Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

mda si mrefu watakua wanaandaa mikutano ya kampeni london, munich, new york nk
 
Pretty.. kwanza nadhani kuna majibu ya kisiasa na majibu ya kimkakati. La kisiasa ni kuwa CCM inafanya hivyo kwa sababu inaweza na kwa sababu Chama kinajijenga zaidi. Kwa upande wa mkakati ni kuwa kwa mtu yeyote ambaye anataka kufanikiwa huko mbeleni (kisiasa, kiuchumi na vinginevyo) ni muhimu kuchagua upande unaoshinda.

Wakati mwingine nafikiria hata yawezekana ni bora kurudisha chama kimoja tu ili kila mtu awe anaingia kwenye chama halafu tukijaza fomu za kuomba kazi, n.k tujaze kuwa "tulipitia UVCCM" au tumewahi kuwa viongozi wa chama mahali fulani. It comes na ujiko fulani.

Lakini upande mwingine inawezekana kabisa wananchi hawa wanamapenzi ya kweli ya CCM na wameshindwa kujizuia kutoyaonesha mapenzi hayo na wameamua kufanya hivyo. Kama hili ni kweli basi ni matatizo ya upinzani kutojitahidi kupata wanachama hadi nje ya nchi au matatizo ya mashabiki wa vyama vya upinzani na wenyewe kutojiunganisha na kuanzisha matawi yao huko waliko.

Tatizo litakuja pale ambapo vyama vya upinnzani navyo vitaanza kuanzisha amtawi kama hapo London n.k na matokeo yakawa ni mgawanyiko wa Watanzania. Ndio maana sisi wengine huku US tuko sensitive kweli na mambo haya ya kuanzisha matawi ya vyama hapa.

Mzee Mwanakijiji, Heshima mbele - Umechambua vyema sana mimi binafsi nakubaliana na wewe kwa yote uliyoandika hapo juu, Chukua Tano Mkuu
 
- Sometimes wa-Tanzania tunapenda sana kukuza ishus bils sababu, wananchi wana haki ya uhuru wa kuchagua wanayotaka kuyafanya na wasiyoyataka as long hawavunji sheria za Tanzania au za nchi walioko, binafsi sioni tatizo lolote na wananchi kujiamulia kuanzisha tawi la CCM au la Chadema hivi kwani wanalazimisha mtu kujiunga nao? Au wamemuharibia mtu kazi huko majuu?

- I mean please, waacheni jamani tunawaonea bure na hizi attacks bila hoja ya msingi, mwisho itaonekana tunawaonea wivu, wakianzisha matawi ya CCM, tuliobaki tuanzishe Jumuiya ya ki-Tanzania ili asiachwe mwananchi bila msimamo, waacheni wananchi wafurahie matunda ya uhuru na Demokrasia ya kujamulia mambo yao wenyewe bila kuamuliwa na serikali.

- So far hatuna hoja ya msingi ya kuwashambulia wananchi wanaoanzisha matawi ya CCM, sasa it about time tukawaacha kama walivyo na matawi yao!

Respect.


FMEs!
 
- Sometimes wa-Tanzania tunapenda sana kukuza ishus bils sababu, wananchi wana haki ya uhuru wa kuchagua wanayotaka kuyafanya na wasiyoyataka as long hawavunji sheria za Tanzania au za nchi walioko, binafsi sioni tatizo lolote na wananchi kujiamulia kuanzisha tawi la CCM au la Chadema hivi kwani wanalazimisha mtu kujiunga nao? Au wamemuharibia mtu kazi huko majuu?

- I mean please, waacheni jamani tunawaonea bure na hizi attacks bila hoja ya msingi, mwisho itaonekana tunawaonea wivu, wakianzisha matawi ya CCM, tuliobaki tuanzishe Jumuiya ya ki-Tanzania ili asiachwe mwananchi bila msimamo, waacheni wananchi wafurahie matunda ya uhuru na Demokrasia ya kujamulia mambo yao wenyewe bila kuamuliwa na serikali.

- So far hatuna hoja ya msingi ya kuwashambulia wananchi wanaoanzisha matawi ya CCM, sasa it about time tukawaacha kama walivyo na matawi yao!

Respect.

FMEs!

Mkuu unachosema ni kweli, chama chochote kama kina uwezo wa kujitanua kuelekea kokote kifanye hivyo, lakini tunatakiwa kuwa makini sana na tuangalie sheria zetu. If our laws are mute (hazipingi na haziruhusu) vyama vyetu kuwa affiliated, supported or funded by overseas groups Tanzanian or non Tanzanian hakuna dhambi ya kufanya hivyo.

