Vua Gamba Vaa Gwanda Yapata Dhoruba Lindi

Vua Gamba Vaa Gwanda Yapata Dhoruba Lindi

Wananchi wa Lindi wanahitaji ukombozi wa fikra kwanza kabla ya mambo mengine. CDM wanayo kazi kuwaelimisha, ukizingatia mtaji wa ccm ni wajinga.
Watu wa Lindi si wajinga ni wapole na waungwana si kama watu wa Kilimanjaro na Arusha,mimi nimefanya kazi Railways Moshi na Arusha nawafahamu sana nyie ndugu zetu na hulka zenu za ubinafsi,uwiano wa shule za msingi na upili katika maeneo mengi Tanzania unatofautiana na hilo si jambo la kuwalaumu wakazi wa sehemu husika pia suala la utajiri wa watu nalo pia linategemea kwa mfano maeneo mengi ya Kusini kuna Gesi Asili,mafuta,chuma,maka ya mawe,uranium vitu ambavyo si rahisi kwa wachimbaji wadogo kuchimba kama vile Tanzanite tunakiri wazi kuwa maeneo ya kusini yaliachwa nyuma kimaendeleo lakini Serikali ilifanya makusudi,siku za karibuni nimetembelea maeneo mengi ya wilaya ya Monduli,Ngorongoro bado pia umasikini wa kutupwa upo tena sana tu ila ukifananisha Makao makuu ya Mkoa wa Arusha na Makao Makuu ya Mkoa wa Lindi Mkoa wa Lindi uko nyuma kiasi si sawa na Arusha ila umasikini kote upo!
 
Wananchi wa Lindi wanahitaji ukombozi wa fikra kwanza kabla ya mambo mengine. CDM wanayo kazi kuwaelimisha, ukizingatia mtaji wa ccm ni wajinga.

Nimeishi kusini miaka 10 na lindi mjini ndiyo nimeishi zaidi nikiwa nafanya kazi katika mashirika ya kimataifa vijijini. Nilishuhudia umaskini wa kutisha na mawazo mgando yaliyolalamika daima "sisi watu wa kusini tumeachwa, kuanzia kung'oa reli" hadi ukosefu wa barabara. Nimeshuhudia wanafunzi wa shule wasiovaa viatu na wasichana wamejifunga vipande vya kaniki wakiimba tuna imani na Mwinyi, Nyerere, CCM huku viganja vikilenga mapaji ya uso salamu ya chipukizi wa TANU youth league!!

Nimeshuhudia watu wakila mbegu za miti zenye sumu sana wengine wakifa!! na hata majani!!
Ndugu yangu kusini ni mtaji mkuu wa CCMAGAMBA yaani UMASKINI. Sasa kudanganywa kunatokana na ahueni ndogo!! ambayo wameipata au ni ujumbe kutoka kwa SALMA JK (First lady) mwenye uenyeji wa hapo MIKUMBI?
Simba wa Nachunyu vipi?? wamethibitiwa?
Ming'oko vipi bado inaliwa? Huo utajiri mlioletewa na CCM ni upi?

Yaani ninachochukia wanaojifanya wana-CHADEMA ni dharau dhidi ya maeneo ya wenzao. Hivi mtu mwenye akili yake timamu atasema Mmasai anaeishi kwa kuhamahama anavaa viatu?! Hivi wale wafugaji ambao hawana hata makazi ambao wamejaa mikoa ya Kaskazini wameenda shule wale?! Hivi wanavaa viatu wale?! Watu leo wako huku, kesho wako kule wana chakula cha kutosha wale?! Hata Kiswahili hawajui mtasema wameendelea wale?! Hivi utajiri wa Arusha mtasema ni utajiri wa wenyeji wa maelefu ya waarusha ule?! Mpuuzi mwingine anasema eti njaa wanakula ming'oko, sasa kwa taarifa yako hicho ni chakula cha asili ambacho watu wa kule wanakipenda kiasi kwamba hata kama mtu ana gunia elfu moja ndani, bado atakula tu!! Mama angu mzazi ambae karibu maisha yake yote yupo hapa dar lakini bado anapenda ming'oko na akiona mtu anaenda kwao lazima aagizie tu. Acheni dharau kwa wenzenu, Tanzania hii ni mpumbavu tu ndie atakayejifanya kwao maisha ni mazuri wakati mikoa mingi ni hoe hae hasa huko vijijini. Na vijiji vingi vya kaskazini na kanda ya kati wala hamna cha kuwacheka watu wa kusini kwani maeneo mengi watu still wanaishi kwenye primitive age. Acheni dharau zenu.....!!
 
unajua CCM wameajiri wakina nape wengi sana humu jamvini so members kuweni makini,ili msipate shida.
 
ndug lind ndio mkoa ulio saharuka na kutelekezwa kuliko mkoa wowote hapa tanzani. ndio maana una onekana mzushi kuongelea ccm lind! maisha ya lindi ni magumu sana,pamoja na kuwepo na barabara. ukumbuke humu sio fb, hil ni jukwaa la wafatiliaji habari kwa karibu. ni mekaa lind zaidi ya miaka 2 na sijui barabara una yosema ni ile ya mkampa! shule kubwa lind ni moja tu na ni lindi sec ambayo iko road kabla ya kufika stend. watch your words
 
Jaman kaelewa, mumsamehe! jasho linamtoka huko aliko. Anajuta kujijamii!
 
Nape kajiunga mara kumi pamoja na watu wake wanatumia username tofauti tofauti
 
Haahaa haha,ndugu yangu endelea kusubiri kushindwa kwa CDM,utashindwa ww na dhoruba zako,usiwatukane wamachinga,hayo mashule yasiyo na walimu wala vifaa,,,au watasubiri ndugu yao first lady akawafundishe? hata ukisema kuna barabara watafundishwa nazo?kutibiwa je.:A S 12:
 
Nikitinga mitaa ya Mtanda, Jamhuri, Mitwelo, Kariakoo, Mikumbi, Mpilipili, Sabasaba; Manispaa ya Lindi imepambwa na bendera za CCM kukiwa na uchache wa bendera za Chadema. Wananchi wa Lindi wamesikika wakinena hawatadanganyika na kujiunga na chama cha Kaskazini, wao sio watu wa kufanywa wa mwisho. Hawatafanya kosa kuiacha CCM iliyoiunua maisha ya Lindi kuipitia sera nzuri mfano ujenzi wa barabara na mashule ya kumwaga.

Wajiangalie, wawaangalie na wakaskazini. Wakiona tofauti wajiunge, wakikataa wafe na umaskini wao! Fananisha Nachingwe Liwale na Marangu au Arumeru? Tupa kule kama hawataki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom