisikia....umeto wapi hiyo?
 
One of the factors behind the differing economic development in Africa and Asia for example, is that in the former, corruption has primarily taken the form of rent extraction with the resulting financial capital moved overseas rather invested at home (hence the stereotypical, but sadly often accurate, image of African dictators having Swiss bank accounts). From 1970to 1996, capital flight from 30 sub-Saharan countries totaled $194 bn, exceeding those nations' external debts. In the case of Africa, one of the factors for this behavior was political instability, and the fact that new governments often confiscated previous government's corruptly-obtained assets. This encouraged officials to stash their wealth abroad, out of reach of any future expropriation. In contrast, corrupt administrations in Asia like Suharto's have often taken a cut on everything(requiring bribes), but otherwise provided more of the conditions for development, through infrastructure investment, law and order, etc.

Conditions favorable for corruption:

• Information deficits.

o Lack of government transparency.
o Lacking freedom of information legislation.
o Contempt for or negligence of exercising freedom of
speech and freedom of press.
o Weak accounting practices, including lack of timely
financial management.
o Lack of measurement of corruption. For example, using
regular surveys of households and businesses in order
to order to quantify the degree of perception of
of corruption in different parts of a nation or in a
different government institutions may increase awareness
corruption and create pressure to combat it. This will
also enable an evaluation of the officials who are
fighting corruption and the methods used.
o Tax havens which tax their own citizens and companies
but not those from other nations and refuse to
disclose information necessary for foreign taxation.
This enables large scale political corruption in the
foreign nations.

• Lacking control over and accountability of the government.

o Democracy absent or dysfunctional. See illiberal
democracy.

o Lacking civic society and non-governmental organizations
which monitor the government.
o An individual voter may have a rational ignorance
regarding politics. especially in nationwide elections,
since each vote has little weight.
o Weak rule of law.
o Weak legal profession.
o Weak judicial independence.
o Lacking protection of whistleblowers.
o Lack of benchmarking, that is continual detailed
evaluation of procedures. and comparison to others
who do similar things, in the same government or others,
in particular comparison to those who do the best work.
The Peruvian organization Ciudadanos al Dia has
started to measure and compare transparency, costs, and
efficiency in different government departments in Peru.
It annually awards the best practices which has received
widespread media attention. This has created competition
among government agencies in order to improve.

• Opportunities and incentives.

o Large, unsupervised public investments, combined with
complex or arbitrary regulations and a lack of
oversight.
o Sale of state-owned property and privatization.
o Poorly-paid government officials.
o Long-time work in the same position may create
relationships inside and outside the government which
encourage and help conceal corruption and favoritism.
Rotating government officials to different positions
and geographic areas may help prevent this.
o Costly political campaigns, with expenses exceeding
normal sources of political funding (BoT funding CCM
campaign 2000 and 2005).
o Less interaction with officials reduces the
opportunities for corruption. For example, using the
Internet for sending in required information,
like applications and tax forms, and then processing
this with automated computer systems. This may also
speed up the processing and reduce unintentional
human errors. See e-Government.
o A windfall from exporting abundant natural
resources may encourage corruption.

• Social conditions.

o Self-interested closed cliques and "old boy
networks".

o Family-, and clan-centered social structure, with a
tradition of nepotism being acceptable.
o In societies where personal integrity is rated as less
important than other characteristics (by contrast,
in societies such as 18th and 19th Century
England, 20th Century Japan and post-war western
Germany, where society showed almost obsessive regard
regard for "honor" and personal integrity, corruption
was less frequently seen)
o Lacking literacy and education among the population.

Most donors such as the WB, IMF even MCA advise us to discourage those four conditions to succeed.
 
jamani mweee mmerudisha ubishi ule uleeee!..
Guys hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa maskini! Umaskini huleta NJAA ya akili na tumbo. Nitarudia kusema kwamba Umaskini wetu ni Ugonjwa!.. unahutaji tiba basi, zaidi ya yapo hakuna! kwa sababu hao hao Waafrika wanapoishi nchi hizi za Ulaya mbona wanafanikiwa sana? tena wengi wamefanikiwa ktk muda mfupi sana kuliko hata wazawa wazungu ktk nchi zao. Je, mnajua kwamba microwave ilivumbuliwa na Mtanzania ambaye kaishi ktk mazingira tofauti. Kuna mifano mingi sana ktk mazingira mazuri na utawala mzuri hata hao wazungu huko Romania na nchi za east Europe wamechoka ile mbaya!.. taratibu wenzetu wameanza kuikubali dawa ya Umaskini sio sisi.

