Vurugu Tegeta, msafara wa JK waathirika pia (Dar)

Lukolo mbona unakuwa kama mjinga... hivi mfano bara bara kama ile watu wasipopisha huo msafara kwa kuendelea na magari yao kama kawaida, atapita wapi? Wakipark bara barani atapita wapi? wakiweka mawe, magogo atapita wapi? wakilala bara barani atapita wapi? Jamani hata hili tunahitaji Phd zenu za kubumba?

kwa formula ya CDM inawezekana kwa zile za usalama si kazi nyepesi kuzuia msafara wa Rais kama unavyozuia raia wa kawaida.... kumbuka kabla Rais hajapita njia imejaa wanausalama wenye mavazi na wasio na mavazi.

kabla hajazuiawa taarifa zinafika...
 
Watu wasiojukikana walikuwa na nia gani wamezuia msafara wa Rais uliolukuwa unapita maeneo ya Namanga.

Watu hao walizuia kwa muda wa sakika kadha hivi kabla ya FFU kutinga maeneo hayo na kuwatimua na ndipo msafara ukapita mpaka sasa FFU wapo kwenye purukushani ya sombasomba maeneo hayo ya namanga.

Chanzo Nimepita hapo muda sio mrefu.

UKWELI:
watu wamechoka kuonewa na maeneo yao kudhulumiwa na matajiri.
 
kwa formula ya CDM inawezekana kwa zile za usalama si kazi nyepesi kuzuia msafara wa Rais kama unavyozuia raia wa kawaida.... kumbuka kabla Rais hajapita njia imejaa wanausalama wenye mavazi na wasio na mavazi.

kabla hajazuiawa taarifa zinafika...

Mama Porojo, naomba nikuulize swali rahisi, msafara wa rais, tena huyu aliye madarakani haujawahi kuzuiwa na wananchi?Mpaka akaongea nao? kma jibu ni Yes, ilikuwaje?
 
Mmmh, sijui maana kwa ule msafara wa Rais unavyokuwaga, sioni kabisa hiyo nafasi ya wananchi kuweza kusimama tu barabarani na kuzuia, otherwise waliambiwa kwamba Rais angepita maeneo hayo. Na sijui wakati wa kuzuia barabara walianzaje, ina maana walizuia na magari ya kawaida? Anyway sijui, but nafikiri ni jambo gumu sana, bora mngesema wameupopoa kwa mawe, lakini si kuzuia.

Hakuna linaloshindikana chini ya jua hasa pale mlalahoi anaposema amechoka! Elewa wananchi wamemchoka JK ingekuw ni amri yao kuchagua kiongozi mwingine now wangefanya hivyo. Kuuzuia msafara wa rais ni kazi ndogo sana watu wakiamua. Ingekuwa mie ndio JK ningesoma alama za nyakati pia elewa watu wanjaua ratiba yake kuwa leo lazima aende mlingotini kila Ijumaa njia anayotumia ndio hiyo hiyo mara zote.

"DHAIFU" hapendwi tena watu wamemchoka na serikali yake "LEGELEGE!"
 
Mambo mengine mleta Mada kachanganya habari. Mosi kulikuwa na Uvunjaji wa nyumba hapo Namanga- Tegeta kwa hiyo kulikuwa na Mabaunsa waliokuwa wakifanya fujo ndipo Polisi wakaingilia kati. Kupita kwa Rais hakuna uhusiano na tukio hilo

siasa ndugu ziko kila sehemu kutufanya sisi wajinga
 
Mods hii ingeenda kule kwenye udaku + utani ingependesa sana aisee :A S shade:
 
Mama Porojo, naomba nikuulize swali rahisi, msafara wa rais, tena huyu aliye madarakani haujawahi kuzuiwa na wananchi?Mpaka akaongea nao? kma jibu ni Yes, ilikuwaje?
Ninatamani kujibu kwa niaba ya MAMA POROJO sina uhakika kama kuna mahali msafara wa rais uliwahi kusimamishwa na yeye akakubali kusimama bila ruhusa ya wana usalama. Msafara wa Rais umekuwa mara nyingi ukizuiwa wakati wa kampeni na si wakati akiwa yupo kwenye shughuli za kikazi. Hata wakati wa kampeni kwenyewe kuna baadhi ya maeneo ambayo Rais halazimika kupunga mikono tu na si kusimama. Yote hayo yanategemeana na taarifa za wanausalama. Hivi msafara wa Rais muusimaishe tu popote akiuawa? Au hujui kwamba kila anachokifanya ni lazima kihakikiwe na vyombo vya usalama? Taratibu mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Msafara WA rais umezuiwa NA wananchi maeneo ya tegeta basi haya NA watu wawili wamelipotiwa kufa akiwemo asikari WA usalama NA mwananchi mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: PPM
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom