Vumbi limetulia ukweli unatamalaki

Vumbi limetulia ukweli unatamalaki

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,466
Reaction score
860,342
NISICHUKULIWE KAMA MKOSOAJI
Magufuli aliongea vizuri sana kuwa atahakikisha serikali yake inahamia/itahamia Dodoma kabla kipindi chake cha kuwa madarakani kwisha, amebakiza miaka minne na ushee
Baada ya hotuba ile tu ukatokea mlipuko wa matamko ya kuhamia Dodoma na mishemishe zikawa nyingi
-Aliaza Chizeba
-Akafuatia Jenista Mhagama
-Mambo ya ndani na wengineo
Hawa wote wakasema ni kabla ya mwezi wa tisa

ATHARI ZA MATAMKO HAYA
maandalizi lipulipu yakaanza Dodoma
Wapangaji wa CDA wakafukuzwa
harakati za kutafuta nyumba na viwanja zikawa nyingi
Wazabuni mbalimbali wanaoidai serikali wakafurika kwenye wizara walizofanyia kazi kudai chao
Shughuli nyingi za ki serikali zikavurugika mpaka mkuu wa mkoa wa Dodoma akasitisha matamko yote ya kuhamia Dodoma kwa wiki mbili

MITANDAO YA KIJAMII YANENA
Vumbi la kuhamia Dodoma lilikuwa kila mahali..mitandaoni kukawa na mijadala ya kila aina lakini wengi wakijikita kwenye haya
.uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi
.bajeti ya kuhamia huko
.miundombinu mbinu ya Dodoma
.maisha mapya huko nk
Hapa wengi tulitukanwa kuwa tunakurupuka na kukosoa kila kitu. tukawa wavumilivu kwakuwa tuliona wazi kuwa tuko sahihi

MAHITAJI YA NYAKATI
Ishu ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na mwalimu Nyerere, aliona Dodoma kama iko katikati ya nchi hivyo kuwa rahisi kufikika kutoka pembe zote za nchi HII NDIO ILIKUWA SABABU PEKEE KUBWA ya kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, kama zipo nyingine ni ndogo ndogo
Kwa dunia ya wakati ule mahitaji ya nyakati yalikuwa sahihi kabisa lakini si sasa na hata baadae , ulimwengu umekuwa kijiji, mambo yamerahisishwa mno maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanaifanya hoja ya kuhamia Dodoma kutokuwa VALID kwasasa, siku hizi hatuhitaji posta wala kusafiri masaa mengi kufuata huduma, siku hizi maendeleo yamesogezwa mikoani wilayani na hata sehemu ambazo mwanzoni hazikufikiriwa kabisa....Nyerere angekuwa hai bado angebatilisha huu uamuzi kwa hakika

BAJETI YA KUHAMIA DODOMA
Wakati wa Mkapa ulifanyika upembuzi yakinifu wa bajeti ya kuhamia Dodoma....ilikadiriwa kuwa zilihitajika kiasi cha shilingi za kitanzania TRILIOM MOJA NA BILIONI MIA MBILI...Ni pesa nyingi kwa nchi maskini kama yetu...Mkapa akashindwa
Leo hii tukitaka kwa hakika kuhamia Dodoma sijui bajeti yake itakuwa shilingi ngapi na hiyo pesa itapatikanaje
Lakini je kuhamia Dodoma kwasasa ndio kipaumbele? Faida zake ni zipi kiuchumi? Sio kwamba tunataka tu kuwatajirisha watu wachache?wengi wakiwa ni raia wa nje...kwakuwa miundombinu mingi watapewa wao kujenga
Je tumeshajitosheleza kwenye huduma zetu muhimu za kijamii? Elimu afya miundombinu nk?
Bandari zetu bado zinahitajika ukarabati mkubwa reli zetu pia nk ...tuwwkeze huku kwanza kunakotuingizia chochote

HITIMISHO
Mkuu wa nchi alisema atahakikisha serikali yake inahamia kabla muhula wake haujaisha na akasema AKIHAMA yeye wengine watafuata
Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu nimekuelewa mzee.
Tatizo la serikali hii wao kazi yao ni kukurupuka na kutoa matamko tu.
Hawajui wala kutaka kupembua mambo kwa kutumia akili.

Akili ya Magufuli ni sawa na mtoto kaona nzi kwenye bakuli la uji. Badala ya kuchukua kijiko na kutoa yule nzi,atampiga nzi kibao na kumwaga uji wote,mwisho wake kumuunguza.