Kama nilivyowahi kusema ktk mjadala mmoja lokuwa ukifanana na huu. mali tulizokuwa nazo sisi ni sawa na sahani la pilau siku ya maulidi!...likishuka chini tu sahani ni tupu kwa sababu hapo mjomba ni Darwin na ujanja kupata sio kuwahi tena. Hivyo basi hata utawala wetu unakuwa hauna mpangilio mzuri utadhani siku ya maulidi na hadi wananchi tumesha adopt concept hiyo. Hii ndio system ya nchi zetu tofauti na wenzetu ambao hawana harka, hula kwa visu na Umma huku wamekaa mezani na kila mtu ana plate yake!.. hiyo ndio sikukuuu ya mzungu.

....maulid zile ilikuwa kiboko...siku hizi ni za kistaarabu!chakula si kipo!

....tukirudi kwenye mjadala! ni kweli elimu ni muhimu<utahitaji wahasibu,wahandisi,madaktari,wanasheria,n.k!>

....umasikini nao si mzuri kwani unatukwamisha kujenga vituo vya afya vya kutosha,kununua madawa,kusomesha madaktari bingwa wa kutosha...halafu watoto wetu wanakuwa wabuya dawa,wezi na majambazi,malaya,n.k....yaani tunazalisha kizazi hasara kwa nchi.

....tatizo letu kuu wala si rushwa<kwani rushwa ipo hata huko asia>sasa,nisieleweke vibaya,siitukuzi rushwa!.tunahitaji zaidi utawala wa sheria na sheria za nchi kufuatwa!

....tatizo ni kuwa,hatuna utamaduni wa kuendelea!tunaridhika na maisha ya kawaida yenye viwango vya chini kabisa vya ubora. hii inatokana na uvivu na vilevile utamaduni usioenzi uchapaji kazi!

....angalia mafundi wetu mbalimbali wanavyofanyakazi zilizo chini ya kiwango<hasa waashi na seremala>kisa,wanamjengea au mtengenezea mswahili mwenzao....sasa,we subiri hiyo kazi wapewe na mzungu au mhindi...utaona tafauti!.utamaduni huu ndio unaoturudisha nyuma kimaendeleo!

....halafu,tunapenda vitu vya mkatomkato<shortcuts>.angalia jinsi tusivyotaka kuwekeza na tunavyokimbilia kuwa wachuuzi<petty traders>yaani,hakuna mtu anayetaka kusota kidogo,wote tunataka faida za haraka haraka!

....hivi,hatuoni ajabu pale mzungu anapotoka kwao yuropa na kuja kuwekeza hapa kuzalisha bidhaa tunazotumia sisi na wala haziendi nje!.wachina hivi sasa wanakula tenda nyingi za kujenga majumba...ambayo sisi wenyewe tungeweza kujenga!

....ni kweli sisi wenyewe hatuwezi bila msaada wa wazungu!
 
DSM,

I like the facts you outlined.

  1. Je uvivu, tamaa, uzembe ni tabia za watu weusi tu, tena wote duniani?
  2. Yule jamaa mchina alichukua rushwa ya dola laki nne na ushee kanyongwa, Tanzania kuna mtu alipkea rushwa na dola milioni 12 zilizokwenda uswis na kuna ushahid, tumenyamaza.
  3. Kuna hadithi ya mchina kuiba pesa za mradi na hata baada ya mradi aliweza kuonyesha ujenzi uliofanyika, wakati mswahili alipoiba pesa za mradi akamaliza zote na hivyo baada ya muda wa mradi akabakikza na pori lile lile alipotakiwa afyeke ili kufanya ujezi.
  4. Unajua Vietnam ilivyovurugwa na wamarekani, unajua leo hii wako wapi? hebu linganisha na Haiti iliyopata Uhuru miaka 200 iliyopita.
 
Here's an interesting illustration of some of the consequences of a country having a large uninformed majority with mediocre (or completely absent) literacy skills in its general populace.

The Nyalali commission findings (1991) on the issue of whether Tanzania should introduce multiparty democracy or retain CCM as the only political party in Tanzania concluded that 80 percent of Tanzanians preferred the later of the two. These results notwithstanding, the Nyalali comission knew better and decided to recommend the former scenario.

