Vituo vya mafuta Dar vyagoma!

nashangaa nchi yetu imegeuka zimbabwe!!!! we need to be dictator sometimes tufunge vituo vyote na kuwanyangana leseni wote wanaohusika!!!

Hata dictator Mugabe alintanyang'anya leseni ya ardhi, kupanga hadi bei za vyakula, gas, etc. na kuifanya zimbabwe iwe kama ilivyo sasa. Udictator hasa hasa ktk kuendesha uchumi si suluhisho.
 
EWURA acheni uzembe, bei sio inabadilishwa kila wiki kufuatia average price ya Brent Crude, bei ya sasa hivi ni contract za Feb karibu na March.

Chukueni bei ya mafuta iliyotumika meli zinapoingia nchini, na hiyo bei inabidi iwe maintained at least a month or at least 2 weeks (whatever time hiyo cargo mpaka iishe) na sio kukurupuka kila week na bei mpya.
 
TPDC iuze mafuta kuondoa kiburi cha wafanyabiashara
Stella Nyemenohi
Daily News; Tuesday,January 13, 2009 @20:00​

“NI nani anayewapa kiburi hawa wafanyabiashara ya mafuta?” Hili ni swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza hususani baada ya kuamriwa na Serikali kushusha bei ya mafuta, lakini wakakaidi kutekeleza hilo haraka. Kupanda au kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli, dizeli na hata ya taa, ni suala nyeti linalogusa ustawi wa watu wote nchini.

Tunashuhudia hivi sasa kila bidhaa na hata huduma, zimepanda huku kisingizio kikubwa kikiwa ni kupanda kwa bei ya mafuta katika Soko la Dunia. Lakini baadaye, Mungu akajaalia bei ya mafuta katika soko hilo ikashuka. Watanzania tukatarajia wachuuzi wa mafuta wangeshusha bei haraka sana. Lakini mambo yakawa kinyume.


Badala yake, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikabidi iingilie kati. Mvutano ukajitokeza baina ya wafanyabiashara na Serikali juu ya kushusha bei ya bidhaa hiyo.

Wakati baadhi ya vituo viliendelea kukaidi, hivi karibuni limeibuka tatizo lingine la uhaba wa petroli. Hata hivyo, huu nauona ni ‘ujanja ujanja’ wa wafanyabiashara.

Ingawa baadhi ya wamiliki wa vituo vinavyouza mafuta wamekanusha kuhusika na vitendo hivyo, lakini hawana budi kuhukumiwa hivyo, kutokana na jinsi walivyoibishia Serikali kupunguza bei na sasa wanavyosababisha uhaba wa mafuta. Upo uwezekano wa wafanyabiashara hao kuamua kudanganya kuwa petroli haipatikani, ili baadaye waiuze kwa bei ya juu zaidi.

Ukiangalia matukio hayo yote, yakiwamo ya kukaidi kushusha bei ya mafuta na hili la kuadimika kwa petroli, inashawishi kuichagiza Serikali ikamilishe haraka mchakato wa kuliwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC ) kufanya biashara ya mafuta na pia uanzishaji na usimamizi wa hifadhi ya mafuta ya akiba. Inafahamika wazi, kwamba TPDC lilianzishwa Mei 30, 1969 chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969.

Majukumu ya msingi yalikuwa ni kutafuta mafuta na gesi, kuzalisha, kusafisha mafuta ghafi, kuhifadhi, kusambaza na kuuza petroli. Hata hivyo, baada ya kuingia katika mfumo wa biashara huria, Shirika hilo lilijiondoa katika uuzaji mafuta. Lakini ni kwa bahati nzuri, hivi sasa Serikali imeamua kuiruhusu tena TPDC kuingia katika uagizaji na kuleta mafuta kwa wingi nchini.

Kama ambavyo tamko la Serikali lilivyo, panahitajika ushindani katika biashara ya mafuta. Hii ni njia pekee ya kuleta changamoto ikizingatiwa, kwamba hapo awali, taarifa zinaonyesha kwamba shirika hili la Serikali lilikuwa likifanya kazi hiyo kwa ufanisi.


Lakini pia, tunaambiwa kwamba Serikali kupitia TPDC imeamua kuanzisha akiba ya mafuta nchini ili kuhakikisha kwamba pale panapotokea matatizo, basi nchi iwe haina matatizo ya mafuta.

Hivi karibuni, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwamba mchakato wa kuanzisha akiba ya mafuta na TPDC kufanya biashara ya mafuta, unaendelea.

Ninashauri mchakato huo uendeshwe haraka, kwani ndiyo itakuwa ‘fimbo’ kwa wafanyabiashara wababe na wenye kiburi wanaojiona kwamba bila wao, malighafi hiyo muhimu haiwezekani kupatikana nchini.

Inaeleweka wazi, kwamba umuhimu wa hifadhi ya mafuta ni kupunguza athari za uhaba wa mafuta kwenye uchumi pale mfumo wa upatikanaji unapokumbwa na matatizo kama vile majanga, vita au ubabe kama huu wa wafanyabiashara tunaoushuhudia sasa.

Kama kutakuwa na hifadhi ya mafuta inayosimamiwa na Shirika la Serikali, hatua hiyo itapunguza makali ya bei kwenye soko la ndani hasa kutokana na mfumuko wa ghafla wa bei katika Soko la Dunia.

Ninafahamu wazi kwamba ipo Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008 iliyopitishwa bungeni Aprili mwaka jana yenye uwezo wa kuwabana wafanyabiashara. Ni sheria hiyo ndiyo iliyoweka bayana wajibu na kazi za Ewura katika kudhibiti biashara ya mafuta.

Lakini pia hakuna ubishi, kwamba hatua ya TPDC kuingia katika biashara, itawakinga walaji dhidi ya wafanyabiashara wababe wanaotumia soko huria kama kigezo cha kukiuka sheria na kuwanyanyasa watumiaji mafuta.
 
Nilishalisema hili kwenye mada fulani. Wengi walitubishia na kusema serikali iache hiyo biashara. Nikasema kuwa kama nchi kuna huduma lazima ziwe mikononi wa Serikali. Hizo ni Elimu, Afya, Maji na Energy. Watu binafsi wasaidie tu. Wengine walituona tumepitwa na wakati. Nchi gani inayoweka mambo ya energy mikononi mwa watu binafsi?
Ntaicheki hiyo makala ...
 
Nilishalisema hili kwenye mada fulani. Wengi walitubishia na kusema serikali iache hiyo biashara. Nikasema kuwa kama nchi kuna huduma lazima ziwe mikononi wa Serikali. Hizo ni Elimu, Afya, Maji na Energy. Watu binafsi wasaidie tu. Wengine walituona tumepitwa na wakati. Nchi gani inayoweka mambo ya energy mikononi mwa watu binafsi?
Ntaicheki hiyo makala ...

Huwa wanakurupuka tu na sera bila kutathmini athari za sera hizo. Hivyo vyote ulivyovitaja hapo juu kamwe havistahili kuachiwa watu binafsi wavisimamie.
 
Huwa wanakurupuka tu na sera bila kutathmini athari za sera hizo. Hivyo vyote ulivyovitaja hapo juu kamwe havistahili kuachiwa watu binafsi wavisimamie.

Hapa ndo huwa nashindwa kuelewa, hivi tuna wataalam kweli?
na kama wapo basi watakuwa wataalam uchwara, na kama si uchwara
ni wapuuzi wanaoshindwa kutumia taaluma zao kunufaisha wananchi.

kama kungekuwa na umakini wakutosha upuuzi unaotokea hivisasa
wa wafanyabiashara wa mafuta kufanya mgomo baridi usingetokea.

Na hii yote ni ile kukosa uzalendo.....
 