Yetu sisi macho. Anajifanya kucheza ba maisha ya watu na amani. Ubabe yeye,matamko yasio na tija ni yeye. Huyu mtu ana aakili timamu kweli?
 
Usihofu, yale ni matamko ya mwendokasi tu. Binafsi sioni faida kwa muda huu, labda kipindi cha Nyerere ndio palikuwa na tija. Kuhama ni gharama na si kipaumbele kwa sasa.
Habari za magazetini leo imethibitika kuwa kuhamia Dodoma si kitu lelemama Si Jenista wala Chizeba wenye dalili ya kusogeza hata kiti
TAMISEMI iko Dodoma tayari lakini pia imekuwa vigumu kuhama sembuse wizara ambazo zina ofisi ndogo tuu
Yangefanyika maandalizi kwasasa Dar ipanuliwe kuelekea Morogoro kuelekea kusini nk
Jiji kwasasa limesongwa linatawikiwa kupanuliwa ili lipumue, tayari kuna miundombinu mingi yenye sura ya makao makuu ya nchi ni swala la kuboreshwa tu kwasasa kuliko kung'ang'ania ndoto isiyotekelezeka na yenye gharama kubwa huku kukiwa hakuna faida za moja kwa moja
Mkuu nimekuelewa mzee.
Tatizo la serikali hii wao kazi yao ni kukurupuka na kutoa matamko tu.
Hawajui wala kutaka kupembua mambo kwa kutumia akili.

Akili ya Magufuli ni sawa na mtoto kaona nzi kwenye bakuli la uji. Badala ya kuchukua kijiko na kutoa yule nzi,atampiga nzi kibao na kumwaga uji wote,mwisho wake kumuunguza.

Yetu sisi macho. Anajifanya kucheza ba maisha ya watu na amani. Ubabe yeye,matamko yasio na tija ni yeye. Huyu mtu ana aakili timamu kweli?
 
Suala la kuhamia Dodoma lilikuwa la kijamaa zaidi. Sasa halina umaana sana kwan usafiri na mawasiliano ambavyo ndio ilikuwa sababu kubwa zaidi ya kwenda Dom sasa vimeboreshwa sana
 
Uwekezaji wa namna hii na miradi mingine ndani ya jiji la Dsm ambayo mingine iko mbio ni kukamilika itakuwa ni hasara kubwa kwa nchi na NHC
1470380356403.jpg
1470380365346.jpg

Unaweza kuta Raisi alisema akihama yeye wengine watafuata lakini wakati huo huo akampa maelekezo Majaliwa aanze kazi mara moja ya kuhamia Dodoma ,
 
Kuhamia Dodoma ni muhimu sana kwa namna ambayo JPM aliweka. I personally agree and wish that to strategically become a success come 2018.
 
Ila kweli mkuu alisema atatangulia then wengine watamfuata sasa nashangaa wao ndio wanatangulia...!
 
NISICHUKULIWE KAMA MKOSOAJI
Magufuli aliongea vizuri sana kuwa atahakikisha serikali yake inahamia/itahamia Dodoma kabla kipindi chake cha kuwa madarakani kwisha, amebakiza miaka minne na ushee
Baada ya hotuba ile tu ukatokea mlipuko wa matamko ya kuhamia Dodoma na mishemishe zikawa nyingi
-Aliaza Chizeba
-Akafuatia Jenista Mhagama
-Mambo ya ndani na wengineo
Hawa wote wakasema ni kabla ya mwezi wa tisa

ATHARI ZA MATAMKO HAYA
maandalizi lipulipu yakaanza Dodoma
Wapangaji wa CDA wakafukuzwa
harakati za kutafuta nyumba na viwanja zikawa nyingi
Wazabuni mbalimbali wanaoidai serikali wakafurika kwenye wizara walizofanyia kazi kudai chao
Shughuli nyingi za ki serikali zikavurugika mpaka mkuu wa mkoa wa Dodoma akasitisha matamko yote ya kuhamia Dodoma kwa wiki mbili

MITANDAO YA KIJAMII YANENA
Vumbi la kuhamia Dodoma lilikuwa kila mahali..mitandaoni kukawa na mijadala ya kila aina lakini wengi wakijikita kwenye haya
.uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi
.bajeti ya kuhamia huko
.miundombinu mbinu ya Dodoma
.maisha mapya huko nk
Hapa wengi tulitukanwa kuwa tunakurupuka na kukosoa kila kitu. tukawa wavumilivu kwakuwa tuliona wazi kuwa tuko sahihi

