Shukrani Elisha: Utitiri wa vituo vya Mafuta karibu na Makazi ya watu jijini Dar es salaam sio sawa kwa usalama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Karibu kufuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 24, 2023 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 12.



Mbunge Prof. Shukrani Elisha ameonesha masikitiko kwa Ofisi ya Mkamu wa Rais, Mazingira na Muungano kushindwa kudhibiti utitiri wa vituo vya Mafuta jijini Dar es salaam.

Amesema vituo hivi vimekuwa vingi sana kiasi cha kuhatarisha usalama wa maisha ya watu ambao baadhi wamekuwa wanajenga nyumba pembeni yake.

"Sasa hivi maeneo ya mjini hasa katika jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani utagundua kuna vituo vya mafuta vinajengwa katika makazi ya watu kila baada ya mita 100, na wakati mwingine vituo hivi vya mafuta vipo upande wa kushoto na kulia wa barabara ya lami. Sasa unajaribu kujiuliza Mhe. Naibu Spika, Kwanini hali hii ipo hivyo?"

Ameongeza, "Hivi hatuoni hatari ya kwamba vituo vya mafuta vipo katika makazi ya watu na wakati mwingine havina hata uzio. Hivi ikitokea moto au ajali, tutasemeaje?"

Pia, ameishauri Serikali kuafuatilia viwanda vilivyopo karibu na makazi ya watu akitolea mfano vile vilivyopo Kibangu Makuburi ambavyo hutoa moshi mzito na kutitririsha maji machafu.

Naye Mbunge wa Magomeni, Mwanakhamis Kassim Said amesisitiza umuhimu wa Muungano na kutaka Watanzania kuuenzi kwa kuwa waasisi waliujenga kwa kuchanganya udongo, lakini sasa muungano huu umejengwa kwa muunganiko wa damu.

Amesema "Kwakweli sisi sasa hivi ni ndugu, tumechanganya damu. Hatuwezi kutengana, hatuwezi kugombana, mambo mengine madogo madogo yatatokea hayo ni mambo ya kibinadamu"

Amempongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayofanya kuusimamia muungano huo pamoja na kutatua kero nyingi zilizokuwa zinaukabili. Amewataka Watanzania kuwa wamoja.

Pia, ameiomba Serikali kutatua changamoto zinazokabili wanawake wajasiriamali kwenye bandari ya Dar es salaam kwani wamekuwa wanasumbuliwa, kudharirishwa na kuteswa.
 
Bunge limekosa mvuto, kufungia fungia Bunge imewagharamisha sana aisee.
 
Back
Top Bottom