Kenya 2022 Vurugu zanukia Kenya, mawakala wa Odinga waishtumu tume kufanya uhalifu

Kenya 2022 General Election
The trend is as if they are digging their own grave. Riots and violence are likely to happen and this time things might go beyond 2017 post elections.
 
Hiyo sio hoja kwenye kupiga kura kila chama kina wakala pili wakihesabu pamoja na kupiga picha matokeo tatu kura zinajumlishwa kijimbo na ile total ni rahisi kila chama kuhakiki baada ya hapo ndipo ile fomu na 34a na 34b inaletwa .makao makuu ya tume na tume inahakiki kama ile jumla iliyoletwa katika fomu na 34b inalingana na ile jumla iliyotoka kule shinani walikopiga kura yaani inztokana na fomu 34a. Sasa hata kama wakikosea kwa bahati mbaya kusahihisha inakuwa rahisi kwani kila wakala wa chama anajua jumla hivyo marekebisho yanafanyika hivyo mwanya wa fujo haupo kwani kila kitu kipo wazi. Pia aliyeshindwa anaweza kwenda mahakamani na ushahidi na mahakama ikatengua.

Raila ameishajua ameshindwa ndio maana jana waliitisha mkutano na makamu wake akautangazia umma kuwa Raila ndiye aneshinda na kuja na hoja nyepesi kuwa wameshinda viti vingi vya ubunge na ugavana wakati wanajua fika hata kwa ushahidi wa matokeo kuwa kuna majimbo yamechagua wawakilishi toka kambi tofauti kwa jimbo hilo hilo. Kama Rsila anajua kuwa ameshinda na kama hatatangazwa anaogopa nini kwenda mahakamani pale matokeo yatakapotangazwa?

Rjto ndiye Rais
Umeongea ukweli mtupu, Tume imefanya kazi nzuri sana na kila kitu kipo wazi
Raila na wenzake wanajua wameshindwa na ndio maana wanafanya vihoja ili kuchochea wananchi wasiiamini tume na kuleta vurugu
 
Mwisho unasema Ruto ndiye rais wakati hata tume haijatangaza ,usipende kubuni vitu kwa ajili ya ushabiki mandazi weka kalio chini subiri matokeo.
Kila kitu kipo wazi mkuu, matokeo yote yapo online na yoyote anaweza ku download na kujumlisha
Raila anajua matokeo halisi yapoje ndio maana analeta uchochezi
 
Hahaaa usha ingoa kwenye Portal ya tume yao? Fomu zote ziko mule wanacho fanya sasa ni kuhakikisha hard copy basi, hakuna kingine, Ile sio NEC yenu inayo ongoza maiti za Kitanzania
Sasa Tanzania na Kenya nani maiti ? Mbona mnapenda kujitusi
 
Mnaombea itokee vurugu mpate kwa kuanzia?Bado.Kenya wameizidi Tanzania mbali sana izungumzwapo demokrasia.Tuna la kujifunza.Hajauliwa wala kupotezwa mkinzani.Intaneti ipo vema.Na wala Chebukati hajafuta uchaguzi ingawa Raila amedai yeye ni mshindi.
NB:Hivi Jecha yupo nchi hii?


Nilipata kuambiwa Jecha yupo Kisaki huko Morogoro!!!, sijui kama ni kweli.
 
Huyu Mzee Chebukati naye ni shida tupu.

Miaka zaidi ya tano yote yeye na tume yake hawakuweza kujipanga kuondoa makosa ya hovyo hovyo katika muundo wa uchaguzi?

Matatizo yanaweza kuanzia kwa hawa wajumbe wa tume ya uchaguzi.
Wakati huu ilitakiwa kila kitu kiwe kimekamilika, wao wanajivutavuta na kutia wasiwasi katika uchaguzi mzima.
Bado vijimakosa hivyo huwezi kufananisha na uhuni wa dhahiri ufanyikao Tanzania.Bado.
 
Huyu Mzee Chebukati naye ni shida tupu.

Miaka zaidi ya tano yote yeye na tume yake hawakuweza kujipanga kuondoa makosa ya hovyo hovyo katika muundo wa uchaguzi?

Matatizo yanaweza kuanzia kwa hawa wajumbe wa tume ya uchaguzi.
Wakati huu ilitakiwa kila kitu kiwe kimekamilika, wao wanajivutavuta na kutia wasiwasi katika uchaguzi mzima.
Wakati wa uchaguzi huwa kuna 'temper' ya hali ya juu mno hasa ushindani unapokuwa mkali, mara nyingi lawama hutupiwa maafisa wa tume tu ila pia wagombea na mawakala wao huweza kuwa moja ya sababu za mivutano.
 
Back
Top Bottom