Fast forward to 2005 and results of the presidential election where by a strange twist of coincidence, Kikwete was elected president by a huge landslide of, well, 80 percent, and the dumb majority (read: CCM knuckleheads) at last had their revenge!
 
DSM,

I like the facts you outlined.

  1. Je uvivu, tamaa, uzembe ni tabia za watu weusi tu, tena wote duniani?
  2. Yule jamaa mchina alichukua rushwa ya dola laki nne na ushee kanyongwa, Tanzania kuna mtu alipkea rushwa na dola milioni 12 zilizokwenda uswis na kuna ushahid, tumenyamaza.
  3. Kuna hadithi ya mchina kuiba pesa za mradi na hata baada ya mradi aliweza kuonyesha ujenzi uliofanyika, wakati mswahili alipoiba pesa za mradi akamaliza zote na hivyo baada ya muda wa mradi akabakikza na pori lile lile alipotakiwa afyeke ili kufanya ujezi.
  4. Unajua Vietnam ilivyovurugwa na wamarekani, unajua leo hii wako wapi? hebu linganisha na Haiti iliyopata Uhuru miaka 200 iliyopita.

....wakati mwingine inatia uchungu sana.

....nadhani,watu weusi by large,tulizaliwa tuwe masikini wa kila kitu!yawezekana ni laana!

....kila jamii duniani<weupe,wekundu,wanjano na weusi>ina watu wazembe, wenye tamaa na wavivu....sisi tumezidi.


....tunaridhika upesi na maisha duni,kisa,hatupendi kufanya kazi!tunafanya kazi ili tupate mlo tu!

....mbaya zaidi,tuna utamaduni wa kulinda maovu. ni wachache kati yetu huweza kuyakemea!halafu jamii ikaona wamefanya jambo la maana.

....it seems as if hatuna sense of belonging,zaidi ya kuiita africa motherland!
 
Here's an interesting illustration of some of the consequences of a country having a large uninformed majority with mediocre (or completely absent) literacy skills in its general populace.

The Nyalali commission findings (1991) on the issue of whether Tanzania should introduce multiparty democracy or retain CCM as the only political party in Tanzania concluded that 80 percent of Tanzanians preferred the later of the two. These results notwithstanding, the Nyalali comission knew better and decided to recommend the former scenario.

Fast forward to 2005 and results of the presidential election where by a strange twist of coincidence, Kikwete was elected president by a huge landslide of, well, 80 percent, and the dumb majority (read: CCM knuckleheads) at last had their revenge!

....we were made to accept multipartism,externally.
 
You may be right, but whether pressure to introduce multipartism came from Nyalali commission, the IMF, World Bank, G8 - and whoever else willing to pour billions of dollars in development aid into the country every year - it still doesn't change the fact that its the ignorant uneducated and downright foolish majority who get to decide how the country is run by putting the same proven thieves, fraudsters, con artists, liars and crooks in everlasting power every 5 years.
 
It all boils down to IQ..IQ..IQ..IQ
Waafrika Ndivyo Tulivyo...

How come everywhere you go blacks are always the downtrodden? Why?
 
