VACANCY NOT BUDGETED

VACANCY NOT BUDGETED

SHAZ96

Member
Joined
May 22, 2022
Posts
59
Reaction score
92
PEPMIS PEPMIS PEPMIS PEPMIS PEPMIS PEPMIS
📢 UFAFANUZI MUHIMU: “VACANCY IS NOT BUDGETED” KATIKA MFUMO WA ESS

Ndugu mtumishi,
Kumekuwa na maswali mengi kuhusu ujumbe huu unaojitokeza kwenye mfumo wa ESS wakati wa kuomba uhamisho:

❗ “Vacancy is not budgeted”

Wengi wanauliza:
“Kama tayari nalipwa mshahara, kwa nini ihitajike budget nyingine nikihama?”

Hapa chini ndio ufafanuzi kamili, rahisi na wa kueleweka 👇

🧾 MAANA HALISI YA UJUMBE HUU
👉 Ujumbe huu unamaanisha:

Nafasi unayoomba INAONEKANA kwenye mfumo ✅
Lakini HAINA BAJETI ya mshahara kwa sasa ❌

📌 Kwa kifupi:
Huwezi kuhamia hapo kwa sababu hakuna fedha iliyopangwa kukulipa kwenye hiyo halmashauri.

💰 BAJETI INAYOZUNGUMZIWA NI IPI?

Ni Bajeti ya Mishahara (PE – Personal Emoluments) ya halmashauri unayotaka kuhamia.

Kila halmashauri inapangiwa:

👥 Idadi maalum ya watumishi (Establishment)

💵 Kiwango maalum cha fedha za mishahara

🤔 SWALI KUBWA: “SI MSHARAHA UNAHAMA NA MTU?”

Jibu ni: HAPANA ❌
Hapa ndipo wengi wanapochanganyikiwa 👇

⚠️ Sababu kuu:
Bajeti haimuhusu mtu binafsi pekee

Inahusisha:
👉Nafasi ya kazi
👉Kituo cha kazi/Halmashauri
👉Kibali cha kifedha

👉 Hivyo:
Wewe unaweza kuwa na mshahara, lakini sehemu unayotaka kwenda isiwe na uwezo wa kukulipa

🔍 SABABU ZA KUONEKANA “NOT BUDGETED”
1️⃣ Bajeti haijatengewa nafasi hiyo
Nafasi ipo kwenye mfumo
Lakini haijapangiwa fedha

2️⃣ Halmashauri imefikia ukomo wa mishahara
Imefikia kiwango chake cha juu (salary ceiling)

3️⃣ Hakuna kibali cha kujaza nafasi
Serikali bado haijaruhusu kuongeza watumishi

4️⃣ Nafasi ipo “kimfumo” tu
Haijawa-activated kwenye payroll

📊 MFANO RAHISI WA KUELEWA
Halmashauri A:
Ina watumishi 100 ✅
Wewe uko hapa na unalipwa

Kisha
Halmashauri B:
Imeruhusiwa watumishi 95 ❌

Na
Tayari wana 95

👉 Ukihamia:
Unakuwa wa 96

Lakini bajeti yao inaishia 95

🚫 Ndiyo maana mfumo unasema:
“Vacancy is not budgeted”

🧠 HITIMISHO MUHIMU
✔️ Hii sio error ya mfumo
✔️ Sio kwamba mshahara wako haujulikani pia

❌ Ni kizuizi cha bajeti ya halmashauri unayotaka kuhamia

👉 Mfumo unalinda:
Nidhamu ya matumizi ya serikali na
Ulinganifu wa watumishi na bajeti

✅ UFANYE NINI SASA?
📞 Wasiliana na HR wa halmashauri unayotaka kuhamia

🧾 Uliza kama:
Nafasi itawekewa bajeti lini
Au kuna nafasi nyingine zilizo “budgeted”

🚨 UJUMBE WA MWISHO
Ndugu mtumishi,
Usichukulie ujumbe huu kama kikwazo cha mfumo

Huu ni utaratibu Mzuri tuu wa kifedha wa serikali.

📌 Sio kila nafasi iliyo wazi, ina fedha ya kulipa mtumishi.

👉 Share ujumbe huu uwasaidie watumishi wengine kuelewa hili jambo muhimu 💡



Imeandaliwa na
Mwalimu Na Mifumo
0753538043
 
Back
Top Bottom