Vituo vya mafuta Dar vyagoma!

Huu ni Uhujumu wa Uchumi. Period!

Kuna umuhimu wa kuwa na emergency meeting ya bunge letu.

Huu sio wakati wa mazingaombwe!
 
Hivi Mizengo Pinda anafanya nini?... Mbona kwenye critical interventions za serikali yeye anakua mtu wa kujivutavuta.

Ngeleja wizara imemwelemea, waziri mkuu kaingia mtini, Rais anajikausha... Kazi ipo.

Hapo ndo unapomkumbuka Lyatonga,...
 
Huu ni Uhujumu wa Uchumi. Period!

Kuna umuhimu wa kuwa na emergency meeting ya bunge letu.

Huu sio wakati wa mazingaombwe!

Hii kuongeza gharama ya posho kwa hawa jamaa kwenda kulala tu kule, nina uhakika 99% ya wabunge hawana uchungu na wengi hawajui kama jamaa wamegoma kuuza mafuta leo, maana wao wanalipwa lita 2000 kama sikosei kwa mwezi, Dawa ni sheria ichukue mkondo tu si ipo!
 
...hatutakiwi kukurupuka kulaumu ewura...kwani waliohakikishia taifa kuwa mafuta yapo ni waziri na naibu wake.....ewura kimsingi walikuwa wanataka mlaji asiumie ndio maana hata wakakagua pumps.........tatizo ni wizara kwa kutupa hakikisho la uwongo...
 
Hii kuongeza gharama ya posho kwa hawa jamaa kwenda kulala tu kule, nina uhakika 99% ya wabunge hawana uchungu na wengi hawajui kama jamaa wamegoma kuuza mafuta leo, maana wao wanalipwa lita 2000 kama sikosei kwa mwezi, Dawa ni sheria ichukue mkondo tu si ipo!

Tricky!
La muhimu ili uwe mwana siasa ktk Tz ni kukosa aibu. Hali ndo hii! Hawa jamaa wanaokaa vikao Dodoma wanalipwa Tshs kwa lita. Sasa ukishusha bei ya mafuta maana yake sasa wapate pesa kidogo kuliko mwezi uliopita. Watakuelewa?

Taabu kabisa! Ndo ubaya wa kuwa na kazi ambayo elimu kubwa siyo kigezo chake.
 
Invisible,

..hata kama ewura walisema kwamba mafuta yapo, statement yao inaathiri vipi upatikanaji wa mafuta?

..mimi naona wananchi kama wanawaogopa wafanyabiashara na wanatafuta bwege wa kumtupia lawama.

..uwoga wetu ndiyo huo huo unaathiri vita dhidi ya rushwa na ufisadi. tunapaswa kutowaogopa wadai rushwa.
 
Hii ni adha ya kuchanganya biashara na siasa. adha ya kukubali chama na viongozi wetu kufadhiriwa na serikali. Adha ya serikali kutegemea misaada na kuwa kama matonya kuomba wafanyabiashara kuchangia vitendea kazi kama laptop na pikipiki kwa ajili ya ulinzi wa nchi.

Ni aibu kwa ulinzi na usalama wa wananchi kutegemea michango ya wafanyabiashara kama hawa wa mafuta. Unategemea nini kwa serikali ambayo wananchi wanalipa kodi na bado inakubali kudharirishwa kwa kuchangiwa vipikipiki na wafanyabiashara? pesa ya kodi inaenda wapi?

Hebu tizama serikali ya awamu ya kwanza kama ilikuwa na ubia na hawa wafanyabiashara? sasa hivi wanasiasa wetu wamewekwa mifukoni na wafanyabiashara tena wengine washukiwa wa EPA wanakaa meza moja na wakuu wa nchi. Unategemea nini katika maamuzi ya msingi kama hili la mafuta kujadiliwa na kupewa ufumbuzi wa msingi?

Uongozi na hatima ya nchi yetu hiko mikononi mwetu wananchi.

Serikali nayo ibadilike katika kufanya umatonya na wafanyabishara katika kuchangia uendeshaji wa shughuli za serikali wakati wananchi wanalipa kodi.


Serikali inaitaji kusimamia soko la nishati na ikishindwa inaweza kujikuta ikipoteza legimacy yake. Pili, wakome kufunga ndoa na wafanyabiashara.
 
Hii kuongeza gharama ya posho kwa hawa jamaa kwenda kulala tu kule, nina uhakika 99% ya wabunge hawana uchungu na wengi hawajui kama jamaa wamegoma kuuza mafuta leo, maana wao wanalipwa lita 2000 kama sikosei kwa mwezi, Dawa ni sheria ichukue mkondo tu si ipo!

Hii sheria ni ipi?

