Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Jamani kuna hii meseji ambayo Voda mnatuma kila siku kwa wateja wenu imekuwa kero sasa. Mimi mpaka nimeamua kuiweka hiyo namba yenu blacklist lakini bado ni kero

Eti "Mmiliki wa 757******* umechaguliwa kushiriki katika droo ya TZS 5,000,000 kesho!"

Mnaboa bhana, kila siku meseji lile lile, ukiona mtu hafuatilii si unaachana nae, ya nini kusumbua wateja kila kukicha?? Ovyo kabisa
 
Facebook Hii ya bure cjaelewa kabisa sahivi picha hazifunguki mpaka data
Mi naona isiwe ya mkate tu data km zamani raha ya Facebook ni picha sio maandishi
Imeniboaa!
 
  • Thanks
Reactions: THT
Facebook Hii ya bure cjaelewa kabisa sahivi picha hazifunguki mpaka data
Mi naona isiwe ya mkate tu data km zamani raha ya Facebook ni picha sio maandishi
Imeniboaa!
Wamefilisika, wanapenda kuiga kwa tigo wakati uwezo wao mdogo ndo maana wameondoa picha kwenye fb ya bure walionjesha kwa muda mfupi walipo piga mahesabu wakakuta wanapata hasara wakaamua kutoa picha yabakie maandishi. Kama kuchati kwa maandishi hawajui kuwa tunaweza hata kutumiana sms za kawaida waache kutuzingua vodacom.
 
Wamefilisika, wanapenda kuiga kwa tigo wakati uwezo wao mdogo ndo maana wameondoa picha kwenye fb ya bure walionjesha kwa muda mfupi walipo piga mahesabu wakakuta wanapata hasara wakaamua kutoa picha yabakie maandishi. Kama kuchati kwa maandishi hawajui kuwa tunaweza hata kutumiana sms za kawaida waache kutuzingua vodacom.
Tigo wako juu baba ni baba unatumia Facebook bila shida lkn RAFIKI zangu VODA waliiga km ulivo sema wakaona huu mziki mnene
 
Nilidhani ni mi peke yangu nimejaribu kuuliza watu wawili watu nao wakasema wana matatizo kama hayo kama ni tatizo naomba mlirekebishe hashtag sokohuria
 
Hivi malalamiko haya yanashughulikiwa na nani? Maana tunatuma kero zetu, hakuna reply yoyote inayojibiwa na wahusika, wala hawajali. Kwa maana hiyo wameshatosheka na kujiona wapo juu sana na kuwa kila mtanzania hana ujanja wa kukwepa huduma zao.
Haya maudhi nimeyashuhudia nilipofanya muamala wa kulipia malipo ya bill ya maji, Idara ya maji mjini Tabora Tuwasa Trh 22/11/2016.
Malipo hayo hayakufika sehemu husika, hali iliyopelekea kampuni kuja kusitisha huduma.
Nilipofuatilia nikaanza kupigwa danadana kwamba pesa ipo hewani! Hewa gani inayomeza pesa za watu?
Pia nikaelezwa kwamba nivumilie na kusubiri masaa 72.
Nikasubiria masaa72 na hakuna marejesho yoyote yaliyofanyika. Nilipo fuatilia tena, nikaelezwa kuwa wamewasiliana na mtu anaeitwa biller wa maxcom ulipokwamia muamala.
Sasa tunaelekea siku ya 10 bila muafaka wowote.
Nabaki kujiuliza, hivi kampuni kubwa kama Voda, yenye watu wenye uweledi mkubwa, yaweza kufanya ujinga huu bila kutanzua tatizo la kawaida la kiufundi siku zote hizo?
Nimekuja kugundua suala hili limekuwa sugu kwenye kampuni hiyo, yaani hivi sasa imekuwa ni kijiwe cha kudanganyia watu. Ukituma pesa, yaweza kukuletea usumbufu sana na bila msaada wowote hasa inapotokea una jambo la dharula kama nililokuwa nalo mie.
Siku niliyopanga kuchukua hatua za kisheria, hapatakuja kuwa na lugha za kitapeli tena za kunituliza kama wanazotumia sasa kunitapelia. Na nitapenda kila mdau wa mawasiliano ya Voda ambaye hajaguswa na kadhia hii, ajiandae kupata suluba ya maudhi kama niliyopata mimi, hata kama hajapatwa, basi aelewe uozo wa miamala ya kifedha unaofanywa na Vodacom hivi sasa, ili aweze kuchukua tahadhari.
Na kwa usumbufu niliopata, katika maisha sitakuja kuthubutu tena kupitishia muamala wangu kwenye kampuni hii ya simu ya kitapeli. Baada ya kumalizana nao sitahitaji kwa njia yoyote ile kutumia huduma za aina yoyote za Vodacom kutokana na uharamia huu wa mawasiliano niliofanyiwa.
Kama habari hii itasomwa na wahusika, waangalie namba hii 0752-914659 kuhakikisha ninayoyasema kabla sijachukua hatua madhubuti ninazozijua mimi.
 
