Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
Kuna uzi mwingine hapa JF unasema kuwa Msajili wa vyama vya siasa amesema ataendelea kutoa ruzuku. Sasa hawa mwananchi wanatuambia PAC 'imemtaka' Msajili aendelee kuvipitia ruzuku vyama vya siasa!
Nani alimuwahi mwenziwe?
Awali PAC ilikurupuka kwa kutoa "maelekezo" kwa msajili kusitisha ruzuku kwa vyama.
Baada ya wadau kuielimisha PAC juu ya mipaka ya madaraka Yao,na baada ya kubaini kwamba msajili alikuwa Makini sana kabla ya kuitikia wito wa kusitisha ruzuku,ndipo sasa PAC ilatambua kuwa ilikuwa imepiga wrong number!
Katika kujikosha na kutaka kufuta madhambi iliyokuwa imeyafanya,PAC imeluja sasa na kauli mpya ya kumtaka msajili aendelee kuvipatia vyama ruzuku.
Kimsingi bado PAC imechemka tena kwaluwa mamlaka Yao yanaishia kwenye kuvipa muda vyama ili viwe vimekaguliwa hadi hiyo January 2014
Suala la kuendelea au kutokuendelea kupata ruzuku linabaki chini ya mamlaka ya msajili,na PAC wasiendelee kujifanya wao wana mamlaka hayo.
Jambo la msingi ambalo mimi nilitarajia kulisikia Leo kutoka PAC ni namna ya kuiwezesha ofisi ya CAG kifedha ili iweze kufanya ukaguzi wa mahesabu ya vyama kwakuwa imeelezwa tangu awali kuwa ofisi ya CAG imeshindwa kufanya ukaguzi wa mahesabu ya vyama kwakuwa hawana bajeti ya kazi hiyo. Lakini naona Hilo hawajalizungumza,na hapo ndipo nataka kulibaliana na wadau kuwa PAC inafanya siasa badala ya kazi za kitaalamu na kisheria.