Vituo vya mafuta Dar vyagoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituo vya mafuta Dar vyagoma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iga, Jan 12, 2009.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI hii ya mafuta ambayo inaelekea kuagiza karibu nusu ya mafuta ytanayoagizwa Tanzania, toka EWURA kutangaza kushushwa bei imekuwa ikitufanyia vituko kwa kuhakikisha karibu vituo vyao vyote havina peteroli.

  Je, serikali inajua kinachoendelea na matajiri hawa wa OilCom ambao baba yao tunamjua kama mcha Mungu pamoja na madhambi yake mengine hakuwa mtu wa dhuluma. Iwaje leo wanawe, wafikia kwake na mameneja wake wnatufanyia hivi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 13, 2009
 2. RR

  RR JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Mkuu umejaribu kupita vituo vya BP ama Total leo? They are in the same boat.
   
 3. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Shibe ni mwana malevya, hao Oilcom wamelewa pesa sasa wanafanya vituko. TPDC nafikiri haiukuachishwa kiubaya ilikuwa ni kuwapa watu wengine chance ya kuonyesha uwezo wao. sasa wameleta jeuiri lazima kutakwua na mkono wa mtu humo, kama siyo fisadi kutoka mjengoni dodoma.

  Unajua nchi kama Rwanda na Burundi wamethiliwa na vita ila kama ungeniambia nichague wapi niishi ningeenda Rwanda, principled country, huwezi kuamka leo ukanzisha sheria yako unayoijua ya ulaji ukafanya implemetation za kijinga kama Tanzania.

  Tuzidi kushukuru kwa kuwa wapumbavu, hatuna choice, kila kitu ndiyo mzee.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Roya Roy, jibu lako linapatikana kwa hii habari hapa chini.

  Ewura sasa inatosha -Waziri
  Waandishi Wetu
  Daily News; Sunday,January 11, 2009 @21:15

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima amesema kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imejikwaa mahali, itoe taarifa serikalini, lakini anaamini miaka miwili sasa tangu kuanza operesheni yake nchini, inatosha kuanza kuonyesha uwapo wake.

  Sanjari na hilo, mamlaka hiyo imeonya kuwa kama kuna wafanyabiashara wanacheza mchezo mchafu ili mafuta ya petroli yaonekana yameadimika, sheria itachukua mkondo wake. Akizungumza jana ofisini kwake, Malima alisema yapo mambo ambayo Ewura bado inajifunza, lakini yapo mambo ambayo kimsingi, yanafaa kuchukua hatua.

  “Ewura inakua, kuna mambo tunaweza kuyaelewa kuwa ni mambo ya kujifunza, lakini mengine hapana…miaka miwili inatosha. Wakijikwaa, kwa sababu kujikwaa si jambo la aibu wala la ajabu, watoe taarifa kwetu,” alisema Malima.

  Alisema serikali itatumia sheria zake katika kuwabana wafanyabiashara wanaokiuka taratibu za biashara ya mafuta nchini, na kusababisha bidhaa hiyo iuzwe kwa bei ghali katika maeneo mengi nchini. “Mara nyingi ninyi (waandishi wa habari) mnatuuliza sasa mtafanyaje? Tutatumia sheria zilizopo. Nondo zipo.

  Ni mwendawazimu anayeweza kuamini kuwa nondo hazipo, lakini wakati mwingine serikali inatumia busara,” aliongeza Malima. Aliwaonya wafanyabiashara hao kuwa wasije wakailaumu serikali mbele ya safari kwani inao uwezo wa kuwabana kwa kutumia sheria hizo zilizotungwa na Bunge, ikiwamo Sheria ya Mafuta ya 2008 iliyopitishwa bungeni Aprili mwaka jana.

  Wakati Naibu Waziri akitoa msimamo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu ameonya kuwa wafanyabiashara wanaodanganya kuwa kuna uhaba wa petroli nchini, wanajitafutia matatizo. Akizungumza kwa simu jana baada ya Jiji la Dar es Salaam kushuhudia upungufu wa petroli, Masebu alisema hilo si tatizo kubwa kwani wanafahamu Kampuni ya GAPCO inayo mafuta mengi, lakini pia meli zaidi zilitarajiwa kutia nanga jana jioni.

  “GAPCO wanayo mafuta ya kutosha na meli nyingine zinaingia leo (jana). Hata huo upungufu hauwezi kubadili bei, na wala hauwezi kutokea upungufu kama ule wa mikoa ya Iringa na Morogoro,” alisema na kuongeza: “Tumefuatilia hali hiyo na hakika tutawashughulikia kisheria wale wote wanaotaka kuanzisha tatizo ambalo halipo.”

  Gazeti hili lilitembelea vituo mbalimbali vinavyouza petroli jana na kukuta hakuna huku mafuta ya taa na dizeli yakiendelea kuuzwa kama kawaida. Miongoni mwa vituo maarufu vinavyouza petroli ambavyo vimekutwa havina bidhaa hiyo ni pamoja na BP, Oryx, Total, Engen, Oilcom huku vituo vya Kampuni ya Gapco vikionekana kuuza bidhaa hiyo kama kawaida.