Huku mtandaoni nimekutana na hii...
Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi, ni pamoja na yale yote yenye kusababisha hasara kwa mamlaka ya serikali.

hayo hapo juu yalisemwa na JJ.

Sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1984 inavieleza vitendo vya uhujumu uchumi kuwa ni pamoja na vitendo vya rushwa na kuhodhi mali au bidhaa ili kusababisha bei kupanda au kushuka.
Kwa vile wamesababisha serikali kutopata ushuru, basi hii itawafaa,yaani sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 1983/84





Katika makala haya ...Inahitajika operesheni ya wahujumu uchumi


Utaona kuwa bunge liko makini(wabunge wa upinzani na hata CCM)

Kuna umuhimu kuonyesha wakati wa kuhadaa kadamnasi UMEISHA!

My take, bunge wakae na kuangalia hiki kitu kwa haraka!

source:http://www.bunge.go.tz/bunge/Qs_Ls.asp?Menu=qsLs&PTerm=2005-2010&vpkey=1442&page=7

Hiyo link hapo juu haina tofauti na yanayoendelea kuhusu Mafuta!
 
Last edited:
Kwani jamani kama mafuta hamna kwenye depot si kiasi cha kutuma magari 2 tu ya watu wa wizara, kukiwa na Polisi na TISS mbrs kukagua kujua ukweli???

Also mafuta yanapofika nchini kunakuwa na date ambayo contract ilitoka ya kununua hayo mafuta na bei za dunia ni public sasa tabu ya kujua hawa watu wamelipia kiasi gani mafuta inatoka wapi???

Mbona jamani vitu tunafanya analog wakati sasa hivi mambo ni digital???
 
Kwani jamani kama mafuta hamna kwenye depot si kiasi cha kutuma magari 2 tu ya watu wa wizara, kukiwa na Polisi na TISS mbrs kukagua kujua ukweli???

.... hii hali kama serikali itashindwa itabidi watuachie wananchi....kama vibaka wanaokwapua sheni wanachomwa moto just because mfumo wa haki umefanya waendelee kushikwa na kuachiwa hadi wananchi wakakosa uvumilivu....basi ipo siku VITUO VYA MAFUTA VITACHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE HASIRA.....KWANI NAO HAWANA TOFAUTI NA VIBAKA........haiingii akilini mafuta ni dola 50 kwa pipa ,tuuziwe bei ileile ya wakati yalipokuwa dola 140 kwa pipa...kama ni rationale leo hii mafuta yangetakiwa yawe si zaidi ya shilingi 1,000 pamoja na kodi zote zote!!!

serikali ikishindwa kuwachuukulia hatua ...basi wananchi tutavichoma moto vituo vyao....tuone watamshitaki nani!......wananchi wenye hasira kali?????
 
Main energy sources zinazosukuma uchumi wetu mbele ni mafuta na umeme-
SWALI: mbona umeme ukikatika hata wiki nzima hatulalamiki kama tunavyolalamika hapa kwa kukosa mafuta kwa siku kadhaa?
 
- Haya ndio mambo ya ubepari tuliyoyarukia na kuidhinishwa na bunge letu bila kuyaelewa, serikali inahusika vipi na hii ishu ya Free Market? Tumerukia maneno ya Free Market sasa yanakuja matatizo hatuna sheria in hand ya ku-deal nayo, kama kawaida sasa tunamrushia kila mtu mwingine lawama, wakuu ifike mahali tuache kukimbia vivuli vyetu.

- Wakuu hili ndilo tatizo lilowafanya USA wakapitisha sheria moja inayoitwa, Anti-Trust Act, ambayo iliaznishwa kutokana na ishu kama hizi za kampuni moja ya Rockfeller kumiliki percent kubwa ya biashara ya mafuta na kuwa na power ya monopoly,

Sasa sisi sheria iko wapi? Hili tatizo lipo mpaka kwenye makampuni yetu ya simu pia! What a shame!
 
EWURA cut fuel prices by 27%. Trouble is, EWURA has no fuel. We cannot buy fuel at their reduced prices! It seems that we now cannot buy fuel at any price!

There has been a failure of process. Effective control guards against backlashes (illegal or otherwise). Does EWURA have Plan B or not? Did it not work out what to do in case things worked out this way?

If EWURA did not foresee the possibility of collective sabotage by the oil companies, then they have just forfeited their right to existence. They should be replaced by a more proactive controller.
 
Huku ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia. Lakini pia EWURA pia wanastahili lawama. Inaonekana hawakufanya homework yao vizuri. indicative prices ziko chini sana. Matokeo ndiyo haya.
Una hisa katika hayo makampuni ya mafuta?
hizo indicative prices unazodai zipo chini una theory gani ya kusupport ur argument?
Mkulu nakuheshimu....
 