Ngabu,

hizi habari nakumbuka vizuri kuwa nilizipata pale Ubalozini petu wakati nikiwa mgeni kwa mara ya kwanza nchi hii. Katika mazungumzo wazee wetu akiwepo balozi marehemu Chief Lukumbuzya na mzee Ally Sykes walizungumzia maswala yanayolingana na mada hii hadi kufikia uwezo wetu. Jina la huyu jamaa limenitoka lakini nitalipata sii muda nachokumbuka ni mtu wa ziwa magharibi. Lakini ndio kama hivyo katumiwa mwafrika na jina lake halipo ktk historia yeyote ya uvumbuzi wa electrical microwave. Tazama basi ni miaka mingapi imepita, na wazee wetu waliweza kuliona tatizo hili la mtu mweusi.
Kisha shukuran kwa kupata kunielewa ktk hoja ya sinia la Pilau. Wee tazama hoja zote zilizozungumziwa hapa hazina tofauti kabisa na visa vinavyotokea ktk janvi la pilau. Corrupton, Accountability, Ulafi, Ubinafsi na kadhalika ndio vitu vinavyoonekana kila siku ya maisha yetu. Hilo sinia linaweza kabisa kushibisha watu wote waliokaa kulizunguka! tatizo ni kwamba hatuna utaratibu -system yetu mbovu sana na ajabu ni kwamba tunaiga mambo yote lakini sio hili la kukaa mezani kila mtu na plate yake. na ndio maana Ujamaa umekuwa na tafsiri mbaya sana kwa sababu moja tu. Ujamaa kwetu ni kuweka sinia moja na ku-share chakula bila kuwa na mategemeo nje ya Uzalendo!..sheria zimeandikwa ktk makabrasha na kufutikwa chini ya vungu...sheria ni Kutawala.kama wazee wetu wanavyotawala janvi la pilau...wataanza kula wao na nyama nzuri ni zao wao!
Haya ukitazama sisi walalhoi, reality inatuambia kuwa walafi hawawezi kukosekana. Kuna watu target yao kwanza ni Nyama, wengine funda moja la mkononi linachukua robo ya sinia. wengine akina sisi makoo yetu madogo na hatupendi kugombania chakula....
Sasa nani wa kumlaumu - sidhani kama ni wapishi hata kidogo ila utaratibu mbaya unaanza pale tunapoweka mafungu ya watu ktk majanvi..Masheikh (viongozi) wana janvi lao kisha kilichobaki ndio walalahoi na mara nyingi waloshughulika ktk kupeleka masinia huondoka na njaa zao. hawa ndo wengi ile mbaya.
Kisha kwa mwenye NJAA utaratibu unatakiwa kuwa mzuri zaidi ya ule wa wazungu wanao tuchapia, tukizingatia kwamba Mbantu ukiweka Buffet utakoma mwenyewe nyama zitawekwa hata mfukoni! wengine wataenda jitapisha choooni warudi kuhakikisha wamesafisha meza....hiyo mipango ya Saccos na kadhalika. Ili mradi sisi waafrika malezi yetu yamekuwa ya shida sana kiasi kwamba neno Ustaarabu lina tafsiri yake tofauti kabisa.

Serikali zetu budi zitazame upya mazingira yetu kisha wajenge mikakati inayolingana na maisha yetu laa sivyo kila rais atakaye kuwa madarakani atafikiria kwanza kuiba na akisha iba wafuasi wake watafuata kwani sababu:- Uwezo wanao, sababu wanayo na nia wanayo!
Tumekwisha mjomba! labda kizazi hiki kipya akina Njabu muwe na mwelekeo mpya!..
 
Looh! Kwa mara nyingine tena mifano yako hai inanifanya nijisikie kama vile niko kwa mzee Makuka nikisubiri lau lau la Iddi. Umeweza kuunganisha vizuri huu mfano na jinsi nchi yetu inavyoendeshwa/ kuporwa (haswa huo mfano wa nyama maana ni kweli kabisa hata mimi mwenyewe n'shawahi kushuhudia hiyo kitu...kabla hata sinia halijatua watu wameshaanza kuchukua nyama juu kwa juu mpaka likishafika chini nusu nzima haipo...kulaleki walahi...hii imenikumbusha mbali sana). Mifano yako huwa inasaidia sana kuelewesha...hasa kwa watu kaa sisi. Shukrani babu.
 
I don’t think if the low IQ level that black Africans have is the reason. The economy of Africa consists of the trade, industry, and resources of the peoples of Africa. Increased corruption and despotism are the main reasons for Africa's poor economy. Some people add the transition from colonialism has been shaky and uncertain, and the Cold War, but I don’t buy the last to items.

Fine, its probably not the IQ, otherwise we would not be writing this here, and there is corruption everywhere, but the fundamental necessity for all, except in Africa, is to build their nations .. to be self reliant, to have your own, to contribute something in the world economy.. not to remain perpetual beggars... its in our culture, we don't despise begging, we think its necessary ...
Oh you guessed it right ... a contract to build that important road to the economy may be obtained fraudulently anywhere, but the road will be built everywhere except in Africa!! ..
Its frustrating, very ..
 
It all boils down to IQ..IQ..IQ..IQ
Waafrika Ndivyo Tulivyo...

How come everywhere you go blacks are always the downtrodden? Why?

Good question!
Why, I still think the answer mainly lies in culture that tolerates Uvivu, free things, sharing etc! Why work if you don't have to, why think if you can cheza ngoma all day and still not starve .. It is just not necessary, and necessity is the mother of all ingenuity/creativity ..
I really do not think it is the IQ, i know some african countries that are slowly evolving out of that complex ....
 