  Licha ya petroli kutopatikana katika vituo hivyo tangu Ijumaa jioni, mabango katika vituo hivyo yameendelea kuonyesha bidhaa hiyo inauzwa kwa Sh 1,233 kwa lita moja bei halali iliyotangazwa na Ewura. Wakizungumza na gazeti hili, wafanyakazi wa vituo vilivyokutwa kutokuwa na petroli, walidai mafuta hayo hakuna katika hifadhi kuu za kampuni zao.

  “Mafuta si kwetu tu hata depot ya BP hakuna na ndio sababu unaona tunauza dizeli na mafuta ya taa pekee,” alisema mfanyakazi wa Kituo cha BP Fire. Wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamedai mahitaji ya petroli nchini ni makubwa kuliko dizeli na mafuta ya taa na ndiyo sababu yanamalizika mapema.
   
 5. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,545
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli haya ndio yanaendelea, serikali inayowajibu wa kukagua hifadhi zao zote za mafuta kijiridhisha kwamba mafuta yapo ila wamekataa kuyauza then wawafungulie kesi ya kuhujumu uchumi. Kama hawakuridhika kushushwa kwa bei wangetoa tamko rasmi kwamba hawatauza mafuta na si vinginevyo.

  The act mount to econominc sabboutage(spelling haziko sawa) maana wamekataa kwa makusudi ili kucreate demand kubwa na kuuza mafuta kwa bei ya juu.

  Mrema tutakukumbuka sana maana watu kama hawa naamini usingewahurumia hata kidogo
   
 6. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,545
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 280
  Hiii ni Tanzania tu,

  Last week walikua wanasema stock yao ya zamani haijaisha ndio maana hawajashusha bei. Baada ya kubanwa sasa wanasema wako out of stock.

  Je stock yao itawasili lini???? Na naamini EWURA washushe tena bei maana hiyo latest stock watakayoipata soon itakuwa imenunuliwa at around 70USd kwa pipa. Hapa ndio serikali inatakiwa nayo ionyeshe ukakamavu na si vinginevyo.

  Pia makampuni yenye mafuta na wamekataa kuuza wafutiwe license mara moja ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kubwa ya kuhujumu uchumi.

  Nakulilia Tanzania
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa hakuna chochote hii ni organised crime ya wenye vituo vya mafuta na sasa imefikia mahali CCM iache kuwa inapokea michango ya uchaguzi ya hawa wanyonyaji ambao baadae wanafanya robbying na watunga sera kwa manufaa yao badala ya manufaa ya wananchi. Umefika wakati sasa Serikali yetu iwe na "strategic petroleum reserve" Kwa ajili ya kupambana na hawa mafisadi wa maendeleo yetu.

  Hivi Serikali yetu haina uwezo wa Kujenga depot yake hata Porini{kwa usalama maana mijini wanaweza itia moto na kuweka ulinzi wa JWTZ kama wanavyolinda silaha zao sensitive} Ambayo itatosha kuhifadhi mafuta ya kutumia nchi nzima hata mwaka mmoja tu, ili watu kama hawa wauza mafuta wakigoma wanafungiwa leseni mwaka mmoja na serikali inachukua jukumu la kusambaza mafuta badala yao?. Likifanyika hili nafikiri serikali itakuwa na nguvu halisi ya kuwasimamia hawa jamaa, vinginevyo ni wizi mtupu kwani wenye vituo wengi wanapepea bendera za kijani za nyundo na jembe na wanajua hawawezi simamishwa kwani wao ndiyo wachangiaji wa fulana, kofia na mafuta ya Campaign za uchaguzi.
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kweli mkuu, Ni kuwabana na Uhujumu uchumi, halafu nafikiri kuna haja ya Azimio la Arusha jipya
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  KARIBU SHELI ZOTE DAR ZIMESIMAMISHA HUDUMA KWA MADAI KWAMBA HAKUNA PETROLI WALA DIZELI, NA KUSABABISHA MISURURU KWENYE SHELI CHACHE AMBAZO ZIMEENDELEA KUTOA HUDUMA. HAPA NI SHELI YA GAPCO YA ST. PETERS. HII IMEKUJA BAADA YA SERIKALI KULAZIMISHA BEI YA MAFUTA ISHUKE, NA REDIO MBAO ZINASEMA HII NI JEURI YA FWEZA NA JAMAA WANA-TESTI ZALI LA JK AMBAYE WANADAI HAWAFANYI LOLOOOOOOOTE....

  [​IMG]
  FOLENI YA MAFUTA HIVI SASA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI RODI

  [​IMG]
  WENGI WALIFUATA MAFUTA KWA VI-DUMU

  [​IMG]
  WENGINE KWA NDOO

  [​IMG]
  ADHA YA MCHOKO WA FOLENI, JAMAA KAINGIA UANI
  [​IMG]

  Source:MICHUZI
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tukiwaita wahujumu uchumi tutaambiwa tunaleta mambo ya Nyerere! Well.. tuwaite mafisadi basi! Huwezi kuzuia bidhaa na kuanza kuiuza kwa kibaba ukabakia kuwa fisadi tu.
   
