Vurugu kubwa kariakoo

Vurugu kubwa kariakoo

...kamanda wapi hiyo jomba..
Kamanda, mambo ya Kitunda, Banana, Kipunguni kwa wauza mayai Mulla. Huku hata TRA, SUMATRA na EWURA ni magheshi! Tupo hapa nyuma ya kituo cha Banana Mulla, unapata kitimoto mchicha wangu! Achaa acha kabisa aisee bora wafe askari polisi 6 kuliko Mkurya mmoja raia mulla!
 
Acha uongo wewe...

Kilichotokea ngoja niwafahamishe wanabodi. Leo ni mapumziko kiserikali kutokana na sikukuu. Machinga siku kama hizi huwa wanakuwa free kupanga bidhaa zao kwa kuwa mgambo wa city hawapo.

Kilichotokea mgambo wa city wakajikusanya kwenda kutafuta pesa kwa machinga, polisi mmoja akijitokeza na kuwambia mgambo hebu waachieni leo wafanye kazi sikukuu.

Basi wale mgambo wakampiga yule askari. Yule askari ndiyo akawaita askari wenzake ndiyo ikaanza piga nikupige wale mgambo wakakimbia, machinga wakaingia mitaani kuwasaka migambo kisha wanawaita polisi.

Mgambo wote wamekimbia kariakoo.

Mkuu hakuwaita police wenzake,policejamii ndo
Wamefanya kazi.wamachinga wale wanapanga kila siku bidhaa...
 
Nyenyere; Hebu dadafua kwa undani zaidi habari hz na ututundikie ipasavyo kwa kuediet post ya awali!


Habari nillizozipata jana kuna chinga mmoja alipigwa sana na wagambo wa jiji bila sababu. Akaenda kushitaki polisi msimbazi. Leo afisa mmoja wa polisi akiwa hajavaa uniform akamchukua huyo chinga ili amwonyeshe hao mgambo waliompiga. Badala yake wale mgambo wakamchapa sawa sawa yule afisa na kumnyanganya bunduki yake.


Hao ndiyo mgambo wa ccm jamani!
 
Last edited by a moderator:
Sasa hizo siku 9 ni kiboko, kuna mtu mmoja amenitonya kuwa huenda damu ikamwagika kuanzia kesho, kwani mgambo hawakubali kitendo walichotendwa. Na wanadai wanawafahamu vema machinga husika. Yetu macho na masikio.
 
Mmenikumbisha wimbo wa Sajna_Iveta. sasa leo ni polisi anakimbizwa.
 
Habari nillizozipata jana kuna chinga mmoja alipigwa sana na wagambo wa jiji bila sababu. Akaenda kushitaki polisi msimbazi. Leo afisa mmoja wa polisi akiwa hajavaa uniform akamchukua huyo chinga ili amwonyeshe hao mgambo waliompiga. Badala yake wale mgambo wakamchapa sawa sawa yule afisa na kumnyanganya bunduki yake.

then ikawaje? Maana utunzi wako unaweza ukawa hauna maana!
 
Taarifa zikamfikia mkuu wa kituo. Akawapa mamlaka wamachinga woote wa kariakoo kuwasaka mgambo wa city popote walipo na wampelekee kituoni, bila kujali wako katika hali gani.

ndicho kilichobaki baada ya policcm kushindwa kutimiza wajibu wao na kusubiria maandamano ya watu kudai haki yao ili wawapige mabomu
 
....na hiki kipigo soon kitahamia kwa waziri wa nishati na team nzima ya TANESCO,kila uongo na uhuni una mwisho!!
 
Sasa hizo siku 9 ni kiboko, kuna mtu mmoja amenitonya kuwa huenda damu ikamwagika kuanzia kesho, kwani mgambo hawakubali kitendo walichotendwa. Na wanadai wanawafahamu vema machinga husika. Yetu macho na masikio.

Hii habari lmenivunja mbavu ,huyo kaanda wa polisi aliyetoa siku 9 akili zake zinamtosha peke yake .
 
Ha ha haa duh hiyo itakua ya kufungulia mwaka.chinga leo wamepewa rungu dah.natamani ningekua chinga japo leo tu
Chinga Ikwiriri wamewasha moto jana, leo Chinga Ntwara wanatembeza mkongo`oto,na Chinga wa kariakoo wanakinukisha, Chinga Mwanza wamechachamaa na Wakulima Dumila wanasema imetosha sasa. Tunakwenda wapi?
 
Kamanda, mambo ya Kitunda, Banana, Kipunguni kwa wauza mayai Mulla. Huku hata TRA, SUMATRA na EWURA ni magheshi! Tupo hapa nyuma ya kituo cha Banana Mulla, unapata kitimoto mchicha wangu! Achaa acha kabisa aisee bora wafe askari polisi 6 kuliko Mkurya mmoja raia mulla![/QU


....wasalimie LUMUMBA.....kamanda...sisi huku A town mambo powa tu...
 
Kuna habari ya askari wa mgambo kulazimisha kumpokonya askari wa ffu silaha aliyokua nayo na badala yake askari huyo kuwaita wenzake na kuja kuwashughulikia migambo hao kwa kipigo.

Hii habar ilikua ni badala ya askari wa ffu huyo kumzuia mfanyabiashara alokua amebeba mzigo wake binafsi na kuanza kumuhoji kama kawaida yao ya kusumbua wafanyabiashara hapa mjini na kila mmoja kumuona ni jambazi. Badala yake mgambo huyo alianza kumuuliza askari sababu aliyomsimamishia kijana huyo.

Hapo ndipo ilipoanza sitomfahamu na mgambo akamnyanganya silaha aliyokua nayo askari.

My take: Nchi hii kiongozi wetu ni nani? Kwanini kila mmoja anaingilia kazi za mwenzake? Je hawa askari kazi zao ni zipi hasa? Je kuna wizi wowote umeripotiwa wa kuiba mali na kila siku askari kuendelea kuwasumbua raia na vikoba ambavyo wanabeba?
 
sasa hivi ulinzi na usalama uko chini ya raia, coz askari wote wameshindwa kazi na wao wanapewa kisago kama kawa.
hii inanikumbusha wakati niko shule serikali poa unakuta viongozi wanapigwa na raia afu serikali ya wanafunzi inashinwa cha kufanya coz inawaogopa wababe.
ndo serikali ya JK imeshindwa kudhibiti mpaka raia wanajichukulia sheria mkononi, kwa sasa ni kawaida waziri na hata Rais mwenyewe kupopolewa mawe na kuzomea. haya yamemtokea JK mwenyewe na mawaziri kadhaa. hii nchi tunakoelekea kwa sasa naona giza nene badala ya nuru. Mungu atuepushe na hizi vurugu.

Legelege....
 
Back
Top Bottom