Vumbi limetulia ukweli unatamalaki

Vumbi limetulia ukweli unatamalaki

Tatizo letu watz ni wasemaji sana na sio watendaji kabisa tunaongea utelekezaji unakuwa mdogo

halafu suala hili liko nje ya uwezo wetu wewe alishindwa mkapa itaweezekana leo hiii
kama tungekuwa tunapenda kujipima na kukubali makosa tuliyokwisha kuyafanya hapo awali,hii miaka hamsini ilitakiwa tuanze ujenzi wa Tanzania mpya sio makundi mapya ya ccm yakushambulia kambi fulani
 
Kwanza hukuelewa muktadha mzima wa hii mada
Halafu kwa uchache nikuambie tu kwamba kwa kuitolea Nairobi kuwa katikati ya nchi kumeisaidia sana kiulinzi ni uongo na makosa makubwa kabisa
Nairobi ni mhanga mkubwa wa mashambulizi ya kigaidi zaidi ya mara kumi
Marekani tumeshuhudia Twin towers ikisawazishwa nk nk
Ingekuwa ni ishu ya kiusalama tungeshapigwa siku nyingi sana. ..vita ya kagera angalia ilitokea wapi. ..tuwaze kwa tafakuri tusiongozwe na mahaba niuwe
La msingi kuliko lote je ndo kipaumbele cha nchi yetu?Sikuwahi kiisikia kipindi cha kuomba kura mbona?
 
Kwanza hukuelewa muktadha mzima wa hii mada
Halafu kwa uchache nikuambie tu kwamba kwa kuitolea Nairobi kuwa katikati ya nchi kumeisaidia sana kiulinzi ni uongo na makosa makubwa kabisa
Nairobi ni mhanga mkubwa wa mashambulizi ya kigaidi zaidi ya mara kumi
Marekani tumeshuhudia Twin towers ikisawazishwa nk nk
Ingekuwa ni ishu ya kiusalama tungeshapigwa siku nyingi sana. ..vita ya kagera angalia ilitokea wapi. ..tuwaze kwa tafakuri tusiongozwe na mahaba niuwe
Acha mipasho ndugu Mshana, kuna maswali mengi ya msingi nimeyauliza hapo nenda kwenye hoja tafadhali.
Muktadha wa hii mda nzima nimeuelewa kuliko wewe ulieuanzisha.
Labda nikufundishe kidogo nchi kuwa pwani inakuwa na hatari kubwa ya kushambuliwa zaidi hasa mashambulizi ya kushtukiza kuliko inavyokuwa katikati,
Umetolea mfano wa kenya na nafikiri unaongelea ugaidi, ugaidi wa kenya unahusisha mambo mengi ikiwemo wakenya wasio waaminifu.
Mfano mwingine ni mashambulizi ya westgate mall yalichukua mda mrefu kuandaa ila kama ile westgate mall ingekuwa pwani kama mombasa isingewachukua mda mrefu wale magaidi kujiandaa na kushambulia,
Pia sasa tecknolojia imekuwa sana hivyo tunaona nchi kama marekani zikitumia bahari kufanya mashambulizi kwa maadui zake kwa kutumia manowari.
Dar kuwa makao makuu ni kosa alilofanya Mwalimu JK Nyerere, hivyo alishindwa kuhamisha tangu tupate uhuru mwaka 1961 , hivyo watanzania tunatakuwa tumuunge mkono Rais JPM anapochukua hatua ngumu kama hii kwani kuna watangulizi wake kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete walishindwa miaka yote lakini Rais JPM anajaribu kwa kipindi cha miezi 8 tu ya utawala wake.
 
Ukijaribu kufikiria toka huu uongozi umeanza rais ameingia katika mfumo wa kutumbua majipu fukuza fukuza nyingi ni kweli imesaidia kiasi kuna watu walilala sana hawakujua kazi zao Lakini hili limepelekea kufanya kazi HOFU NA UOGA MWINGI KILA MTU ANAOGOPA
Tamko lake si la kwanza yametamkwa sana lakini si suala la kukurupuka hivi hivi tathmini mawazo chanya yanahitajika Rais nae ni binadamu tutambue hili WAACHE NIDHAMU YA UOAGA kuna viongozi wakiongea na JPM WANAWEZA JAMBAJAMBA YOTE UOGA KISA KAWAULIZA KITU
TUMESHUHUDIA HAYA pale JK NYERERE INTER.................
 
