Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Vyama vya Siasa na Matawi ya Ughaibuni

Kwa jukwaa hili, subiri matusi, lakini isikutishe, ni bora kupuuzwa na wajinga 1000mil. ila ukaungwa mkono na mwerevu mmoja!

........Kwanini tufuge paka tutarajie kula mayai?
Si tumetaka Demokrasia, wanaojifanya wajanja ndio hao wanaitumia! Walianza ccm, nccr, cuf, cdm, na upuuzi mwingine kama huo! Ukishangaa ya Musa, utaona ya Firauni! Ndio hayo.
Ila tukithubutu tunaweza, Mungu wetu anaita!

apo nafikiri bado nashangaa ya MUSA mkuu...
 
Kwa mawazo yako ni kwamba watanzania walio nje ya nchi hawana haki kushiriki siasa za nchi yao, siyo?
 
wakuu labda mnisaidie!kuna umuhimu gani wa chama pinzani kuanza kufungua matawi nje ya nchi wakati kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi hii hawajayafikia, ukizingatia watanzania wengi nje ya nchi hawaji kupiga kura wakati wa uchaguzi,na hatuna mfumo wa ON LINE VOTING?? inanitatiza sana hii

Kuna hisi kuwa chama kikiwa na matawi nje ya nchi chaweza kuvuna hela toka kwa wanachama wake walioko huko kwa kukichangia, si hivyo tuu lakini Viongozi wetu wanaopenda kusafiri kila uchao wanapenda kila nchi ambayo wanamaslahi nayo kiuchumi (kule wanakofichia hela wanazoiba hapa home) wanajitahidi waweke kama si watoto wao basi ni vimada wao, kama umewahi kufatilia sana utagundua mara nyingi wanaofungua matawi ya vyama hivi huko ughaibuni ni wale wanaojifanya wanasoma hasa Masters na wengi wao kama si watoto wa mafisadi walioko home basi ni vimada wao (MADEMU) wao au ni wale wale wanaonufaika na mfumo wa kijizi uliopo hapa home.

Na Maafisadi wetu huwa hawaishi kutembelea nchi hizo mara kwa mara, nikupe kesi moja tuu ya VICK Kamata (mbunge Viti maalumu Geita) kwanza alikuwa ni demu wa gamba ingawa naye alikuwa ni kiruka njia lakini labda sura ilimuuza, baada ya kumaliza saut alipelekwa kusoma Ungereza na alipokuwa huko alikuwa ni mmoja wa viongozi wa chama cha baba na mama al maarufu Gamba, baadda ya kumaliza alipwa kazi ya kuwa afisa mahusiano BOT na sasa ni "KITU MAALUMU" mjengoni namtolea mfano kwa sababu namfahamu toka akiwa SAUT alikuwa ni kimada wa niliowataja awali. mwenye mfano mwingineamwage najua ipo...
 
Kwa mawazo yako ni kwamba watanzania walio nje ya nchi hawana haki kushiriki siasa za nchi yao, siyo?

mkuu nadhani hujanielewa tu, nachoomba kujua ni umuhimu wa huo ushiriki uko nje wakati hatujawafikia wengi waliomo humu ndani(tz)
 
ni show za kijinga tu! mbona vyama vya nje hatuoni matawi yake hapa kwetu?
 
Kwa jukwaa hili, subiri matusi, lakini isikutishe, ni bora kupuuzwa na wajinga 1000mil. ila ukaungwa mkono na mwerevu mmoja!

........Kwanini tufuge paka tutarajie kula mayai?
Si tumetaka Demokrasia, wanaojifanya wajanja ndio hao wanaitumia! Walianza ccm, nccr, cuf, cdm, na upuuzi mwingine kama huo! Ukishangaa ya Musa, utaona ya Firauni! Ndio hayo.
Ila tukithubutu tunaweza, Mungu wetu anaita!

Sijui nisemeje?
 
apo nafikiri bado nashangaa ya MUSA mkuu...

Tujiulize tu kwanza...
Kunaweza kuwa na urafiki wowote mwema kati ya mtumwa na bwana wake?
Au, sisi kama sisi tunaweza kupandikiza mamluki wetu ughaibuni? Je, wao kwetu?
Kwani huko siko zinakopotelea mali zetu? Tuna uhakika gani kama hao watakaoongoza matawi nje hawawezi kununuliwa ili watuuze? Mbona waliopo hapa nchini tu wananunulika? Si tumewaona kwenye EPA, Richmond, nk.
Utegemezi, Utegemezi, Utegemezi +Utumwa, Utumwa, Utumwa, zao la UNAFIKI NA ULAGHAI WA WANASIASA WETU!
Mungu wetu anaita!
 
Wana forum na wataalamu wa siasa za bongo naombeni mnijuze hili swala manake sielewi, je kuna umuhimu gan wa vyama vya siasa kuwa na matawi nje ya nchi? Na je wanachama wanaweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi? may be online voting?

Hiv kuna nchi yeyote ya dunia ya kwanza ambayo vyama vyake vya siasa vina matawi nje ya nchi? (to be specific ni Africa)
 
Idea ya kuanzishwa kwa TANU ilitokea kwa watanganyika waliokuwa Burma. Waliporudi nyumbani jitihada zikaanza, vikazaliwa vyama vya awali and later TANU.
 
Mie nami nimejiuliza sana swali hili, nikaona ufanisi wa matawi haya utakuwa mdogo kutokana na mazingira ya kuwa mbali na wananchi.

Lakini pia nikatambua kwamba kukataa matawi ya vyama nje ya nchi ni kuwanyima Watanzania walio nje ya nchi haki yao ya kikatiba ya kujumuika kwa madhumuni ya pamoja ya kisiasa.

Mbali na vyama kuwa ndani au nje ya nchi, kwa kuangalia majibizano ya sasa ya kisiasa, nimefikia wakati wa kujiuliza umuhimu wa vyama kabisa.
 
Idea ya kuanzishwa kwa TANU ilitokea kwa watanganyika waliokuwa Burma. Waliporudi nyumbani jitihada zikaanza, vikazaliwa vyama vya awali and later TANU.
Zemarcopolo,
That is a good one. Halafu hakuna ubaya kila mahali walipo Watanzania kuji organize kuzungumzia masuala ya nyumbani na kutoa mchango wao kama utahitajika. Nakumbuka mwaka 1979 Mwalimu Nyerere pale London aliwahimiza wanafunzi kushiriki katika mijadala ya kusaidia kujenga nchi yao hata kama wako nje ya nchi. Akakumbushia kuwa hata yeye alipokuwa mwanafunzi alijitahidi kujielimisha juu ya nchi yake na kwa kukutana na Waafrika wengine kutoka diaspora akapata mwamko wa kuikomboa Tanzania.
 
Mie nami nimejiuliza sana swali hili, nikaona ufanisi wa matawi haya utakuwa mdogo kutokana na mazingira ya kuwa mbali na wananchi.

Lakini pia nikatambua kwamba kukataa matawi ya vyama nje ya nchi ni kuwanyima Watanzania walio nje ya nchi haki yao ya kikatiba ya kujumuika kwa madhumuni ya pamoja ya kisiasa.

Mbali na vyama kuwa ndani au nje ya nchi, kwa kuangalia majibizano ya sasa ya kisiasa, nimefikia wakati wa kujiuliza umuhimu wa vyama kabisa.

Mkuu Kiranga,
Swali hilo tunajiuliza wengi, ndio maana wakati fulani nilisema haya https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-vyama-vingi-na-katiba-ya-chama-kimoja.html
 
Hao waliopo nje ni Watanzania na inawahusu sana mienendo ya nchini kwao kwa mustakabali wao na wa watoto zao huku nyumbani.

Sema nawasikitikia Watanzania wa nje wanapoamuwa kujiunga na chadema, vimichango vyao vya kujenga chama vikifika huku, vinakopwa na mjanja mmoja. Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
kuna jambo moja halizungumziwi hapa
wanachama wa vyama hivi amba wana uraia wa nchi mbili
hasa kama chama husika kinapinga hili la uraia wa nchi mbili
 
Idea ya kuanzishwa kwa TANU ilitokea kwa watanganyika waliokuwa Burma. Waliporudi nyumbani jitihada zikaanza, vikazaliwa vyama vya awali and later TANU.
The idea of establishing CHADEMA is home grown. The idea of establishing branches abroad is "hopeless" particularly because Tanzania communities abroad contitute in most cases of people who are just surviving there...that is Tanzanian community have failed to cross economic boundaries and make a significant mark abroad particularly in USA and UK.In addition most of the Tanzanians seen in the so called branches abroad are petty orpurtunists who wants a ticket to come home as political leaders which in anyway you want to look at it is absurd.
 
Kwa sababu mzee Mtei ni member hapa, anaweza kutusaidia kwenye hili, idea ya kuanzisha CHADEMA aliipata akiwa wapi na harakati za awali alizianzisha akiwa wapi, you will be surprised!
 
Kwakweli binafisi sioni sababu zozote zaidi ya ghasia tu. Chadema nadhani wameingia mkenge wa CCM, kwakuwa chama tawala kinajua kinafanya uozo mwingi hofu yao nadhani ni vijana wanaosoma nje wakirudi wengi wao huwa si mabwege tena na huona kasoro za uongozi wetu.

Nadhani ni fikra ya kuwaweka vijana wasomi ndani ya chama hili hata kama malalamiko yao yawe within the boundaries and be contained maana kuna so much bureaucracy within ya kutowasikiliza, hivyo ni bora kulikoni hawa jamaa wakiwa majukwaani kuwakosoa mfano embu jiulize JF member "Mchambuzi" angekuwa anatoa attacks za uozo wa chama majukwaani ingenguaje mi nadhani angekuwa more effective kuwaelimisha watanzania kulikoni watu wengi ambao wapo JF ambao tayari wanayajua hayo.

Lakini kwa yeye kuwa being a member of the party his ideas are contained to a small audience. Hiyo ndio strategy yao, kuna wanachama wa CCM ambao wapo UK nawajua wamepiga vitabu na ni maloya wa mikataba kutoka vyuo vya maana including oxford wanabaki wakilalamika kuhusu uozo wa chama na wakijaribu ubunge, no support from the party, yaani chama kiko tayari kumuweka darasa la samba kuliko oxford graduate (fact) kwakuwa wanajua ni trouble but there happy to contain him within.

Sasa chadema sijui strategy yao ni nini hasa maana watu mnaowanadia chama huko ingawa wamechoka na uozo lakini si mabwege kama huko vijijini mnapoenda, usidhani haya matusi na ushabiki wa kijinga ndio itakuwa mvuto people want to hear sound arguments na sio ushabiki wa kishamba shamba kuhusu chama. Pengine ndio sababu wengi wanona platform ni CCM tu ni kusubiri na kuvuta muda.

And hoo-yeah before i forgot ufaransa wameweka mmbunge wao kwa wafaransa wanaoishi uingereza apparently idadi ya raia wanoishi uingereza ya wafaransa inafanya london huwe mji wa sita yenye idadi kubwa ya wafaransa idadi hiyo ni kubwa kuliko miji ya Bordeaux, Nantes and Strasbourg.

Na kwa kweli kuna watanzania wengi sana UK its time sasa kuwe na mmbunge wakutambulika maana kuna matatizo mengi sana ambayo watu wanakumbana nayo kutokana na sera za nyumbani na jamaa wa ubalozini wanatabia mbaya sana wengine bila ya explanations not to forget wabunge huko Dodoma sidhani kama wanaelewa sawasawa matatizo ya diaspora katika sheria ambazo CCM inapitisha kujilinda na hili kundi.

Wakileta swala la mmbunge wa diaspora hapo sasa ndio siasa kweli zitakuwa zipo huko ugenini vinginevyo wala msiangaike na wapuuzi wengi ambao ni opportunist tu wanao taka stepping stone into politics under the current administration.
 
Hizo ni siasa uchwara za kitanzania. Maana ukichunguza hawa wanaojiita viongozi wa matawi ya nje ni watu walioshindwa maisha huko ughaibuni sasa wanatafuta jinsi ya kuepuka aibu na kupata sababu ya kurudi nyumbani. Mmojawapo ni WJ S Malecela aliyeshindwa maisha huko New York. Hakuna mpuuzi aliniudhi kama yule anayejiita katibu wa tawi la CCM la DMV kihiyo fulani anayejikomba kama changu kwa CCM. Bahati mbaya hata CDM wameingia mkenge na kuanzisha upuuzi huu wa matawi ya nje. Matawi ya nchini hamjayaimarisha mnakimbilia ya nje? Ukienda mikoani kuna sehemu bado watu wanajua rais wa Tanzania ni Nyerere hawajui CCM wala CDM bali Tanu. Nendeni kwa hao badala ya kupoteza nauli zenu kwenda nje au ni utalii wa wanasiasa? Kweli huu ni usanii.
 
Back
Top Bottom