Lakini siku vyama hapa nyumbani vikianza kuwa na uhusiano na Al qaeda, au vikaanzisha matawi, Afghanistan, Pakistan, Iran au Sudan, we should be equally mute as we are on CCM UK. Au kama makundi mengine kutoka nje ya TAnzania yanaanzisha shughuli zao za kisiasa hapa Tanzania we should equally be mute. Ukiangalia kijuujuu unaweza kuona kuwa hakuna tatizo, lakini tunatakiwa kuangalia mbali zaidi, na ni lazima kuwa na level play ground kwa vyama vya siasa hapa Tanzania. Kama TLP haiwezi kuanzisha matawi ya kisiasa London na CCM ina uwezo huo, that will is unfair.
 
Wote wanaohusika na matawi hayo ya nje ama wana uhusiano na vigogo wa CCM au wanatafauta namna fulani ya kupata ujiko serikalini kwa namna moja au nyingine. Ndivyo system yetu ilivyo.
 
.........Siku hizi naona matawi mengi ya CCM yanafunguliwa huko ughaibuni, lakini mwenzenu sielewi malengo yake haswa ni nini? Je kama taifa linapata faida gani kutokana na hayo matawi ya chama cha siasa nje ya nchi?

Mwenzenu najiuliza hivi kwa sababu sijajua bado kama nchi nyingine hapa duniani nao wana utaratibu wa kufungua matawi ya vyama vyao tawala nje ya nchi zao?

Hapa Tanzania wapo raia wa nchi mbali mbali wanaishi hapa, lakini sijasikia kama wamefungua matawi ya vyama vyao vya siasa hapa nchini.

Lengo haswa ni nini hadi CCM inafungua matawi huko ughaibuni?Mie huwa najiuliza sababu ya ufunguzi wa hayo matawi sipati jibu...........hivyo nimeamua kuleta hapa labda nitapata majibu.

Strategic plan for victory & a very good one I might add. Ughaibuni kuna Watanzania vijana ambao wapo vyuoni ambao vipaji vyao na elimu yao ina hitajika na chama kama CCM. Kwa hiyo hapa wana angalia future ya chama. Pia Watanzania wa ughaibuni ni source of funds kwa ajili ya chama. Unaweza ukakuta huko nje kuna watanzania wenye uwezo mkubwa wa kukichangia chama.

Nchi zilizo endelea hazi weki matawi nje kwa sababu tayari wana vyuo vikubwa vinavyo weza kuproduce vipaji hivyo na pia tayari wana wananchi wengi wenye uwezo wa kipesa kwa hiyo tayari wana source kubwa ya funds nchini. Kama nchi zingine maskini hawafanyi hivi(I'm not sure kama kweli hawafanyi or not) basi labda ni strategy ambayo hawaja fikiria au tayari wana njia zingine za kutimiza malengo hayo hayo ambayo CCM inayo kwa kuwa na matawi nje.

Hate it or love it, I think it is very smart of CCM for doing so. Wanajua Watanzania waliyopo nje ni untapped resource ambayo wana taka kuwa wakwanza kuexploit. Baadae vyama vya upinzani navyo viki funguka macho na kuwa na uwezo zaidi usi shangae nao wakianza kufungua matawi nje.
 
Mie nadhani hawajiamini na maisha yao, hivi mfano unakazi au unasoma utaweza kupata muda wa kuhudhuria upuuzi huu??? mhh asilimia kubwa ya hao watu ni chadirishani😀😀
 
Mie nadhani hawajiamini na maisha yao, hivi mfano unakazi au unasoma utaweza kupata muda wa kuhudhuria upuuzi huu??? mhh asilimia kubwa ya hao watu ni chadirishani😀😀

Usi shangae kukuta baadhi yao ni watu wenye uwezo kuliko uzaniavyo. Na wengine hizo ndiyo shughuli zao so wewe unapo ona hawana kazi kumbe ndipo wanapo fanyia kazi 🙂
 
VERY INTRESTING KWA KWELI nimeskia wadau wa huko Marekani wakisema huyo Balozi Mama Maajar akija huko USA alikoletwa na JK akileta huu ushamba wa UK wa kufungua matawi ya CCM watamtoa ushamba wake wanasema siasa za matawi ya Reading ni huko huko Uingereza ushamba wa UK usilete Washington DC , wabongo watakucheka na kukutoa nishai.
 
