Vodacom ni balaa

Kama wadau wengine walivyosema...mazoea ni mabaya sana...nimefanya majaribio ya kubadili line...lakini wapi ikashindikana kuna contacts nyingi sana za watu za kibishara na kawaida....lakini lazima nichomoke one day!

Mkuu hata mimi nilikuwa nashindwa kuhama lakini taratibu nimehama nilicho fanya nikawa na cmu 2 moja ya tiGo na ingine ya Voda watu wangu wa tiGo nikawa nawapigia kwa tiGo tena nilikuwa na namba nzuri sana ni hii ****900400 bahati nzuri nikapata tiGo namba hiyo hiyo aaah baadae nikafutilia mbali nimehama voda na sasa napeta na tiGo kwa siku gharama zangu za kupiga zimepungua kwa kiasi kikubwa kuliko nilivyo kuwa Voda sms xtreme ni 400/= kwa siku unachombeza na watu wote wa mitandao yote nchini. Mpaka sasa nimeota sugu dole gumba kwa kutuma sms.
Cha ajabu juzi kati hapa nilienda kuomba namba Zantel hizi hizi ****900400 nikanyimwa nikaambiwa nilipie Tsh.500,000/= kupata line hiyo nikamwambia mama hii kampuni inawateja kiasi gani mpaka nilipie kilo tanoi? Mbona nina namba ya voda na tiGo namba hiyo hiyo wakasema ndo sheria wamejiwekea kuwa eti namba inayo ishia na 00 lazima ilipiwe laki tano nikamwambia muda si mrefu kampuni yenu mtafulia endeleeni na utaratibu wenu.
 
ni kweli kabisa mkuu, voda ni balaa, nami nakaribia miaka 8 toka niwe na voda na nimekuwa muumini mzuri wa hii kampuni nikihofia kubadilisha number kwamba it will be inconvinient kwa jamaa zangu ( bila kujijali mimi kwanza).

yaani ukiweka sh.5000 kama vile kuna kidudu mtu flan make ukibahatika kupiga simu nne ambazo ni dakika2 nakuendelea kila moja sijui, labda uwe voda jamaa ambayo ina limit watano at a go na 15 kwa mwezi. Wakati mtandao mwingine unaweza ukadunda na 5000 (si zain) kwa siku, kwa voda atleast 15,000. Mnatuua jamani voda ama ndo asila za kagoda, richmond na dowans?

nakushauri ujijali wewe mwenyewe kwanza kisha kwa kipimo hicho hicho uwajali hao unaowaurumia.

Achana na mitandao ya kifisadi kisha washawishi wale unaowapenda na kuwajali wahame! Karibu tigo uhitaji kujisajili wala kuwasajili cha kuhofia ni degedege la tanesco tu
 
Hivi karibuni pesa zinaondoka kweli... tia elfu tano piga simu mbili ya tatu utasikiaa piiiiiii halafu calas, sijui ni ule ushuru au ni nini kama hii ni trick fulani nadhani hii ni balaaa

Kwa mara ya kwanza nimeingia kampuni nyingine (jina mezea sipo kutangaaza biashara ya mtu) ile ile elfu tano nimepiga simu kibao

aaaah, tumeshaujua bana, safi!.
 
Duuu kumbe tupo wengi tunaojeruhiwa na hawa jamaaa....aisee one day nilikuwa na balance kama ya Tshs 1050.....nikampigia mtu wa zain, nikashangaa ghafla kitufe kinalia...kucheki salio ni 0.5 then nikaangalia last call time ikawa inaonyesha 1.51 minutes. Sasa ukipiga hesabu hapo yaani ni kama dakika moja ni Tshs 695 hivi!.....This is too much kwa kweli!

Kama wadau wengine walivyosema...mazoea ni mabaya sana...nimefanya majaribio ya kubadili line...lakini wapi ikashindikana kuna contacts nyingi sana za watu za kibishara na kawaida....lakini lazima nichomoke one day![/QUOTE]

Tupo wote mkuu one day YES.
 
Mbona tulisha toa wito msusie huu mtandao mlikuwa wapi?
Mi ukoo wetu wote tunatumia tiGo voda tulisha wamwaga siku nyingi.

Kaka tutakuunga mkono soon......tusije fulishwa bure!

BWT: Fidel unatafutwa sana kule kny thread ya Chaku!
 