Mwanzoni walisema wanaomba kwanza stock yao iishe ndio washushe bei. Sasa wanadai hawana mafuta. Huu ni ubabe wa kijinga kabisa. Washughulikiwe.

Hivi Serikali ikiamua kutaifisha hivi vituo hawa jamaa si wanaweza kukimbilia mahakamani na kuibwaga serikali? Ni nini sasa kifanyike ili tuwabane kila kona na kuwaondoa kabisa kwenye hiyo biashara bila kuathiri utawala wa kisheria? Naombeni jibu!!
Sheria ya Uhujumu Uchumi,Sheria ya Mafuta na ile ya EWURA.Zatosha kuwatoa kwenye Industry.
 
Shibe ni mwana malevya, hao Oilcom wamelewa pesa sasa wanafanya vituko. TPDC nafikiri haiukuachishwa kiubaya ilikuwa ni kuwapa watu wengine chance ya kuonyesha uwezo wao. sasa wameleta jeuiri lazima kutakwua na mkono wa mtu humo, kama siyo fisadi kutoka mjengoni dodoma.

Unajua nchi kama Rwanda na Burundi wamethiliwa na vita ila kama ungeniambia nichague wapi niishi ningeenda Rwanda, principled country, huwezi kuamka leo ukanzisha sheria yako unayoijua ya ulaji ukafanya implemetation za kijinga kama Tanzania.

Tuzidi kushukuru kwa kuwa wapumbavu, hatuna choice, kila kitu ndiyo mzee.

Ebo mpumbavu ni wewe peke yako, nenda huko Rwanda na Burundi unakoona panakufaa, TENA LEO LEO. kesho utasema bora ungezaliwa nyumba ya jirani wanakopika pilau kila siku.
 
....wanafanya hivyo kwa sababu wanajua hakuna serikali pale,hizo kamba zao za kusema stock imekwisha ghafla ni upumbavu wa hali ya juu na uwongo wa kitoto,serikali lazima wapate sababu za kueleweka na zinazokubalika kisheria kwanini hawakuagiza mafuta on time wakati wamepewa hilo jukumu na kama kuna uzembe au any sabotage hawa ng'ombe lazima watiwe adabu,na uchunguzi(physical) kwenye mapipa yao lazima ufanywe sio data zao zao za kupikwa...hakuna mtoto hapa wa kudanganywa na tunajua hizi ni deal zao za kilafi tuu ili kupata super profit,dawa ni kuwafuta kwenye biashara ya mafuta forever na kuwafikisha mahakamani kuwachapa fine za kuwafilisi mpaka mali zao,hatuwezi kuvumilia sabotage kama hizi za kurudisha nchi nzima nyuma kiuchumi na kutishia usalama wetu...inakuwaje leo oil price ikipanda new York nao wanapandisha for the same reason lakini ikishuka eti stock ni ya mwezi uliopita? sasa ni time ya kuwafanya mfano kwa watu wote wenye tabia kama hizi na kuhakikisha hakunasector/mtu atatuchezea kwa namna hii tena...ni EWURA/waziri wa nishati nao watimuliwe kwa uwongo wao wa kusema last week kuna mafuta ya kutosha na Ewura wameshindwa kuwadhibiti hawa walfi wakti kuna sheria kibao zilikuwepo za kuwatia adabu lakini hawakufanya kitu...lazima kuwe na zero tolerance kwenye vitu kama hivi la sivyo tutazidi kuwa maskini tuu.
Kwa nini Waziri na EWURA wajiuzulu?Hiyo conclussion kwamba wamedanganya mmeitoa wapi?
Zero torelance yes,lazima iwepo pale mambo yapokwenda ndivyo sivyo.
Do not forget, hii ni serikali kabla ya kutoa maamuzi magumu lazima wajiridhishe kuwa all bases are covered.
Usihofu ndg yangu, serikali inajua nini cha kufanya to get out of this crisis.
Believe me.
 
Hivi Mizengo Pinda anafanya nini?... Mbona kwenye critical interventions za serikali yeye anakua mtu wa kujivutavuta.

Ngeleja wizara imemwelemea, waziri mkuu kaingia mtini, Rais anajikausha... Kazi ipo.

Hapo ndo unapomkumbuka Lyatonga,...
Mlitaka waende kwenye magazeti na TV ndio mjue wanafanya kazi?
 
Hapa ndipo ninapotaka kuisikia serikali, meno wanayo, uwezo upo, nawasubiri....... Even if we have to wait for 2 weeks in this dilemna, as long as you are on a right course. Umma wa watanzania unataka wafanyabiashara waelewe kuna Serikali, yenye meno, bila kujali uhusiano na historia.
Hapo sasa.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom