Kwa hili natoa pongezi jeshi la polisi Bunda

Kwa hili natoa pongezi jeshi la polisi Bunda

Tutu kalundji

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
532
Reaction score
1,287
Kwa mara ya kwanza natumia ukurasa huu kwa kulipongeza Jeshi la Polisi wilayani bunda kwa kuanza kufanyia kazi kero ya ongezeko la vibaka na wahalifu hasa kata ya bunda mjini,operation ambayo imefanikiwa kuwanasa baadhi ya wahalifu sugu wa kutapeli watu kwa mtindo wa kuwauzia dhahabu feki,kukaba,kucheza kamari nk

Wito wangu bado hili genge ni kubwa mno na mbaya zaidi linaungwa mkono na familia zao pamoja na wazawa hivyo nguvu ya ziada inahitajika kuondoa kabisa hii mizizi ya uhalifu ambayo imevutia vijana wengi wa eneo husika kusitisha masomo na kujiunga na magenge haya ili kupata pesa za haraka kwa njia zisizo halali!

Kwa taarifa nilizonazo mmoja wa wazazi wa mtuhumiwa kahamisha baadhi ya mali alizozipata mwanae kwa njia zisizo halali na kwenda kuzihifadhi mbali ili kupoteza ushahidi.Baadhi ya mali hizo ni pikipiki iliyonunuliwa hivi karibuni nk.

Polisi tumieni intelijensia zenu kuendelea kuwanasa hawa wahalifu sugu kwani pindi wapatapo pesa kero nyingine ni kukodi pikipiki na kuendesha kwa kasi kubwa na vurugu nyingi huku wakisababisha kero na hata ajari kwa wapita njia.

Pamoja na hayo vijana hawa ni kama wamelidharau Jeshi la Polisi maana wanapofanikiwa kupora au kutapeli Wala hawahangaiki kukimbia, badala yake hutamba hadharani mtu waliyempora(kolo).Na ikitokea muathirika wa kufanyiwa utapeli kawapata, vijana hawa huwa na umoja thabiti ambapo huungana na kumshushia kipigo kizito hadharani huyo huyo waliyemtapeli.

Mbaya zaidi taarifa za kuwakamata huwa zinawafikia mapema zaidi kupitia mgambo wenu na hivyo inakuwa rahisi kukwepa mtego wa kuwakamata. Kiukweli mgambo mnaowatumia hawana maadili kabisa ya kudhibiti uhalifu, mhalifu asiyekuwa na utaratibu wa kuwapa mgambo chochote huwa wanapambana nae kinagaubaga ila asiye na mkono wa birika wanamlinda kwa kila namna ikiwemo kumpa taarifa mapema kuhusu operation zitakakopita na zitawalenga zaidi kina nani.Kuna haja ya kuwaondoa mgambo wote mnaowatumia na kutafuta njia nyingine saidizi.

Unashangaa mgambo anapita na kukuta kundi la vijana na kuita baadhi na kuanza kuomba omba, pesa hadi AIBU!Hasa yule mfupi anayetembea na pingu masaa 24 kazidi sana kujidhalilisha!

Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli,Mimi ni balozi wa usalama!
 
Back
Top Bottom