 11. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Duuh! Lakini vituo vya SHELL si viko vichache sana kwa Dar?! Kama SHELL wamegoma nafikiri hizo kampuni nyingine kama BP, Agip, GAPCO, TIOT, Caltex, Total, na nyinginezo nyingi tu zinaweza kukidhi mahitaji. Au hapa ulimaanisha SHELI = ANY FILLING STATION??!!
   
 12. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kibongobongo SHELL inamaanisha any Gas Station au Petrol Station au Filling Station.
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huku ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia. Lakini pia EWURA pia wanastahili lawama. Inaonekana hawakufanya homework yao vizuri. indicative prices ziko chini sana. Matokeo ndiyo haya.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Politics zina poingia kwenye biashara hayo ndio matokeo yake
   
 15. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu tatizo sio indicative prices bali wamesema stock ya petrol imeisha wamebakiwa na disel na mafuta ya taa.

  Kama wiki chache walisema wanastock kubwa ya zamani ndio maana hawajashusha bei leo iweje basi wasiwe na stock ya kutosha???????

  Hawa wanahitaji kichapo=Futa license zao wote na faini juu. EWURA Watanzania tuko tayari tutembee kwa miguu kuliko kufaidisha watu wachache.

  Huu ni wakati wa kila mtu kutimiza wajibu wake bila kutishiwa nyau
   
 16. K

  Koba JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...hii sio free market tena ila ni umafia tuu,dawa yao ni kuondoa licence zao tuu na kuwapa ban for life...mafuta yameshuka toka 147 mpaka chini ya 50$ lakini bei zao ni zile zile za 147$,kuna ushenzi unaendelea hapa,kama hawawezi fair play waondoke tuu...hakiyamungu hawa ni kuwatia adabu na hakuna kuuza tena mafuta kwenye ile nchi na wafunge pump zao....hatuwezi kunyanyaswa na hawa walafi,fanya huo ushenzi states kwa baba wa capitalism uone kama utarudi tena kwenye biashara na jela lazima uione,free market haina maana unajipangia bei yeyote unayotaka...hawa dawa yao ni kuwafutia licence tuu na kuwapa ban for life na watu honest watakuja
   
 17. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni Tanzania Tu hii sector haijawa regulated

  Katika nchi zote duniani Mafuta, Umeme na Company ya simu ni heavily controlled kwa usalama wa nchi. Hivi vikiachiwa kwenda kiholela kama sasa
  security of the state iko at risk.
  nadhani uliwahi kujiuliza Swali kwa nini kwenye vita yeyote reserve ya mafuta, power stations, telecom n.k ndio vitu vya kwanza kuwa attacked???

  Serikali ifanye kazi yake sasa nasema Futa lisensi zao wote waliogoma kuuza mafuta
   
 18. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hao wauzaji wa mafuta ni wauwaji kabisa. Hakuna haja ya kuwaonea huruma.Serikali ifute lesini zao mara moja kuanzia leo na wasipewe tena. Wapewe watu wanaoweza kufanya biashara na sio wababaishaji. Hakuna haja ya kubembelezana katika hali kama hii. Ni hivi karibuni wasambazaji walidai kwamba kuna stock ya kutosha zaidi ya siku 28 kama sijakosea iweje leo hii mara ghafla hakuna bidhaa hii kama sio uhuni ni kitu gani? Je mikoani nao wamegoma au wao bado wanauza mafuta??
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mod nafikiri hii thread na ile ya OIL.COM zinafanana 100%.

  Hivi Sheria ya uhujumu uchumi ya 1984 si bado inafanya kazi?. sasa ni wakati wa sheria kuchua mkondo wake basi asiyetaka biashara ya mafuta akalime sasa. Hapa cha kufanyika ni vyombo vya dola kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye hivi vituo na ma depot yote yakikutwa mafuta yakamatwe na mwenye kituo afunguliwe mashitaka chini ya sheria ya uhujumu uchumi 1984 na pia kufungiwa kutoa huduma ya kuuza mafuta kwa miaka 5, nina uhakika sheria ikichukua mkondo hakuna atakaye leta uhuni tena in the future, Yaani hii nchi sasa inabidi iendeshwa kama "enzi za mwalimu" ambapo maslahi ya wananchi yanakuwa mbele.
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  MWKJJ,

  hii ni kweli that is economic sabotage. sasa tuone JK atawafanya nini hawa jamaa manake ndo wachangiaji wakubwa wa chama chake kiuchumi. Kama Bush alivyosema leo " many times, it is friends who let u down terribly". Mh. JK hiki ni moja ya vipimo kwako. I really miss Mh. Edward Moringe Sokoine..hizi blah blah za wafanyabiashara kubaka uchumi kwa jasho la mwananchi kulikuwa hakuna. Mh. JK, nakupa benefit of doubt naomba ufute huu utamaduni na kudumisha 'corporate good governance'
   
Loading...