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Tatizo mijitu inapenda sifa na kujipendekeza kwa mkuu wao
 
Mimi nafikiri kabla ya kuanza kutoa lawama na shutuma kwa Rais JPM na safu yake ya uongozi juu ya uamuzi wake wa kuhamisha makao makuu ya nchi na serikali yakutoka jijini Dar hadi mkoani Dodoma ni vizur tukajiuliza haya maswali machache
1. Dhumuni hasa la muasisi wa nchi yetu Mwalimu JK Nyerere kuhamia Dodoma lilikuwa nini hasa?
2. Kwa nini mataifa makubwa duniani hayajaweka makao makuu ya nchi zao kwenye maeneo ambayo ni pembezoni mwa bahari mfano Marekani - washington DC, Uingereza - London, China - Beijing, South Afrika - Pretoria, Majirani zetu kenya nao wameweka Nairobi iliyopo katikati ya nchi na sio Mombasa iliyopo pwani mwa nchi yao?
3. Kiusalama ni vizuri makao makuu ya nchi yakae pwani au yakee katikati mwa nchi?
4. Kuleta maendeleo yenye usawa sawa katika nchi ni je vizur makao makuu ya nchi yabaki Dar au tuamie dodoma?
5. Ili kuweka karibu kuweka huduma za kiserikali karibu na wananchi ni vizur makao makuu ya nchi yaendelee kuwa dar au tuamie dodoma?

Mwenye majibu mujarabu wa haya maswali ndio anaweza kuendelea kukosoa uamuzi wa serikali kutoka Dar kwenda dodoma.
Note:
Kuna kosa ambalo alifanya mwalimu JK Nyerere la kuruhusu kutumia Dar kama makao makuu ya nchi, kwani ule uamuzi ndio ulipelekea mikoa mingine iendelee kudumaa nchini Tanzania hadi sasa, hivyo watanzania naomba tumuunge Rais JPM kwa dhumuni la kusahihisha makosa yaliyofanywa na mwalimu JK Nyerere, ambapo watangulizi wake kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete walishindwa.
Pili watanzania inabidi tuvumilie maumivu tutakayopata kwa sasa baada ya zoezi la kuhama kutoka Dar kwenda dodoma litakapoanza, kwani badae hali itatengamaa na pia nchi yetu itakuwa katika nafasi nzuri ya kukua strategical.
(a)Hoja ya usalama kwa kipindi hiki cha Teknolojia ya hali ya juu ni mfu.

(b) Hoja kupeleka maendeleo maeneo mengine basi wagawanye kila Mkoa kuwe na Makao Makuu ya Wizara na taasisi zake.
 
(a)Hoja ya usalama kwa kipindi hiki cha Teknolojia ya hali ya juu ni mfu.

(b) Hoja kupeleka maendeleo maeneo mengine basi wagawanye kila Mkoa kuwe na Makao Makuu ya Wizara na taasisi zake.
Kwa hiyo hoja yako ninini mdau?
 
mawaziri wa jpm ni kama wacheza show kazi yao kucheza anachoimba bosi wao ,hawajipi muda wa kutafakari wala kumuuliza , mkuu wakati anahutubia hata alikuwa hajamaliza sentesi ya kuhamia dodoma jenista mbio na godoro lake

😀😀😀
 
Natamani hizo fedha za kuhamia mbio mbio dodoma zingetumika kuboresha hospitali za wilaya mikoa na zahanati kwa kuhakikisha kuna vifaa tiba na madawa ya kutosha.

Kulipa deni la msd...

Kuboresha shule si tu kwa madawati bali maabara na library

Kuboresha miundombinu haswa ya maji..... mijini na vijijini kutakowezekana
 
Wanaume wa dar wana manyanyaso na masimango sana. Bora ukutane na mwanamke huwa hawana dharau sana ukilinganisha na mwanaume anayeishi dar hata kama amehamia.
Kuleta shughuli kubwa za kiserikali Dodoma means kusogeza serikal karibu na wananchi physically which is more tangible kuliko kukaa dar.
Halafu ni Dar peke yenu ukifuatilia ndio mnalalamikia hili, Ukiangalia wote toka kanda ya Magharibi, Ziwa, Juu Kusini Kati wanasapoti hii kitu.
Wengi wape.
Mlijikweza mno na nyie.
Na nnaamini JPM atakuwa ni mmoja wa walionyanyasika kwa kutozaliwa Dar.
Viva Magufuri.
Viva Dodoma
I see......[emoji36] [emoji36]
 
Mkuu nimekuelewa mzee.
Tatizo la serikali hii wao kazi yao ni kukurupuka na kutoa matamko tu.
Hawajui wala kutaka kupembua mambo kwa kutumia akili.