Ndugu zangu Waafrika,
Ni utumwa tu wa fikra kuwa sisi hatuwezi kitu! Maadui zetu wale2 watatu- Ujinga, maradhi na Umaskini! Kwa nini hatuwezi kujikomboa- hatuna jibu!
Mila na desturi zetu na utamaduni wa kulindana na kuoneana haya hata tunapoharibu! Kule Tanga kuna watoto huiba hizi nyaya za umeme za TANESCO na kuuza Kenya- wazazi, viongozi wa kijiji wanawafahamu- ila serikali ikichuza- watu hukaa kimya! Eti- "kwanza nyumba sisi tunazoishi hazina umeme- hata waibe au waache itatusaidia nini?"
Huu ndo ushenzi wa kijinga- na watu kama hawa hatuhitaji demokrasia ya magh ili wabadilike! Mimi naona kuna haja ya kutumia nguvu kwa muda wa kama miaka 10 so as kuleta discipline katika kazi, uwajibikaji, uadilifu n.k. Baada ya hapo ndo tuongelee demokrasia! Mtu hana choo- na unamwelimisha anasema hataki kujenga choo chake- ukimlazimisha ankuambia hatakuchagua! Kipindupindi kinatokea mtu huyu anakufa! Je kama ukiwa Mkuu wa Wilaya- kuna haja kumbembelezana kweli? Mimi nadhani kuna mambo yabidi tutumie nguvu kubadika- kama elimu, usafi na ujenzi wa barabara! Hakuna nchi hata moja iliyoendelea ambapo nguvu hazikutumika yaani wananchi walipembelezwa kuleta maendeleo!
This issue is complex- jawabu sii kutawaliwa na wazungu directly- huwa huru ni jambo zuri- ila uhuru wa bendera na kuwa omba omba wa misaada- du ni aibu kubwa!
 
Vyote vile ina wezekana-!!Tusamehe!! kwasababu Kira Uginga wa rangi Ulichochea Yale tunayo yaita Ustaarabu-kwani kwa kila anaye bagua kwa rangi sasa anaonekana ********-

Lakin bado wapo wahindi-wazungu -wa africa-wachina- ...... NK wanao nufaika na kuthirika Kutokana na Ubaguzi...
 
Wazee naomba kuuliza swali, hawa kina Balali na mkewe walikuwa kwenye mashirika ya pesa ya kimataifa na waka-perfom perfectly na hatujkusikia negativity, sasa wakishaingia tu serikalini bongo basi tunaanza kusikia noma, je nayo ni low IQ au elimu ndogo?

Just curious?
 
..... Mimi naona kuna haja ya kutumia nguvu kwa muda wa kama miaka 10 so as kuleta discipline katika kazi, uwajibikaji, uadilifu n.k. Baada ya hapo ndo tuongelee demokrasia!

Naam, hili laweza kuwa ni jibu ...
Lakini hata sasa hivi wanatawala kwa nguvu, hii ni demokrasia uchwara! Kama wangetaka, wangefanya hivyo unavyosema, kulazimisha watu kustaarabika, kuheshimu kazi/kupata KWA JASHO LAO, ...
CHINA inafanya hivyo, na inafanikiwa, tofauti na sisi ni kwamba viongozi wao wanajua wanachofanya, na hawamsikilizi yeyote, awe Mmarekani na demokrasia yake wale Papa una dini yake.... Wao wanafanya mambo yao. Sisi kila kikao tunawatafuta na kuwaabudu Development Partners!! Shame upon us. Watu wamekuja Afrika kutafuta sisi tunafikiri wametuonea huruma wanatusaidia... na kwa nini tupende kuonewa huruma na kusaidiwa??? Hili ni tatizo kubwa.. Why should anybody do things we can do for ourselves, and in so doing learn to make mistakes and right things along the way? How else do we build the required capacities and experiences to run our own country if from early on think we cannot do things, and hence call in development partners??

You see, despite all, I am a great fan of EL, for having the right spirit. The only one who could unceremoniously chase away a "development partner" (It was a persona non grata), the former City Water bosses!

WE SHOULD NOT BEG, IT DESTROYS A MANS SOUL, THE VERY SOUL ON WHICH WE DEPEND TO DRIVE OURSELVES FORWARD!! ...