Hapa ndo huwa nashindwa kuelewa, hivi tuna wataalam kweli?
na kama wapo basi watakuwa wataalam uchwara, na kama si uchwara
ni wapuuzi wanaoshindwa kutumia taaluma zao kunufaisha wananchi.

kama kungekuwa na umakini wakutosha upuuzi unaotokea hivisasa
wa wafanyabiashara wa mafuta kufanya mgomo baridi usingetokea.

Na hii yote ni ile kukosa uzalendo.....

Kwa ufahamu wangu TPDC hatuna wataalamu wa mafuta. Tuna watu wajanjawajanja tu pale. Watu wa maarifa-maarifa. Wataalam wa mafuta walikuwa TIPPER na walitelekezwa baada ya TIPPER kufungwa.

Suala la jingine la msingi ni kwamba TPDC hawana facilities za kuhifadhi mafuta ya akiba. Kitaalamu, huwezi kuhifadhi mafuta yaliyosafishwa "on the ground". TIPPER walikuwa wanahifadhi mafuta ghafi "on the ground". So, the idea that TPDC should maintain national oil reserve is far from materializing and corruption will not allow for any significant success. TPDC involvement in petroleum business is extremely susceptible to corruptions and thence underperformance. The long-lasting solution will be to resuscitate our refinery plant at Kigamboni. By doing that we will be importing crude oil and the only importer will be the refinery. All other players will be required to queue at the refinery. In that way, it'll be far easier to regulate the petroleum business.
 
Wachangiaji na MODS, nafikiri mmefanya kosa kuichanganya hii makala kwenye vituo vya mafuta. Naomba muichanganye na hii makala chini.
Tulishawahi kuliongelea hili na watu kama KOBA wakawa wanapinga vibaya sana. Ukiiunga hapa na kuipa kichwa kipya, italeta mtiririko mzuri.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/15600-tanzanians-pay-much-more-power-2.html

....hii sio free market failure ila ni sabotage tuu ya hawa walafi,dawa ni kuwakomesha kwa sheria zilizopo na hawatarudia tena,kumbuka unapopewa licence to operate oil company inakuja na legal obligations zake,ndio maana sio kila mtu anaweza kupewa hiyo licence hata kama una pesa, ni privilege tuu na inaweza kuchukuliwa anytime ukishindwa operations,sio kwa sababu una hiyo licence basi unaweza kufunga na kufungua pump anytime ukitaka na usifikiri free market ina maana unaweza kujipangia bei yeyote unayotaka,na huwezi kusema huuzi mafuta kwa ajiri stock imekwisha bila sababu zinazoeleweka au uzembe tuu,bei ya mafuta haitoki mbinguni na hata Tanzania kuna legal chanel za kupandisha na kushusha bei na lazima uzifuate na ziko clear kwa kila mtu anayeomba hiyo licence,ndio maana EWURA wameweza kuja na hiyo bei,kisheria ukiomba licence ya kuuza mafuta lazima uuze katika capacity uliyoomba...hii issue ni lazyness tuu ya utawala uliopo na oil moperator wanaojiona wako above everything na wanaamini serikali haiwezi kuwafanya kitu kwa sababu wamezoeshwa hivyo,ila nakuhakikishia kama serikali inafanya kazi huu upuuzi ni wa kumaliza kwa dakika mbili na watu hapa lazima wafikishwe mahakamani na licence lazima ziwe revoked...hakuna market failure hapo ni uzembe na ulafi tuu!
 
oil moperator wanaojiona wako above everything na wanaamini serikali haiwezi kuwafanya kitu kwa sababu wamezoeshwa hivyo,ila nakuhakikishia kama serikali inafanya kazi huu upuuzi ni wa kumaliza kwa dakika mbili na watu hapa lazima wafikishwe mahakamani na licence lazima ziwe revoked...hakuna market failure hapo ni uzembe na ulafi tuu!

- Tupo wote hapa mkuu Koba.
 
- Tupo wote hapa mkuu Koba.