Akili ya Magufuli ni sawa na mtoto kaona nzi kwenye bakuli la uji. Badala ya kuchukua kijiko na kutoa yule nzi,atampiga nzi kibao na kumwaga uji wote,mwisho wake kumuunguza.

Yetu sisi macho. Anajifanya kucheza ba maisha ya watu na amani. Ubabe yeye,matamko yasio na tija ni yeye. Huyu mtu ana aakili timamu kweli?
Wata kuTunduLisu.
 
NISICHUKULIWE KAMA MKOSOAJI
Magufuli aliongea vizuri sana kuwa atahakikisha serikali yake inahamia/itahamia Dodoma kabla kipindi chake cha kuwa madarakani kwisha, amebakiza miaka minne na ushee
Baada ya hotuba ile tu ukatokea mlipuko wa matamko ya kuhamia Dodoma na mishemishe zikawa nyingi
-Aliaza Chizeba
-Akafuatia Jenista Mhagama
-Mambo ya ndani na wengineo
Hawa wote wakasema ni kabla ya mwezi wa tisa

ATHARI ZA MATAMKO HAYA
maandalizi lipulipu yakaanza Dodoma
Wapangaji wa CDA wakafukuzwa
harakati za kutafuta nyumba na viwanja zikawa nyingi
Wazabuni mbalimbali wanaoidai serikali wakafurika kwenye wizara walizofanyia kazi kudai chao
Shughuli nyingi za ki serikali zikavurugika mpaka mkuu wa mkoa wa Dodoma akasitisha matamko yote ya kuhamia Dodoma kwa wiki mbili

MITANDAO YA KIJAMII YANENA
Vumbi la kuhamia Dodoma lilikuwa kila mahali..mitandaoni kukawa na mijadala ya kila aina lakini wengi wakijikita kwenye haya
.uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi
.bajeti ya kuhamia huko
.miundombinu mbinu ya Dodoma
.maisha mapya huko nk
Hapa wengi tulitukanwa kuwa tunakurupuka na kukosoa kila kitu. tukawa wavumilivu kwakuwa tuliona wazi kuwa tuko sahihi

MAHITAJI YA NYAKATI
Ishu ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na mwalimu Nyerere, aliona Dodoma kama iko katikati ya nchi hivyo kuwa rahisi kufikika kutoka pembe zote za nchi HII NDIO ILIKUWA SABABU PEKEE KUBWA ya kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, kama zipo nyingine ni ndogo ndogo
Kwa dunia ya wakati ule mahitaji ya nyakati yalikuwa sahihi kabisa lakini si sasa na hata baadae , ulimwengu umekuwa kijiji, mambo yamerahisishwa mno maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanaifanya hoja ya kuhamia Dodoma kutokuwa VALID kwasasa, siku hizi hatuhitaji posta wala kusafiri masaa mengi kufuata huduma, siku hizi maendeleo yamesogezwa mikoani wilayani na hata sehemu ambazo mwanzoni hazikufikiriwa kabisa....Nyerere angekuwa hai bado angebatilisha huu uamuzi kwa hakika

BAJETI YA KUHAMIA DODOMA
Wakati wa Mkapa ulifanyika upembuzi yakinifu wa bajeti ya kuhamia Dodoma....ilikadiriwa kuwa zilihitajika kiasi cha shilingi za kitanzania TRILIOM MOJA NA BILIONI MIA MBILI...Ni pesa nyingi kwa nchi maskini kama yetu...Mkapa akashindwa
Leo hii tukitaka kwa hakika kuhamia Dodoma sijui bajeti yake itakuwa shilingi ngapi na hiyo pesa itapatikanaje
Lakini je kuhamia Dodoma kwasasa ndio kipaumbele? Faida zake ni zipi kiuchumi? Sio kwamba tunataka tu kuwatajirisha watu wachache?wengi wakiwa ni raia wa nje...kwakuwa miundombinu mingi watapewa wao kujenga
Je tumeshajitosheleza kwenye huduma zetu muhimu za kijamii? Elimu afya miundombinu nk?
Bandari zetu bado zinahitajika ukarabati mkubwa reli zetu pia nk ...tuwwkeze huku kwanza kunakotuingizia chochote

HITIMISHO
Mkuu wa nchi alisema atahakikisha serikali yake inahamia kabla muhula wake haujaisha na akasema AKIHAMA yeye wengine watafuata
Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Mungu ibariki Tanzania
Facts
 