MAHITAJI YA NYAKATI
Ishu ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na mwalimu Nyerere, aliona Dodoma kama iko katikati ya nchi hivyo kuwa rahisi kufikika kutoka pembe zote za nchi HII NDIO ILIKUWA SABABU PEKEE KUBWA ya kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, kama zipo nyingine ni ndogo ndogo
Kwa dunia ya wakati ule mahitaji ya nyakati yalikuwa sahihi kabisa lakini si sasa na hata baadae , ulimwengu umekuwa kijiji, mambo yamerahisishwa mno maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanaifanya hoja ya kuhamia Dodoma kutokuwa VALID kwasasa, siku hizi hatuhitaji posta wala kusafiri masaa mengi kufuata huduma, siku hizi maendeleo yamesogezwa mikoani wilayani na hata sehemu ambazo mwanzoni hazikufikiriwa kabisa....Nyerere angekuwa hai bado angebatilisha huu uamuzi kwa hakika

BAJETI YA KUHAMIA DODOMA
Wakati wa Mkapa ulifanyika upembuzi yakinifu wa bajeti ya kuhamia Dodoma....ilikadiriwa kuwa zilihitajika kiasi cha shilingi za kitanzania TRILIOM MOJA NA BILIONI MIA MBILI...Ni pesa nyingi kwa nchi maskini kama yetu...Mkapa akashindwa
Leo hii tukitaka kwa hakika kuhamia Dodoma sijui bajeti yake itakuwa shilingi ngapi na hiyo pesa itapatikanaje
Lakini je kuhamia Dodoma kwasasa ndio kipaumbele? Faida zake ni zipi kiuchumi? Sio kwamba tunataka tu kuwatajirisha watu wachache?wengi wakiwa ni raia wa nje...kwakuwa miundombinu mingi watapewa wao kujenga
Je tumeshajitosheleza kwenye huduma zetu muhimu za kijamii? Elimu afya miundombinu nk?
Bandari zetu bado zinahitajika ukarabati mkubwa reli zetu pia nk ...tuwwkeze huku kwanza kunakotuingizia chochote

HITIMISHO
Mkuu wa nchi alisema atahakikisha serikali yake inahamia kabla muhula wake haujaisha na akasema AKIHAMA yeye wengine watafuata
Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Mungu ibariki Tanzania
mshana jr , mkuu kama haya yote yametoka kichwani mwako basi wewe ni bora mara 100 ya yule nanilinhii mkurupukaji....
Subir uone povu la mafisiem sasa......
 
Kuhamia Dodoma ni muhimu sana kwa namna ambayo JPM aliweka. I personally agree and wish that to strategically become a success come 2018.
Rudia kusoma kwa makini nilichoandika tafadhali
 
Mkuu tatizo la serikali yetu ni kuongozwa na viongozi waliogubikwa na nidhamu ya woga.Binafsi sikuona mantiki ya kila waziri kujinasibu kwenye vyombo vya habari huku wakitoa matamko yenye kila rangi juu ya adhima ya kuhamia Dodoma.Rais kutamka kuwa atahakikisha ametimiza ahadi iliyoahidiwa kwa muda mrefu kuhamia dodoma ndani ya miaka hii iliyosalia alijua kuwa bado anahitaji kudunduliza vijisenti katika bajeti zilizobaki kabla ya kuhitimisha muhula wake wa uongozi.
Tatizo ni kutoelewa kusudio la mkuu wa nchi kuwa hakusema waanze kuhama wala kufurahisha hadhira kupitia matamko yao.Kusema akihama tu waandamizi wake inabidi wafanye hima.Mkuu sasa wameumbuka maana kuna waliosema mwisho wa wiki hizi zilizopita eti watakuwa wametimiza agizo la mkuu kumbe hawakudhani kuwa isingewezekana kwani si kuhama wao tu bali waandamizi wote.Daima kesheni mkiomba utajiri wa FIKRA na uwezo wa kutafakari kabla ya kutenda.Samahani wakuu nimewaza kwa sauti.
 
