Mahakama yatupilia mbali Rufaa ya Odinga, yakubali Ruto ameshinda kihalali Urais wa Kenya, leo Jumatatu Septemba 5, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,306
5,452
MARTHA KARUA: NAHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA ILA SIKUBALIANI NAYO​

Aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Azimio la Umoja katika Uchaguzi wa Urais Kenya, Martha Karua amesema anaheshimu maamuzi ya Mahakama lakini hakubaliani nayo.

Mahakama ya Upeo imetangaza kupitisha matokeo yaliyompa ushindi William Ruto kuwa Rais Mteule wa Kenya na kutupilia mbali rufaa ya Raila Odinga aliyepinga matokeo ya uchaguzi huo wa 2022.

Tumbe ya Uchaguzi na Mikapa (IEBC) chini ya Mwenyekiti Wafula Chebukati ilimtangaza Ruto kuwa mshindi kwa kura 7,176,141 sawa na 50.49% ya kura zote za Urais zilizopigwa dhidi ya Odinga aliyepata kura 6,942,930 (48.85%).

===================

The Supreme Court Monday afternoon upheld the election of William Samoei Ruto as Kenya’s fifth president, summing up the meteoric rise of a man who defied his boss and the sitting administration to be the country’s youngest Head of State.

The Chief Justice Martha Koome-led Bench unanimously threw out a petition by Azimio la Umoja One Kenya Coalition candidate Raila Odinga, who argued the declaration of Dr Ruto was null and void.

Justice Koome said that the court will issue a summary, and then give the full judgment after 21 days.


===============================

Mahakama ya Upeo nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi siku ya Jumatatu kuamua kuhusu masuala yaliyoibuliwa na walalamishi kuhusu uadilifu wa uchaguzi wa Agosti 9 na uhalali wa kumtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa Rais mteule.

Iwapo wengi wa majaji watatupilia mbali malalamiko yalioibuliwa na Mgombea wa Urais kupitia Muungano wa Azimio One Kenya, Raila Odinga na kuunga mkono matokeo yaliyotangazwa na baraza la uchaguzi, Rais Mteule William Ruto basi ataapishwa Septemba 13 kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta na kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya .

Lakini iwapo watabatilisha ushindi wa William Ruto mamlaka zitakuwa na siku 60 kufanya uchaguzi mpya iwapo mahakama itatoa uamuzi unaomuunga mkono Odinga, ambaye tayari amepinga matokeo ya urais mara tatu katika maisha yake ya kisiasa ya muda mrefu na kuyataja matokeo ya kura ya hivi punde kuwa "upotovu".

Na Iwapo mahakama itakubali maombi ya Raila Odinga ya kutaka mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati afunguliwe mashtaka na kuzuiwa kuendesha uchaguzi wa marudio, itachukua muda mrefu kufanya uchaguzi mpya.

Tayari baadhi ya wakenya wameelezea kukosa imani na Tume ya IEBC kufuatia migawanyiko ya ndani, ambayo imeshuhudia kundi moja la makamishna wakikataa matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti Wafula Chebukati .

Wiki iliyopita kundi la Muungano wa Azimio One Kenya pamoja na wanasheria wa Odinga waliwasilisha kesi wakidai kuwa mfumo wa uchaguzi Nchini kenya ulikubwa na dosari nyingi pamoja ya Uingiliwaji wa Teknolojia za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC n na kubadilisha picha halisi za fomu za matokeo ya vituo vya kupigia kura na kuweka za uwongo, hivyo basi kuongeza mgao wa Ruto katika kura ya Agosti 9.

Aidha ombi la Odinga pia lilidai kuwa matokeo ya Urais ni batili kwa sababu yalitangazwa na mwenyekiti badala ya tume nzima huku Odinga akitaka mwenyekiti wa IEBC abadilishwe.

Kwa upande wa Mawakili wa IEBC na William Ruto walimshutumu Odinga kwa kughushi kumbukumbu za kompyuta ili kuleta mgogoro wa kikatiba na kulazimisha makubaliano ya kugawana mamlaka.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema uchaguzi ulikuwa "huru, haki na wa kuaminika" katika majibu yake ya mahakama huku Makamishna wanne wapinzani wakiwasilisha majibu ya kuibua wasiwasi kuhusu mchakato wa kujumlisha kura na mienendo ya mwenyekiti.

Baada ya kusoma maombi yaliowasilishwa, Mahakama ya Upeo ikiongozwa na Jaji Mkuu na Rais wa Mahakama ya Juu Martha Koome ilipunguza madai na kadhia nyingi katika kesi nane za kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 hadi masuala tisa ambayo matokeo yake yataamua iwapo Ushindi wa Ruto utaidhinishwa.

Baada ya kukamilika kwa mvutano wa mawakili, macho yote sasa yanawaangazia majaji hao kutoa uamuzi ambao utaamua mustakabali wa taifa la Kenya.
----

Kenya's Top Court To Rule On Disputed Presidential Election
Kenya's Supreme Court will decide on Monday whether to uphold or nullify the result of last month's presidential election, a ruling anxiously awaited in a country scarred by previous bouts of poll-related violence.

The seven-member court will rule following three days of oral arguments last week by lawyers representing the two main candidates and rival camps of election commissioners.

Opposition leader Raila Odinga, making his fifth presidential bid, says Deputy President William Ruto's narrow win was the product of massive fraud. Four out of seven election commissioners disowned the result announced by the commission chairman, saying the tallying had been opaque. read more

The Supreme Court made history in the last election in 2017 by annulling President Uhuru Kenyatta's victory over Odinga because of procedural irregularities.

Kenyatta prevailed in a re-run that Odinga boycotted.

About 100 people were killed in election-related clashes that year. This time, protests briefly broke out in several Odinga strongholds after the election commission chair declared Ruto the victor on Aug. 15, but Odinga urged supporters to stay peaceful and the streets have remained calm since.

Tempers have mainly flared online, where Odinga and Ruto's partisans have bombarded social media with often outlandish claims and counter-claims.

Source: VOA & Citizen Digital

================
 
Naomba Sana was Kenya mkubaliane na matokeo yoyote itakYopatikan na kuleta kwenu
 
Leo wanatoa tu mwelekeo wa hukumu.. Hukumu rasmi itasomwa baada ya siku 21

Majaji wanaohusika wako 7
Itabidi wakubaliane kwa wingi wa kura, wakishindwana kabisa itabidi kila jaji asome hukumu yake
Na kil hukumu ya mmoja itatoa hutimisho either, uchaguzi urudiwe, ama Ruto mshindi..conclusion zitabase hapa..kwa kuwa the no of judges is odd. Therefore a winner in decision lazima apatikane. Ila Wakenya wametuacha mbali kwa Usomi, Usomi huku kwetu ni matumboni tu.
 
Hukumu ya Mahakama ya Juu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kuhusu Pingamizi la Urais itatolewa leo Jumatatu, Septemba 5, kuanzia saa 6:00 mchana

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msajili wa Mahakama ya Juu ya Kenya, Letizia Wachira, jopo la majaji 7 linatarajiwa kutoa uamuzi huo katika Mahakama ya Milimani Law.

Majaji hao ni pamoja na Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Isaac Lenaola, Smokin Wanjala, Ibrahim Mohammed, Njoki Ndungu na William Ouko.

"Fahamu kuwa hukumu katika ombi hili itatolewa Jumatatu, Septemba 5, 2022, saa sita mchana katika Mahakama ya Juu ya Kenya Milimani Law Courts," ilisomeka sehemu ya notisi hiyo.

Raila Odinga wa Azimio na Martha Karua waliwasilisha ombi la kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais kumpendelea rais mteule, William Ruto.

Miongoni mwa masuala ambayo Raila aliyataja katika ombi lake ni pamoja na; Ruto hakupata asilimia 50 pamoja na mahitaji ya kura moja, akisema kuwa matokeo kutoka maeneo bunge 27 yalikuwa bado hayajahesabiwa na kuthibitishwa kufikia wakati wa tangazo hilo.

Azimio pia alidai kuwa IEBC haiwezi kuhesabu kura 250,000, bila kujumuisha kura zilizopigwa. Raila na mgombea mwenza waliitaka mahakama kuu kuwatangaza rais mteule na naibu rais mteule mtawalia.

Raila pia alitaka ukaguzi wa kina na wa kitaalamu wa vifaa na teknolojia zote zilizotumiwa na tume ya uchaguzi katika uchaguzi wa urais. Raila pia alitaka Chebukati atangazwe kuwa hafai kushikilia wadhifa wa umma.

KENYANS
 
20220905_095022.jpg


Hukumu ya Mahakama ya Juu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya pingamizi la matokeo ya Rais itatolewa Jumatatu, Septemba 5, saa sita mchana.

Kulingana na notisi kutoka kwa msajili wa Mahakama ya Juu ya Kenya, Letizia Wachira, benchi la majaji saba litatarajiwa kutoa uamuzi huo katika mahakama za Milimani Law.

Majaji hao ni pamoja na Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Isaac Lenaola, Smokin Wanjala, Ibrahim Mohammed, Njoki Ndungu na William Ouko.

"Fahamu kuwa hukumu katika ombi hili itatolewa Jumatatu, Septemba 5, 2022, saa sita mchana katika Mahakama ya Juu ya Kenya Milimani Law Courts," ilisomeka sehemu ya notisi hiyo.

Raila Odinga wa Azimio na Martha Karua waliwasilisha ombi la kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais kumpendelea rais mteule, William Ruto.

Miongoni mwa masuala ambayo Raila aliyataja katika pingamizi lake ni pamoja na; Ruto hakupata asilimia 50 pamoja na mahitaji ya kura moja, akisema kuwa matokeo kutoka maeneo bunge 27 yalikuwa bado hayajahesabiwa na kuthibitishwa kufikia wakati wa tangazo hilo.

Azimio pia alidai kuwa IEBC haiwezi kuhesabu kura 250,000, bila kujumuisha kura zilizopigwa. Raila na mgombea mwenza waliitaka mahakama kuu kuwatangaza rais mteule na naibu rais mteule mtawalia.

Raila pia alitaka ukaguzi wa kina na wa kitaalamu wa vifaa na teknolojia zote zilizotumiwa na tume ya uchaguzi katika uchaguzi wa urais. Raila pia alitaka Chebukati atangazwe kuwa hafai kushikilia wadhifa wa umma.
 
Hakuna sababu ya kufanya ghasia maana mahakama zenu ni independent. Dunia nzima inajua hivyo na hivyo uamuzi wa leo itakuwa sahihi. Supreme Court ina rekodi nzuri.

Siyo kama kwa jirani zenu ambako dunia nzima pia inajua kuwa judiciary is highly compromised.
 
Wakenya wanaanza safari mpya ya kupata uzoefu mpya wa rais mpya na maisha yaleyale ya zamani

Hivi bei ya unga imefika ngapi sasa
 
Back
Top Bottom