Mkuu Mshana nimekubaliana na wewe kwa kiasi lakini kiasi pia natofautiana na wewe.
1. Kiusalama ikitokea vita (Mungu aepushie mbali) kutekwa kwa mji mkuu ni ishara kuwa nchi/Serikali imeangushwa. Dodoma bado inakuwa sehemu nzuri ikitokea cha kutokea. UUwepo wa Dar kama mji mkuu yenye serikali kandokando ya bahari (maji) ni tatizo.
2. Hoja ya kupanua Dar es Salaam ili mji upumuo haina mashiko. Kinachokosekana mji huu ni mipangomiji, serikali kutokuwekeza kwenye makazi na hulka ya kila mtu kuwa na kiwanja chake. Unapopanua mji zaidi unaongeza gharama za uwekezaji kwenye miundombinu. In fact huu mji haukupaswa kuzidi 20 Km radius kutoka mjini kati ili maeneo mengine watu waendelee kulima na kupanda miti.
Kwangu, suala la kuhamisha serikali Dodoma ni nzuri nina tatizo na huu uharaka basi.
Rudi shule ukasome,Mkuu Mshana ameeleza vizuri sana bila chenga,na kila kitu ameweka wazi kabisa,sasa wewe unakuja na upupu wako kuhusu vita kutokea na mji mkuu kutekwa?,au uko kilabuni unakunywa kangara,kaa kimya kuliko kutujazia kurasa.
 
Rudi shule ukasome,Mkuu Mshana ameeleza vizuri sana bila chenga,na kila kitu ameweka wazi kabisa,sasa wewe unakuja na upupu wako kuhusu vita kutokea na mji mkuu kutekwa?,au uko kilabuni unakunywa kangara,kaa kimya kuliko kutujazia kurasa.
Wote hatuwezi kuwa na mawazo sawa. Naheshimu mawazo yako mkuu. By the way karibu tupate kangara.
 
Kwanza hukuelewa muktadha mzima wa hii mada
Halafu kwa uchache nikuambie tu kwamba kwa kuitolea Nairobi kuwa katikati ya nchi kumeisaidia sana kiulinzi ni uongo na makosa makubwa kabisa
Nairobi ni mhanga mkubwa wa mashambulizi ya kigaidi zaidi ya mara kumi
Marekani tumeshuhudia Twin towers ikisawazishwa nk nk
Ingekuwa ni ishu ya kiusalama tungeshapigwa siku nyingi sana. ..vita ya kagera angalia ilitokea wapi. ..tuwaze kwa tafakuri tusiongozwe na mahaba niuwe
Mkuu umemaliza kila kitu bila kuacha kitu,usipoteze muda wako kujibu watu ambao wala hawajui dunia iko wapi na inaenda wapi?
 
Mkuu umemaliza kila kitu bila kuacha kitu,usipoteze muda wako kujibu watu ambao wala hawajui dunia iko wapi na inaenda wapi?
Ushabiki utakumaliza kijana, penda kufikiria kwa kutumia ubongo na sio moyo kama unavyofanya.
 
Mkuu tatizo la serikali yetu ni kuongozwa na viongozi waliogubikwa na nidhamu ya woga.Binafsi sikuona mantiki ya kila waziri kujinasibu kwenye vyombo vya habari huku wakitoa matamko yenye kila rangi juu ya adhima ya kuhamia Dodoma.Rais kutamka kuwa atahakikisha ametimiza ahadi iliyoahidiwa kwa muda mrefu kuhamia dodoma ndani ya miaka hii iliyosalia alijua kuwa bado anahitaji kudunduliza vijisenti katika bajeti zilizobaki kabla ya kuhitimisha muhula wake wa uongozi.
Tatizo ni kutoelewa kusudio la mkuu wa nchi kuwa hakusema waanze kuhama wala kufurahisha hadhira kupitia matamko yao.Kusema akihama tu waandamizi wake inabidi wafanye hima.Mkuu sasa wameumbuka maana kuna waliosema mwisho wa wiki hizi zilizopita eti watakuwa wametimiza agizo la mkuu kumbe hawakudhani kuwa isingewezekana kwani si kuhama wao tu bali waandamizi wote.Daima kesheni mkiomba utajiri wa FIKRA na uwezo wa kutafakari kabla ya kutenda.Samahani wakuu nimewaza kwa sauti.
Mkuu, siku hizi hata ukimsaidia mtu shilingi elfu saba za bandej, lazima uonekane ITV...usipoonekana wiki nzima unaweza ukatenguliwa.
 
Back
Top Bottom