Right. Unaweza ku-revoke licenses kama una njia mbadala ya kuingiza mafuta nchini. Kama Serikali ita-revoke licenses za makampuni yote au baadhi, unafikiri ni nini kitatokea? I think, there's no single current player with the capacity to supply for the entire country. BP? Oil Com? The bottom line is our Government is not prepared to implement what you are proposing. What do you think?
 
Right. Unaweza ku-revoke licenses kama una njia mbadala ya kuingiza mafuta nchini. Kama Serikali ita-revoke licenses za makampuni yote au baadhi, unafikiri ni nini kitatokea? I think, there's no single current player with the capacity to supply for the entire country. BP? Oil Com? The bottom line is our Government is not prepared to implement what you are proposing. What do you think?

- Serikali inaweza fanya anything inachotaka kwa faida ya wananchi na ikawezekana, tatizo ni viongozi wetu wengi wame-invest personally kwenye mafuta, ndio maana hapa kuna kusua sua, serikali yetu inaweza fukuza makampuni yote tuliyoyano sasa hivi na kutoa zabuni kwa mengine mapya na kusiwe na tatizo lolote,

- Wameleta haya makampuni uchwara, wame-invest hela zao binafsi huko ndio maana wamezuia competition sasa wa kulipa ni sisi wananchi, I bet you magari yote ya viongozi wa serikali hayakuwa na tatizo la mafuta, tatizo langu mimi ni kamati ya bunge inayo-deal na mafuta nchini wako wapi? Maana hili ni la jurisdiction yao sasa ungetegemea kuwasikia wakilalama, lakini wapi!
 
....hii sio free market failure ila ni sabotage tuu ya hawa walafi,dawa ni kuwakomesha kwa sheria zilizopo na hawatarudia tena,kumbuka unapopewa licence to operate oil company inakuja na legal obligations zake,ndio maana sio kila mtu anaweza kupewa hiyo licence hata kama una pesa, ni privilege tuu na inaweza kuchukuliwa anytime ukishindwa operations,sio kwa sababu una hiyo licence basi unaweza kufunga na kufungua pump anytime ukitaka na usifikiri free market ina maana unaweza kujipangia bei yeyote unayotaka,na huwezi kusema huuzi mafuta kwa ajiri stock imekwisha bila sababu zinazoeleweka au uzembe tuu,bei ya mafuta haitoki mbinguni na hata Tanzania kuna legal chanel za kupandisha na kushusha bei na lazima uzifuate na ziko clear kwa kila mtu anayeomba hiyo licence,ndio maana EWURA wameweza kuja na hiyo bei,kisheria ukiomba licence ya kuuza mafuta lazima uuze katika capacity uliyoomba...hii issue ni lazyness tuu ya utawala uliopo na oil moperator wanaojiona wako above everything na wanaamini serikali haiwezi kuwafanya kitu kwa sababu wamezoeshwa hivyo,ila nakuhakikishia kama serikali inafanya kazi huu upuuzi ni wa kumaliza kwa dakika mbili na watu hapa lazima wafikishwe mahakamani na licence lazima ziwe revoked...hakuna market failure hapo ni uzembe na ulafi tuu!

Koba, ukinyanga vibali uwarudishe Tz Petrolium au ulete wakina GAPCO wengine? Hapa hukusema vizuri. Sisi haya tuliyajua zamani na tukajua siku moja yatakuja fumuka.
Nimekuwa nafuatilia ugomvi wa Mrusi na jirani zake. Mrusi hataki uwekeze kitu kwake, ila yeye sasa hivi yuko busy kujenga au kununua petro-station nyingiii nchi za ulaya na kuandika LUK-OIL. Ujeruman wanasema karibu 1/3 ya hizo filing station ni zake. Hilo bado wanambeba kwa shida shida. Ila ugomvi wa sasa ndiyo hilo linalotokea Tanzania. Mrusi anataka ku-take contol ya mafuta na gas yote na mwisho yeye kuuza ndani ya Ukraine. Yaani Ukraine wasiwe na kitu hata kidogo zaidi ya kupata kodi. Hili jamaa ndiyo hawalitaki. Sasa hivi Warusi kwa kutumia gia ya Ukraine inaiba Gas, wameshapeleka watu wao kuanza ku-contol pamoja na watu wa EU. Ukraine kashashtukia mchezo na kafunga tape za Mrusi. Ingelikuwa Tanzania tungelisema free market. Ila kila nchi inayoelewa energy ni nini, hawawezi kuruhusu hilo.
Viongozi wetu wanapenda sana kukimbia majukumu. Ingekuwa hii kitu iko chini ya serikali, basi tungelijua kama kweli hamna mafuta au lahh. Hakuna shirika au kampuni inayofanya biashara ya mafuta na kupata hasara. Hii kitu irudishwe na MILELE ibaki chini ya SERIKALI.
 