Eh bwana eee na mimi pia ni mmoja kati ya watu wa mwanzo kuingia vodacom [nilikimbia mobitel] na nimekuwa muaminifu mno lakini kwa sasa inanitia hasara sana na mwanzo nilifikiri mwenzangu alikuwa akihamisha 'airtime' yangu lakini sasa amehama na hali inazidi kuwa mbaya. Tatizo nililokuwa nalo ni kuwa sijui niende wapi kwenye afadhali hivyo utasaidia sana mwana jamii mwenzako kwa kushauri twende vipi [hiyo siyo kufagilia]
 
kwanza jamani huu mtandao si una mkono wa yule jamaa yetu anaitwa sijui Rosti-tamu au sio huu?
njooni tujiexpress bana!.
 
uniulize mimi

nilika nao wee mpaka ikafika point hakuna anayenipigia simu

nenda Zantel iko fresh unaweka babu kubwa kisha unakamua
 
Wanabahati niko uswekeni uku tigo na zantel tabu otherwise ningetia moto line zao.
Wito washushe bei kama wenzao simu sio ANASA JAMANI!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa nini tigo na zantel ni tabu tena? Au wameshindwa kuwekeza kwenye network?
 
sure, wengi ni brand loyal ila inafika wakati unafikiria vingine. bado sijaona mtandao makini kwa sasa. nadhani voda ilikuwa standard ila ujanja umezidi
 
Prof Nkoma of TCRA, you shoul put your EYE on this company. Wanatuua, UUUUUUUUUwi, twaaa!
 
Sio siri, Vodacom ni wachumi wa chapchap. Matangazo yao ya kuvutia lakini mikong'oto kibao. Nilishasahau hata namba yangu ya vodacom, maana ulanguzi wao uko juu mno! Tena wana kiburi cha uzima sokoni. Wenzao wanaposhauri kuleta unafuu kwa wateja wao utadhani wako sayari nyingine. Lakini wale wanaopenda sifa wanang'ang'ania tuuuuu wanaendelea tu.

Umesikia wapi kaburu akawa rafiki wa masikini?

Leka
 
Wajameni mie nina watu wangu watano wa voda jamaa lakini naona pesa inaisha faster sana hizi siku mbili
 
Mnao endelea kutumia Voda endeleeni kuwachangia mafisadi unajua yule boss mzungu wa voda analipwa bei gani? Analamba milioni 25 kwa mwezi bado malupu lupu na masolo solo.
 
Mkuu hata mimi nilikuwa nashindwa kuhama lakini taratibu nimehama nilicho fanya nikawa na cmu 2 moja ya tiGo na ingine ya Voda watu wangu wa tiGo nikawa nawapigia kwa tiGo tena nilikuwa na namba nzuri sana ni hii ****900400 bahati nzuri nikapata tiGo namba hiyo hiyo aaah baadae nikafutilia mbali nimehama voda na sasa napeta na tiGo kwa siku gharama zangu za kupiga zimepungua kwa kiasi kikubwa kuliko nilivyo kuwa Voda sms xtreme ni 400/= kwa siku unachombeza na watu wote wa mitandao yote nchini. Mpaka sasa nimeota sugu dole gumba kwa kutuma sms.
Cha ajabu juzi kati hapa nilienda kuomba namba Zantel hizi hizi ****900400 nikanyimwa nikaambiwa nilipie Tsh.500,000/= kupata line hiyo nikamwambia mama hii kampuni inawateja kiasi gani mpaka nilipie kilo tanoi? Mbona nina namba ya voda na tiGo namba hiyo hiyo wakasema ndo sheria wamejiwekea kuwa eti namba inayo ishia na 00 lazima ilipiwe laki tano nikamwambia muda si mrefu kampuni yenu mtafulia endeleeni na utaratibu wenu.

haaa Fidel umekosea ama? ya nini yote hiyo wakati vocha zao wa sie kibamba mpaka twende kimara? khaa wamejichokea nao.
 
Mnao endelea kutumia Voda endeleeni kuwachangia mafisadi unajua yule boss mzungu wa voda analipwa bei gani? Analamba milioni 25 kwa mwezi bado malupu lupu na masolo solo.
Ukiwa TiGo msg za Majuu hupati! mtandao feki kweli kweli! ka TiGo vile
 
haaa Fidel umekosea ama? ya nini yote hiyo wakati vocha zao wa sie kibamba mpaka twende kimara? khaa wamejichokea nao.

Kama mi nimekuongepea Nyamayao niombee basi hiyo namba nije nichukue kwako kama hutatajiwa kilo tano omba namba hii kama mi naongopa ****900400
 
Back
Top Bottom