Sidhani kama nchi za kigeni zinaruhusu watu wa nchi nyingine (wageni) wafanye shughulu zao za kisiasa nchini mwao. Kwa mfano siamini kuwa Tanzania itaruhusu watu wa Rwanda, Burundi, DR congo, Kenya, Zambia, Uganda na kwingineko, waje wafungue matawi ya vyama vyao mabali mbali vya kisiasa. Huo utakuwa mwanya wa fujo zisizokuwa za msingi.

Kwanza unaanza anzaje kuisajili CCM Uingereza, Marekani, Urusi na kwingineko, mpaka uje ufungue na matawi yake. Naona tunajifanyia tu mambo mengine. Hayana faida kwa Taifa.

Jingine ni kujikombakomba tu na kujitafutia umaarufu. Kama mtu anataka kujiingiza katika ulingo wa kisiasa si arude tu nyumbani tuhangaike naye?
 
ni njia moja ya kuwajengea mazingira mazuri ya kupewa vyeo watoto, marafiki, jamaa wa wakereketwa wa chama ambao wanasoma au kufanya kazi nje ya nchi.
akirudi Tanzania basi `anaandika` kwenye CV yake kuwa amekitumikia chama ughaibuni
 
Katiba ya CCM inayatambua matawi haya ya ughaibuni. Hili tumelijadili sana humu. Tujaribu kuwa tunatembelea threads za zamani tutayaona haya na mengine mengi. Au tu wavivu wa kusoma?
 
Mie nadhani hawajiamini na maisha yao, hivi mfano unakazi au unasoma utaweza kupata muda wa kuhudhuria upuuzi huu??? mhh asilimia kubwa ya hao watu ni chadirishani😀😀

Kama una muda wa kwenda shopping, kanisani, msikitini, ama kwenda pub/bar na sehemu zingine za starehe wakati unakazi au unasoma utaweza pia kupata muda wa kuhudhuria vikao ama shughuli za ccm
 
Hata walioko Italy wamefungua !Lakini kama kuna mtu anajua mambo ya Italy,especially ya immigrant wa kiafrika walioko huko,tuliotembea tunajua .
CCM itakuja kuadhirika na watu hawa ,wengi wana history mbaya.
Mwenye macho haambiwi ona mkuu! Watayaona mbele ya safari baada ya kukusanya kila wanalotaka kukusanya hata kama ni mabomu ya kutegwa
 
Napenda kuchukua fursa hii kuwaulizeni wanajamii kuibuka hivi karibuni kwa matawi ya CCM huko Ughaibuni e.g,Moscow,Italy,Germany,UK,USA,je kuwa na mtawi huko kuna tija gani kwa Taifa au nini malengo hasa,mbona vyama vya huko havina matawi Tanzania?
 
hao wanaoanzisha matawi huko wanajipendekeza, waendelee kuosha vyombo ulaya, wapuzi
 
Hao ni aidha Misukule (Mazuzu) au wanafaidika na ubaya ubaya wa CCM kwa taifa letu. Wametelekeza ndugu zao na ni walamba miguu ya MAFISADI.
 
wakuu labda mnisaidie!kuna umuhimu gani wa chama pinzani kuanza kufungua matawi nje ya nchi wakati kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi hii hawajayafikia, ukizingatia watanzania wengi nje ya nchi hawaji kupiga kura wakati wa uchaguzi,na hatuna mfumo wa ON LINE VOTING?? inanitatiza sana hii
 
wakuu labda mnisaidie!kuna umuhimu gani wa chama pinzani kuanza kufungua matawi nje ya nchi wakati kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi hii hawajayafikia, ukizingatia watanzania wengi nje ya nchi hawaji kupiga kura wakati wa uchaguzi,na hatuna mfumo wa ON LINE VOTING?? inanitatiza sana hii
Kwa jukwaa hili, subiri matusi, lakini isikutishe, ni bora kupuuzwa na wajinga 1000mil. ila ukaungwa mkono na mwerevu mmoja!

........Kwanini tufuge paka tutarajie kula mayai?
Si tumetaka Demokrasia, wanaojifanya wajanja ndio hao wanaitumia! Walianza ccm, nccr, cuf, cdm, na upuuzi mwingine kama huo! Ukishangaa ya Musa, utaona ya Firauni! Ndio hayo.
Ila tukithubutu tunaweza, Mungu wetu anaita!
 
Back
Top Bottom