Utata wa Kauli-mbiu ya Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata wa Kauli-mbiu ya Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Jun 9, 2012.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  2.jpg

  Kauli mbiu ya 'Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo' kwangu mimi naona inaleta utata hata haileweki na nadhani inajichanganya na kujipinga yenyewe. Nakubaliana kwa asili mia moja na kauli ya 'Vua Gamba', kwani Watanzania wote tunapenda magamba ndani ya CCM na serikali kuacha ufisadi na kuwa wazalendo, yaani 'Vaa Uzalendo'.

  Kauli ya 'Vaa Gwanda' kutokana na sera za CHADEMA nazo zinalenga katika kuvua gamba. Kwa mantiki hiyo basi ukivaa gwanda moja kwa moja unaashiria kuwa wewe ni MZALENDO!! Hivyo basi kauli mbiu ambayo Watanzania wote tunatakiwa kuifuata ni 'Vua Gamba, Vaa Gwanda' kwani kwa kufanya hivyo unatetea uzalendo.

  Ningependa kuwauliza wale/yule aliyetunga kauli hii ya 'Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo', kuwa je wanaovaa magwanda si wazalendo. Kama si wazalendo ni kitu gani walichokifanya au kukisema kuwafanya wao kuwa si wazalendo?

  Katika kuangalia mantiki hii kwa ujumla, haihitaji elimu ya juu kuweza kupambanua ni yupi ambaye anatetea uzalendo.

  Wale ambao wanadhani kuwa wananchi hawana akili ya kuweza kupambanua kuwa ni kitu kipi ni chema au kibaya kwao, aidha wamelala usingizi wa pono, au hawajaona alama za wakati. Ukiangalia kauli mbiu hii tata utagundua kuwa wanaitoa ni magamba halisi ambao wanataka kuchanganya watu akili kwa kujificha nyuma ya neno 'uzalendo'.

  Kwa mfano tu, nimeshaona mara nyingi mwizi anayekimbizwa na watu kujichanganya na kundi na yeye kuanza kuita, 'Mwizi...mwizi..' ili kupoteza lengo aweze kuokoka na ghadhabu ya umma. Lakini hata hivyo akiondoka hapo, hataacha tabia yake ya wizi!!
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Uzalendo ni nini? Kwa nani? Kwa manufaa ya nani?
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuvaa uzalendo bila kuvaa gwanda. Tumeona wanaotaja mafisadi na kutetea raslimali za watanzania wengi wao ni wavaa magwanda. Na waliotajwa kwenye list of shame wote ni kutoka chama kile kile chenye watu walewale ambao leo wanaitwa magamba. Wakivua magamba = kuvaa uzalendo, ukivaa uzalendo = kuvaa gwanda.

  Hii copy and paste haikutumia akili, imechakachua falsafa kama jinsi walivyo chakachua vituo 52 hewa kule Arumeru na kukwapua kura zaidi 5000 za urais kule nyamagana.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wanajiuliza ni kwanini viongozi wa CCM wamekazana kuiibia hii nchi? mikataba mibovu, nyumba za serikali, EPA, Meremeta, wanyama hai wanaibwa, rada, sasa leo tunaanza kupata 'hint' wanasema 'vaa uzalendo!

  Mwizi mwenye uzoefu miaka 50 anasema vaa uzalendo! Mimi nahisi CCM wana definition yao ya neno 'uzalendo'.
   
 6. Mbavu mbili

  Mbavu mbili JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 804
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  INASHANGAZA KUONA JINSI
  AMBAVYO the green party wanatumia muda mwingi kujibu kauli mbiu za hao chadema...mimi nilifikiri wangekuja na kauli mbiu yenye kuhamasisha ma dvt zaidi...na siyo hiyo
  huu ni mtazamo tu; nahisi kama wanazidi kuwapa umaarufu hao wazee wa peoplezzzz
   
 7. Zux de

  Zux de JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wao ni wazalendo?
   
 8. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  vua gamba, vaa gwanda........................huu ndo ubunifu
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,759
  Trophy Points: 280
  Vaa uzalendo my foot ,wezi tuu hawa
  na huu mkutano wao wanakula pesa zetu
  wakati kuna watu wanataabika vijijini
  hawana hata nguo za kuvaa mwilini NO LONGER.jpg
   
 10. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  chanzo kikuu cha matatizo ni viongozi wa nchi ambao ni wanachama wa ccm kukosa uzalendo,wanajitafunia nchi kama hawana akili nzuri, kwangu mimi gwanda ni ishara ya kupigania nchi ili kutetea maslahi ya wananchi na huu ndio uzalendo. na viongozi wa cdm at least wamenionyesha kwamba hicho ndio wanachokifanya kwa sasa.

  kwangu mimi gamba ni ufisadi, wakisema vua gamba vaa uzalendo ina make sense, yaani acha ku sapoti ufisadi anza kutetea maslahi ya wananchi kwa faida ya wananchi, na hicho ndio cdm wanachopigia debe. Lakini, kabla ya kuanza kuongelea uzalendo wasimame majukwaani wafunguke wazi jinsi wao walivyovua magamba yao na waonyeshe hadharani uzalendo waliouvaa baada ya kuvua gamba, bila hivyo naona kama wananitusi na kunifanya mimi mpumbavu, dumb na punguani
   
 11. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  du hapo yatakiwa upembuzi yakinifu
   
 12. K

  Konya JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hayo magamba imekua yanajiotea tu kila mahali, linahitaji ufafanuzi wa kina hili,sina wasiwasi na magwanda coz hata yakichanwa hayana effect yoyote zaidi ya kujivua tu magamba yaliyoshikana toka tulivyo kubaliana kama chama kwenye kale ka mkutano ketu vinginevyo ni kutaka kujihuisha kutoka kwenye aibu
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hawa akili zao zimedumaa sana. Ndo maana maendeleo yapo hapa kwa kukosa viongozi wabunifu.
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  kila siku wanakuja na staili mpya au ndo "THE SOUNDING BRASS"..
  hawana jipya tumechoka na propaganda na uenezi tunataka vitendo tuu
   
 16. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Chana gwanda na gamba vaa uzalendo.mbona ccm hawaeleze uzalendo waliko upeleka ili uvaliwe.
   
 17. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,450
  Trophy Points: 280
  Sisi hatutaki slogan mbali mbali eti vaa nini .... vua nini. We want action.
   
 18. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwanza kitaa haitobamba kwa kuwa slogani yenyewe ndefu na inachosha kutamka, wataaibika sasa hivi nyie subirini
   
 19. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  CCM kinaanza kujisogeza taratibu kuwa Chama cha Upinzani rasmi. Wasipotibu huu ugonjwa wao sugu wa ufisadi hata wangeandika vipi ni bure.
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  mbona ipo perfect haina utata wowote
   
Loading...