Wabunge:Wauza mafuta wafutiwe leseni
WASEMA NI WAHUJUMU WA UCHUMI
Festo Polea

WAKATI tatizo la upungufu wa mafuta likionekana kutopata ufumbuzi, wabunge wameitaka serikali kuchukua hatua kali, ikiwa ni pamoja na kuwanyang'anya leseni wamiliki wa vituo vya mafuta waliodiriki kuficha nishati hiyo muhimu na kusababisha usumbufu mkubwa.

Katika hali isiyo ya kawaida, vituo vingi vya mafuta vilikuwa havina mafuta aina ya petroli kwa takriban siku nne, ikiwa ni siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta (Ewura) kutangaza bei mpya za bidhaa hiyo, ambayo ilipingwa vikali na wauzaji.

Vituo vingi vilikuwa vimebandika bei ya mafuta iliyotangazwa na Ewura, lakini ni dizeli pekee iliyopatikana katika vituo hivyo na kusababisha misululu mirefu kwenye vituo vichache vilivyokuwa vikiuza mafuta.

Hali hiyo iliifanya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kushangazwa na jinsi wafanyabiashara hao walivyoamua kuonyesha kiburi na kuisumbua serikali inayowaongoza kwa kufanya mgomo baridi.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wajumbe wa kamati hiyo waliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali inatakiwa kuchukua jukumu la juu kwa kuwa wafanyabiashara hao hawana huruma na uchumi wa nchi.

Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alisema wauzaji hao wanastahili kuitwa wezi na mafisadi kwa kuwa wamejipatia fedha nyingi kutokana na kuficha mafuta na baadaye kuyauza kwa bei ya juu katika siku hizo mbili, tofauti na ilivyokusudiwa.

"Wauzaji wa mafuta ni wezi na mafisadi, angalia leo serikali inafanya jitihada za kushusha bei wao wanaficha mafuta... wana sababu gani ya kuendelea kuwepo... wafutiwe tu leseni zao hawana faida kwa taifa zaidi ya kuuua uchumi," alisema Lembeli.

Lembeli aliitaka serikali kufanya jitihada za kupata wafanyabiashara wazalendo kujitokeza katika umiliki na uendeshaji wa biashara hiyo ili kusaidia ufichaji wa mafuta kama huo usiendelee kujitokeza.

"Serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa sababu ndiyo iliyotengeneza mazingira kwa wauzaji hao kuwa na kauli ya kujipangia watakavyo, kitu ambacho ni hatari kwa uchumi wa nchi," alisema Lembeli.

Mbunge wa Viti Maalum (CUF, Tabora), Magdalena Sakaya alisema ufichaji wa mafuta uliofanywa na wafanyabiashara hao unatokana na jeuri waliyonayo kwa serikali.

"Kuficha mafuta ni hujuma kwa uchumi, taifa na kwa wanajamii wote walio katika nchi hiyo kwani hutegemea mafuta, hivyo katika harakati za kuokoa hali hiyo, ni muhimu kufungia vituo vyote vinavyoficha mafuta na kuwapokonya leseni wamiliki wa vituo hivyo," alisema Sakaya.

"Hawa wafanyabisahara ni wahujumu wa nchi kwa kuwa katika biashara wanayoifanya wanataka kupata faida ya asilimia 100 na kuacha nchi tupu," alisema Sakaya.

