Vituo viwili vya Mafuta Dodoma vyafungiwa kwa Miezi 6

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kuvifungia vituo vingine viwili kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kuhodhi mafuta kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.

Vituo vilivyofungiwa ni kituo cha Kipenda Roho Investment kilichopo Soya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma pamoja na kituo cha Oilcom kilichopo Soya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo amesema uamuzi huo umefanywa baada baada ya kupitia utetezi wao katika kikao kilichofanyika Oktoba 09, mwaka huu na kujiridhisha kuhusika na kitendo hicho.

“Kwa uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi, hadi sasa utakuwa umegusa vituo tisa (9) na bado uchunguzi unaendelea kwa vituo vingine,” amesema.

------

Kwa mujibu wa Sheria ya Petroli, Sura Na 392, EWURA ina jukumu
la kuhakikisha upatikanaji wa mafuta wakati wote na katika maeneo yote nchini. Hata hivyo, kuanzia mwezi Julai kumekuwepo na matukio kwa baadhi maeneo hasa pembezoni mwa nchi kukosa mafuta hasa kipindi bei zinapoelekea kubadilishwa na kusababisha kuwa na usumbufu
mkubwa kwa wananchi na madhara ya kiuchumi.

2. SABABU ZA UPUNGUFU WA MAFUTA BAADHI YA MIKOA
Pamoja na mafuta kuwepo nchini, changamoto ya upungufu wa mafuta
katika maeneo mbalimbali ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta kwa makusudi kabisa kuamua kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya kibiashara ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za mafuta kinyume cha sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.

3. HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Kutokana na hali hiyo, EWURA imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwemo kuvifungia baadhi ya vituo vilivyothibitika kuficha mafuta kinyume na kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini.

Hadi tarehe 29 Septemba 2023, EWURA ilikuwa imevifungia vituo saba(07) kwa miezi 6 kwa makosa ya kuhodhi mafuta kinyume na sheria.

Kama tulivyoeleza katika mkutano na waandishi wa Habari tarehe 29/09/2023 jijini Dodoma, EWURA itaendelea na uchunguzi wa vituo vingine zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa ya kuwasilisha utetezi wao

Baada kupitia utetezi wao, katika kikao cha tarehe 9 Oktoba 2023 (jana);
Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilijiridhisha pasipo shaka kuwa vituo vingine viwili vilitenda kosa la kuhodhi mafuta kati ya mwezi Julai na Agosti 2023 na hivyo kuamua vifungwe kwa kipindi cha miezi 6. Vituo hivyo ni:-

(a) Kituo cha Kipenda Roho Investment kilichopo Soya, Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma

(b) Kituo cha Oilcom kilichopo Soya, Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma Kwa uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi hadi sasa utakuwa umegusa vituo tisa (9) na bado uchunguzi unaendelea kwa vituo vingine.

EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote wa biashara ya mafuta nchini kuhakikisha wanaendesha biashara zao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo inayosimamia biashara ya mafuta nchini
EWURA inatoa ONYO kwa OMCs na wamiliki wa vituo vya mafuta, kuwa Serikali inafuatilia suala hili kwa karibu kupitia vyombo vyake mbalimbali na kuwa ikithibitika uvunjaji wa sheria na kanuni umetendeka HATUA KALI za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwamo kuwafutia leseni zao za biashara.
 
Wanafanyaje kazi kwa hearsay eti Wafanyabiashara wa Mafuta wanayaficha kwenye Malori kwa siku tano.

Hivi anajua Lori likitembea mwendo wa kawaida hadi Karagwe linachukua muda gani?

Wasitengeneze mazingira ya kutafuta rushwa.
 
Back
Top Bottom