NISICHUKULIWE KAMA MKOSOAJI
Magufuli aliongea vizuri sana kuwa atahakikisha serikali yake inahamia/itahamia Dodoma kabla kipindi chake cha kuwa madarakani kwisha, amebakiza miaka minne na ushee
Baada ya hotuba ile tu ukatokea mlipuko wa matamko ya kuhamia Dodoma na mishemishe zikawa nyingi
-Aliaza Chizeba
-Akafuatia Jenista Mhagama
-Mambo ya ndani na wengineo
Hawa wote wakasema ni kabla ya mwezi wa tisa

ATHARI ZA MATAMKO HAYA
maandalizi lipulipu yakaanza Dodoma
Wapangaji wa CDA wakafukuzwa
harakati za kutafuta nyumba na viwanja zikawa nyingi
Wazabuni mbalimbali wanaoidai serikali wakafurika kwenye wizara walizofanyia kazi kudai chao
Shughuli nyingi za ki serikali zikavurugika mpaka mkuu wa mkoa wa Dodoma akasitisha matamko yote ya kuhamia Dodoma kwa wiki mbili

MITANDAO YA KIJAMII YANENA
Vumbi la kuhamia Dodoma lilikuwa kila mahali..mitandaoni kukawa na mijadala ya kila aina lakini wengi wakijikita kwenye haya
.uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi
.bajeti ya kuhamia huko
.miundombinu mbinu ya Dodoma
.maisha mapya huko nk
Hapa wengi tulitukanwa kuwa tunakurupuka na kukosoa kila kitu. tukawa wavumilivu kwakuwa tuliona wazi kuwa tuko sahihi

MAHITAJI YA NYAKATI
Ishu ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na mwalimu Nyerere, aliona Dodoma kama iko katikati ya nchi hivyo kuwa rahisi kufikika kutoka pembe zote za nchi HII NDIO ILIKUWA SABABU PEKEE KUBWA ya kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, kama zipo nyingine ni ndogo ndogo
Kwa dunia ya wakati ule mahitaji ya nyakati yalikuwa sahihi kabisa lakini si sasa na hata baadae , ulimwengu umekuwa kijiji, mambo yamerahisishwa mno maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanaifanya hoja ya kuhamia Dodoma kutokuwa VALID kwasasa, siku hizi hatuhitaji posta wala kusafiri masaa mengi kufuata huduma, siku hizi maendeleo yamesogezwa mikoani wilayani na hata sehemu ambazo mwanzoni hazikufikiriwa kabisa....Nyerere angekuwa hai bado angebatilisha huu uamuzi kwa hakika

BAJETI YA KUHAMIA DODOMA
Wakati wa Mkapa ulifanyika upembuzi yakinifu wa bajeti ya kuhamia Dodoma....ilikadiriwa kuwa zilihitajika kiasi cha shilingi za kitanzania TRILIOM MOJA NA BILIONI MIA MBILI...Ni pesa nyingi kwa nchi maskini kama yetu...Mkapa akashindwa
Leo hii tukitaka kwa hakika kuhamia Dodoma sijui bajeti yake itakuwa shilingi ngapi na hiyo pesa itapatikanaje
Lakini je kuhamia Dodoma kwasasa ndio kipaumbele? Faida zake ni zipi kiuchumi? Sio kwamba tunataka tu kuwatajirisha watu wachache?wengi wakiwa ni raia wa nje...kwakuwa miundombinu mingi watapewa wao kujenga
Je tumeshajitosheleza kwenye huduma zetu muhimu za kijamii? Elimu afya miundombinu nk?
Bandari zetu bado zinahitajika ukarabati mkubwa reli zetu pia nk ...tuwwkeze huku kwanza kunakotuingizia chochote

HITIMISHO
Mkuu wa nchi alisema atahakikisha serikali yake inahamia kabla muhula wake haujaisha na akasema AKIHAMA yeye wengine watafuata
Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Mungu ibariki Tanzania

Ajabu ni kwamba wewe ambaye haumo hata kwenye serikali umemuelewa Mkuu kuliko hata hao waliopo serikalini,maana ulivyoelewa wewe ndivyo nilivyoelewa mimi,huwa najiuliza siku zote hivi hawa watu utendaji wao wa kazi huwa unaongozwa na nini hasa?unafiki wao? uoga wao?au sera na utaratibu maana sikuona hata sababu ya wao kukurupuka kule ikiwa umemuelewa mkuu wako wa kazi kasema nini,suala ni kuelewa umeambiwa nini na kisha nini kifuate basi,lakini hawa wenzetu unafiki ni mwingi kuliko uhalisia.
 
Back
Top Bottom