Nakubali, demokrasia up to a point, may be for only the ELITES that are set on a noble course... lakini kwa nchi iliyojaa wajinga wasiolewa mambo, un-educated mass ni kurudi nyuma. Sana sana watatumiwa na wajinga wenzao wanaotaka madaraka kwa manufaa yao!
Kwa mfano kwa kutumia demokrasia wale jamaa wanaoomba pale kwenye mataa ya akiba (ambao wala siyo vilema) wataitaka serikali iwaletee miavuli ...

Stupid!
 
Tunaweza, lakini tunahitaji utashi (commitment ya kufanya hivyo)
Hiyo ndio kitu cha kwanza hata bila hiyo elimu ya kisasa.
Na Mifano tumeiona huko numa kama KNCu na Nyanza co-operative walivyo fanya kabla ya uhuru, hata Vilabu vyetu vya mpira kama Yanga chini ya Uongozi wa akina Taabu mangara Tabu.
Sasa tatizo linaanzia unapopata kiongozi asiye na committment ndio hapo anapoanza kutokusimamia sehemu yake ya kazi vizuri na kupuuza ushauri anaopewa hasa wakitaalamu, sheria, na hata katika kuingia ktk mikataba mibovu sio kwamba haelewi, bali hana huo utashi wa kupiga mahesabu ya mbele.
 
Gigo,

Ni kweli kabisa kuwa vyote vinawezekana. Na elimu ndio msingi bora wa wananchi kufuata sheria na taratibu za maendeleo yao. Siwezi kusema kwamba wananchi wanapokula ktk sinia moja ni low IQ kwa sababu mtayarishaji ni serikali ambaye kawapanfga watu wake kwa mafungu, na sinia letu linatoka Bungeni likiwa limejaa wali mkavu na nyama za kugombania!. hali hii haina rangi ya mtu hata kidogo na unaweza kuona hata nchi za wazungu ambazo zilikuwa na utaratibu mbaya kama wetu waligombania nyama!.
Mfumo wa Darwins upo kitaifa ktk external forces lakini kwetu waafrika tumejengewa mazingira kiasi kwamba tuna malizana sisi wenyewe!
Ni wazi wazungu watashindwa kutuelewa kwani wao nyama ya kuku ndio rahisi kwa bei upatikanaji wake kuliko nyama nyingine yoyote. Sisi waswahili nyama ya kuku ndio fahari ya utajiri wenyewe.
Kwa hiyo siwezi kusema kwamba sisi waafrika ni wajinga ama IQ yetu ni duni kwa sababu binadamu wote tumeumbwa na sehemu ndogo sana ya akili ambayo inatutofautisha sisi na wanyama. Huo uwezo wa kufikiria na kuchambua kati ya mazuri na mabaya!
Uwezo ambao unakuwa controlled na factors nyingi zikitanguliwa na IMANI. Waafrika tumekosa Imani na mara nyingi tumekuwa tukiiga kila kitu toka kwa hao wenye rangi ambao walitutawala kwani ndio wenye ELIMU.
Wee tazama Gadaffi kaomba Afrika tuwe taifa moja lenye nguvu ya kuweza kuwakilisha mawazo yetu lakini viongozi wetu wamekataa katakata kwa sababu ambazo hazifahamiki. Kwani JK akiwa senetor wa Tanzania akakuwa amekosa kitu gani kama kiongozi na mwakilishi wetu? hawa viongozi wanafahamu fika kwamba Afrika kama nchi tofauti sijui 50 hatuwezi kuwa na sauti kabisa ktk UN na taasisi zake!.
Utajiri tunao wa kutosha na pengine nchi hizi matajiri zinatuhitaji sisi kuliko sisi tunavyowahitaji wao. Chukulia tu kwamba wao wana elimu na uwezo wa kutengeneza finished product na sisi akina Yakhe Mungu katujalia rasilimali ambazo ni pamoja na madini, vipaji asili vya kuzalisha mali ghafi inayohitajika na hawa wenye rangi.

Pamojana yote hayo akili zetu zimefungwa na viongozi wacheche wenye nguvu na akili ya kurubuni watu kuwa hakuna pepo ila kwa kupitia kwao, na wengi tumekubali kwa sababu hatuna elimu. Hivyo basi tatizo letu kubwa ni ELIMU zaidi ya hiyo IQ!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom