Vurugu Tegeta, msafara wa JK waathirika pia (Dar)

Vurugu Tegeta, msafara wa JK waathirika pia (Dar)

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,196
Reaction score
11,624
Watu wasiojukikana walikuwa na nia gani wamezuia msafara wa Rais uliolukuwa unapita maeneo ya Namanga.

Watu hao walizuia kwa muda wa sakika kadha hivi kabla ya FFU kutinga maeneo hayo na kuwatimua na ndipo msafara ukapita mpaka sasa FFU wapo kwenye purukushani ya sombasomba maeneo hayo ya namanga.

Chanzo Nimepita hapo muda sio mrefu.

UHALISIA:
Pale Namanga kuna sheli ya BigBon iko barabarani kwa nyuma yake amepakana na nyumba za wanakijiji, sasa yeye anadai kanunua hilo eneo lote na anamiliki hati wanakijiji wamesema hawamtambui wala hawajawahi kuuza kwa mtu eneo hilo, kesi ilikwenda baraza la ardhi kwa mbinu na hila akafanikiwa kushinda kwani baraza hilo halina haki kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.

Wananchi wameamua kuipeleka kesi mahakama kuu na wameshatoa notisi ya siku 90 kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili kuishitaki wizara ya ardhi, kuna kesi nyingine ya madai ameshtakiwa mahakama kuu kitengo cha ardhi na mzee mmoja amepakana nae kwenye hilo eneo kwa kumuingilia na kuharibu mali zake zote kwa kudai (BigBon) kuwa eneo hilo ni lake. kesi imepangwa kusikilizwa July.

Leo hii BigBon akijua fika kua kuna kesi mahakamani na hazijasikilizwa bado amepeleka kikundi cha mabaunsa kwenda kuvamia kwa nguvu eneo hilo la wanakijiji kwa lengo la kuwatoa, ndipo vita kali baina ya mabaunsa hao na wanakijiji ilipozuka kwa taarifa nilizozipata, zaidi ya mabaunsa wanne wameuliwa na wanakijiji ila kwasasa hali imetulia.

Wakati vurugu hizo zikiendelea na msafara wa rais ulikuwa ukipita maeneo hayo hakuna uhusiano wowote kati ya vurugu hizo na msafara huo, ila ilikua ni jambo la heri kwani msafara huo ulisaidia kuzima vurugu hizo baada ya askari wa FFU kufika katika eneo hilo na kuanza kutawanya watu...

Source: taarifa kutoka kwa mzee mmoja mwanakijiji ambae nae ni mmojawapo kati ya wanakijiji wanaogombania eneo na BigBon
Source: RADIO ONE
WANANCH WALIKUWA WANAGOMBANA WAKILALAMIKA NYUMBA ZAO KUVUNJWA NA ENEO KUUZIWA MMILIK MMOJA WA MAFUTA

VURUGU ZILIANZA KABLA HATA YA MSAFARA WA RAIS KUFIKA ENEO LILE

KWAHYO SI KWAMBA WANANCH WALIJIPANGA KUZUIA MSAFARA BALI WALIKUA NAVURUGU ZA HAPANAPALE KUZUIA NYUMBA ZAO ZISIVUNJWE.
 
ni namanga ya tegeta njia ya kuelekea bagamoyo..ni kituo kimoja tu toka tegeta kibaoni....nimeskia milipuko kadhaa muda si mrefu nahisi yatakuwa mabomu ya machozi...hali si swari sana maeneo haya kwa sasa
 
asanteeee....
 
Ni upepo tu utapita

liwalo na liwe.

Jk ni dhaifu
 
popoa mawe kabisa alikuwa anaenda wapi si tunahangaika

Watu wasiojukikana walikuwa na nia gani wamezuia msafara wa Rais uliolukuwa unapita maeneo ya Namanga.

Watu hao walizuia kwa muda wa sakika kadha hivi kabla ya FFU kutinga maeneo hayo na kuwatimua na ndipo msafara ukapita mpaka sasa FFU wapo kwenye purukushani ya sombasomba maeneo hayo ya namanga.

Chanzo Nimepita hapo muda sio mrefu.
 
Asanteee wananchi. Ajue hali halisi iliyopo mtaani sio kilasiku kuletewa taarifa za uongo tu ikulu.
 
hata kama ni ya kutunga ila ni hatua inayotakiwa kuchukuliwa hasa pale atakapokuwa anataka kuelekea Airport inabidi tumzuie
 
Back
Top Bottom