Mbunge wa Nzega, Lukas Seleli alisema tatizo la kukosekana kwa mafuta linatokana na serikali kutojua kiwango kamili cha mafuta yanayoingizwa na kubaki katika akiba iliyobaki kwa ajili ya siku zijazo.

"Serikali haipo makini na masuala hayo muhimu kwani hadi leo Ewura, ambacho ndiyo chombo cha serikali katika kushughulikia mafuta, haina mitandao katika mikoa... walikimbilia biashara huria ndio maana inawapa shida," alisema.

"Hivi mafuta wanasema hawana kweli inaingia akilini wameuza wapi wakati kulikuwa na akiba ya siku nyingi... ndiyo maana nasema serikali haijawa makini katika mambo hayo," alisema Seleli ambaye aliitaka serikali kuchunguza kwa kina kama mafuta hayo yapo ama hakuna ndipo wafanye utaratibu wa kufungia.

Mbunge wa Kongwa, Job Ndungai alisema endapo serikali inataka kumaliza tatizo hilo, haina budi kuiwezeshe kampuni ya TPDF iweze kuingiza mafuta mengi na kuyauza kwa bei nafuu.

Wakati huo huo waandishi Tumsifu Sanga na James Magai wanaripoti kuwa makampuni ya mafuta yanatarajia kuingiza shehena kubwa mafuta nchini ambayo itaondoa uhaba wa mafuta ulioikumba nchi kwa takribani siku nne sasa.

Akijibu maswali ya waandishi wa habri jana kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Ewura, mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya uagizaji wa mafuta nchini (Taomac), Salum Bisarara alisema tayari kuna meli za mafuta ambazo zitaingia na kushusha mafuta bandarini wakati wowote.

Bisarara alisema kampuni ya mafuta ya Gapco imeingiza nchini lita milioni 10 na kampuni ya BP inatarajia kuingiza shehena ya mafuta tani 1,000 ifikapo Januari 18, wakati Januari 25 Oryx inatarajia kuingiza tani 8,000 pamoja na GP ambayo inatarajia kuingiza tani 3,000 ambapo zote kwa jumla zitakuwa zimeshusha tani milioni .

Bisarara alitumia nafasi hiyo kukanusha taarifa kuwa wafanyabiashara wa mafuta wanaihujumu serikali kwa kugoma kuuza mafuta kama njia ya kupinga bei elekezi zinazotolewa na Ewura kwa madai kuwa wanapata hasara.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Ewura, Anastas Mbawala, akielezea hali halisi ya uhaba wa mafuta ulioikumba nchi tangu Jumamosi, alisema hali hiyo imetokana na makampuni ya mafuta kuogopa kuagiza mafuta mengi wakihofia kupata hasara kufuatia hatua ya Ewura kutangaza bei elekezi kila wiki.

"Wenye vituo vya mafuta wamekuwa na hisia kuwa Ewura itakapobadilisha bei inaweza kushuka na hivyo kupata hasara. Hivyo kuna wale ambao waliacha kufanya manunuzi makubwa ili kutosheleza siku za mwisho wa wiki pamoja na sikukuu ya Mapinduzi," alifafanua Mbawala.

Hata hivyo Mbawala alisema walipofanya ukaguzi katika katika vituo na maghala mbalimbali ya makampuni ya mafuta walibaini kuwa kulikuwa na mafuta ya kutosha kwa matumizi ya matumizi ya siku 10.

Source: Mwananchi Read News
 
- Mkuu are you serious au unatania, serikali ipi hiyo? Hivi hukuwepo enzi za kutokuwa na mafuta weekend? Unataka turudi tena kuleeeeee! Woooi!

Mkuu niko serious,
Naona hiyo njia mpya nayo haisaidii. Na kama halitapatikana suluhisho la muda mrefu, basi hili litarudi tena.

Naona huu MUONO siko peke yangu:-

Mbunge wa Nzega, Lukas Seleli alisema tatizo la kukosekana kwa mafuta linatokana na serikali kutojua kiwango kamili cha mafuta yanayoingizwa na kubaki katika akiba iliyobaki kwa ajili ya siku zijazo.

"Serikali haipo makini na masuala hayo muhimu kwani hadi leo Ewura, ambacho ndiyo chombo cha serikali katika kushughulikia mafuta, haina mitandao katika mikoa... walikimbilia biashara huria ndio maana inawapa shida," alisema.

"Hivi mafuta wanasema hawana kweli inaingia akilini wameuza wapi wakati kulikuwa na akiba ya siku nyingi... ndiyo maana nasema serikali haijawa makini katika mambo hayo," alisema Seleli ambaye aliitaka serikali kuchunguza kwa kina kama mafuta hayo yapo ama hakuna ndipo wafanye utaratibu wa kufungia.

Mbunge wa Kongwa, Job Ndungai alisema endapo serikali inataka kumaliza tatizo hilo, haina budi kuiwezeshe kampuni ya TPDF iweze kuingiza mafuta
mengi na kuyauza kwa bei nafuu.
 
Serikali imeonesha meno ya maneno, je, tutaona pia meno ya misuli.

Yote tisa, kumi ninaamini tulifanya makosa kuachia uagizaji mafuta ufanywe na watu binafsi.

Aidha serikali ifanye kazi na watu wastaarabu kama GAPCO na ENGEN kwa kuingia ubia wa uagizaji na uhifadhi mafuta kwa muda mrefu. Katika ubia huo lazima serikali iwe na sauti juu ya kupanda au kushuka bei ya mafuta kulingana na gharama za ununuzi na usafirishaji mafuta zilizopo wakati huo!
 
- , tatizo ni viongozi wetu wengi wame-invest personally kwenye mafuta, ndio maana hapa kuna kusua sua,

- Wameleta haya makampuni uchwara, wame-invest hela zao binafsi huko ndio maana wamezuia competition sasa wa kulipa ni sisi wananchi, I bet you magari yote ya viongozi wa serikali hayakuwa na tatizo la mafuta,

Kumbe viongozi hawa hawa wa serikali, wanaweza kuunda kampuni na kuchukua mali za uma kuendesha mashirika hayohayo na yakaleta faida. Ila shirika hilohilo likiwa ni la serikali basi linakosa faida. Mkuu, sasa nikuulize wewe, ARE WE serious?

Now I can see the connection kwa nini makampuni haya ya mafuta yanachangia fedha nyingi sana wakati wa kampeni... kumbe ni zao wenyewe!!!!

Nashukuru umeiona hiyo connection.

- Mkuu are you serious au unatania, serikali ipi hiyo? Hivi hukuwepo enzi za kutokuwa na mafuta weekend? Unataka turudi tena kuleeeeee! Woooi!

FMes, ni hayohayo tu ya Tanesco. Wanalimaliza nguvu shirika, wanasema njia nzuri ni kubinafsisha. Wanaletwa akina Richmond na linalofuta linajulikana. Huo ni mwanzo tu, wakitaka basi watakuwa wakorofi zaidi.
Hakuna shirika la mafuta linaweza kufanya kazi bila ufanisi. Kama walikuwa wanasababisha weekend kukosa mafuta, basi walikuwa wanafanya kwa makusudi na ndiyo ilikuwa mipango. Mie sisemi Petro station ziwe za serikali ila IMPORT ya mafuta kutoka nje, asilimia 60 ifanywe na serikali na hao wengine wafaidi hiyo 40%. Taztizo hapa ni kuwa huko kwenye Import unamkuta YONA na Mkapa ambaye anatakiwa kumuwajibisha ni MSHIKAJI wake na hadi wamefungua kampuni moja. Ndiyo maana nasema, kama ikisemwa, iwe isiwe hiyo ni kazi ya serikali, hakuna atakayefanya UHUJUMU ili kesho yeye hiyo kazi aifanye kwa faida kubwa na kuanza kutuonyesha msuli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom