Mimi nafikiri kabla ya kuanza kutoa lawama na shutuma kwa Rais JPM na safu yake ya uongozi juu ya uamuzi wake wa kuhamisha makao makuu ya nchi na serikali yakutoka jijini Dar hadi mkoani Dodoma ni vizur tukajiuliza haya maswali machache
1. Dhumuni hasa la muasisi wa nchi yetu Mwalimu JK Nyerere kuhamia Dodoma lilikuwa nini hasa?
2. Kwa nini mataifa makubwa duniani hayajaweka makao makuu ya nchi zao kwenye maeneo ambayo ni pembezoni mwa bahari mfano Marekani - washington DC, Uingereza - London, China - Beijing, South Afrika - Pretoria, Majirani zetu kenya nao wameweka Nairobi iliyopo katikati ya nchi na sio Mombasa iliyopo pwani mwa nchi yao?
3. Kiusalama ni vizuri makao makuu ya nchi yakae pwani au yakee katikati mwa nchi?
4. Kuleta maendeleo yenye usawa sawa katika nchi ni je vizur makao makuu ya nchi yabaki Dar au tuamie dodoma?
5. Ili kuweka karibu kuweka huduma za kiserikali karibu na wananchi ni vizur makao makuu ya nchi yaendelee kuwa dar au tuamie dodoma?
Mwenye majibu mujarabu wa haya maswali ndio anaweza kuendelea kukosoa uamuzi wa serikali kutoka Dar kwenda dodoma.
Note:
Kuna kosa ambalo alifanya mwalimu JK Nyerere la kuruhusu kutumia Dar kama makao makuu ya nchi, kwani ule uamuzi ndio ulipelekea mikoa mingine iendelee kudumaa nchini Tanzania hadi sasa, hivyo watanzania naomba tumuunge Rais JPM kwa dhumuni la kusahihisha makosa yaliyofanywa na mwalimu JK Nyerere, ambapo watangulizi wake kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete walishindwa.
Pili watanzania inabidi tuvumilie maumivu tutakayopata kwa sasa baada ya zoezi la kuhama kutoka Dar kwenda dodoma litakapoanza, kwani badae hali itatengamaa na pia nchi yetu itakuwa katika nafasi nzuri ya kukua strategical.