Tatizo langu kwenye mtandao wa vodacom ni kuhusu vocha Mara ninapo ingiza nashangaa,mfano naingiza shilingi elfu moja 1000/= nashangaa napata ujumbe uliounganika kwamba umekatwa VAT 152.23 Na ukingiza Mia tano500/=unakatwa VAT.71.9 nashangaa nikwanini ? Wakati Voda kama Voda hamjawai wajulisha wateja kwamba kuna VAT?ndio kitu kinaumiza sana.
 
Ulishawahi kujiuliza kwa biashara yenye Wateja let's say minimum 5 million, ukiwa unajichukulia shilingi 1 kila lisaa limoja kwenye account zao mwisho wa siku utakuwa na kiasi gani?
Naona watu wengi wamelalamika masalio kupotea kwenye account zao na isitoshe malalamiko yamezidi kuwa mengi daily.
Nimejaribu kuota kama Lema. Nahisi ndoto pia hutimia kama zikifanyiwa kazi.
 

ASKARI WA TANZANIA BUILIDING AGENCY MKOA WA DAR WANALALAMIKIA T.B.A KUWAFANYISHA KAZI KWA MUDA MREFU BILA MKATABA WA KAZI.,WAPO ASKARI WA MIEZI 8,9,10 NA WA MWAKA MMOJA NA NUSU BILA YA KUPEWA MKATABA WA KAZI.



Rejea hotuba ya Rais JP Magufuri kuagiza kuwa usimfanyishe mtu kazi bila mkataba wa kazi.Taasisi ya serikali Tanzania bulding agency (T.B.A) mkoa wa Dar es salaam iliyoko chini ya wizara ya ujenzi imekuwa sugu kutokutoa mkataba kwa askari wake wanaolinda nyumba za serikali.
Askari hao ambao wanalalamikia uongozi huo wa (T.B.A) wa mkoa wa Dar es salaam kwa kuhujumiwa kutowapa mkataba wa kazi kwa muda wote huo,wapo askari wengi ambao wakinung`unikia chini kwa chini kwa kuhofia kufukuzwa kibarua cha kazi.
T.B.A mkoa wa Dar es salaam imekuwa ikiwalipa mshahara askari hao jumla ya Tsh.180,000 kwa mwezi ni sawa na Tsh.6000 kwa siku.
Askari hao wanafanya kazi masaa 12 bila kupewa overtime ya masaa yanayozidi.
Askari wamekuwa hawapati malipo ya ziada siku za sikukuu wakiwa kazini
Tukirudi nyuma kwa askari wa mkoa wa Dar es salaam kunaposho ya chakula Tsh.300,000 inatolewa kwa askari wote wenye mkataba na wasiyo na mkataba.lakini posho hiyo inawafikia baadhi ya maskari wachache na wengi wao hawaipati posho hiyo. Je posho ya chakula ya askari wa mkoa wa Dar es salaam inakwenda wapi? Kama ipo kwa nini hawapewi?
Mpaka sasa kuna maskari wa mkataba wanadai pesa zao za malimbikizo ya mishahara yao zaidi ya miaka miwili je watalipwa lini?
TBA imekuwa ikiwacheleweshea maskari wake mishahara kitendo ambacho kinawaumiza sana wafanyakazi wake wamekuwa wakitoa mshahara tarehe 8,9,15 ya mwezi mpaka leo hii tarehe 8/12/2016 hatujapata mshahara wa mwezi wa kumi na moja.
Uwongozi huo umekuwa ukiwadhalau na kuwapuuza maskari wake hawo kwa kushindwa kuwapa vitendea kazi kama vile tochi, filimbi, buti, makoti ya mvua na silaha n.k.
Tunaomba waziri mwenyedhamana hiyo afatilie kwa kina kilio hicho cha wafanyakazi hao ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu na kuwasikiliza kilio chao yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom