Vyama vya Siasa fundeni watu wenu

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kama Kuna Jambo litakalonipa amani wakati huu wa uchaguzi ni kuona wanasiasa wanajikita kwenye siasa za masuala( politics of issues).

Na kweli kiasi unaweza ona wanasiasa cut across wanaeleza issues.

Tatizo ninaloliona ni mashabiki wao au wanachama ukipenda. Wengi hawafuatilii issues na naona Kama wanakuwa kwenye mikusanyiko ili wajioneshe ukereketwa wao, au tu kwa maoni yangu,, wafanye fujo unnecessarily. Wakati mgombea wa chadema alipokuwa anahutubia Dodoma baada ya kuchukua fomu, ukisikilize ile clip, Kuna sauti zilikuwa zinaonyesha kuunga mkono alokuwa anasema Lisu, lakini mwitikio haikuwa ndiyoo au hata kusema ni sawaaa au kupiga makofi. Badala yake, unasikia watu wakitukana na wakikashifu Kama kiitiko (echo) Cha aliyosema mgombea.

Kwangu Mimi huo sio usitaarabu na siyo siasa za kistaarabu. Najua wakati mwingine ni vigumu kudhibiti watu, hasa wenye hamasa, lakini ukweli kuacha watu kutukana na kuongea Mambo yasiyofaa katikati ya hotuba siyo vizuri.

Ndo maana napenda style ya Mbowe kiasi. Anapokuwa anaongea Mara kadhaa nimemsikia akikemea na kutahadharisha hadhira yake kutopiga kelele unnecessarily, bali wakae kimya.

Kuna hatari ya kuwa branded majina mabaya Kama wahuni, wenye fujo, uncivilised, nk kwa baadhi ya vyama Kama hamtachukua tahadhari hiyo.

Matusi, dhihaka kwa viongozi wa nchi, recklessly, inayofanywa na mashabiki inaondoa umakini (seriousness) na baadae itakufanyeni kuonekana hamko mature katika Mambo yenu.

Nategemea kuona wahutubiaji wakitawala (take charge) majukwaa kwa maana ya kuleta order na sanity wanapohutubia. Kumbuka ukiwa jukwaani unahutubu, wewe ndo main player. Hakikisha, sanity, order na integrity ya mkutano inakuwepo. Inakubidi hata kuamuru mashabiki waliozidisha ukereketwa kuacha.

Vinginevyo, baadhi tutaacha kuwasikiliza maana hatupati madini yanayotupeleka huko, bali matusi, kejeli, na kelele zisizo na maana.

Wasaalamu.
 
Na wewe jiu
Tena muulize zuio la kuwazuia watu kufanya siasa kwa miaka 5 lilifanyika chini ya kifungu gani cha sheria???
Na wewe jiulize ni kifungu gani kinakuruhusu wewe kuacha jimbo lako na ukafanye siasa jimbo lingine lisilo lako?
Na kama kipo kinawaruhusu, kwa nini hukwenda mahakamai kudai haki yako?
 
Na wewe jiu
Na wewe jiulize ni kifungu gani kinakuruhusu wewe kuacha jimbo lako na ukafanye siasa jimbo lingine lisilo lako?
Na kama kipo kinawaruhusu, kwa nini hukwenda mahakamai kudai haki yako?
Hujui kuwa kama hakuna sheria inayokataza maana yake sio kosa??? Umetoka shule za kata za CCM nini??? Mbona upeo wako mdogo ivo???
 
Back
Top Bottom