Vituko vya mayweather

Duuh sasa kma huyu mshamba je wa kutoka ndwele huko kijijini kwenu ataitwaje
 
Huyu jamaa investments zake nyingi ni zile ambazo huisha
 
sijaona ushamba wake ila wasomaji wameshindwa kuheshimu hisia binafsi mtu ashindapo game
 
Kuna crip moja jamaa anasoma,duu kama mtoto wa darasa 1 anavyosoma,Baba yake Mayweather sr analalamika matumizi yasiyo ya maana ya mwanae,anasema akiacha ngumi na asipobadilika kimatumizi atafirisika....ana kipaji lakini athari za kukosa mapenzi na malezi mazuri utotoni yanamwathiri...
 

Hivi pamoja na kuongea kiswahili, kuna watanzania wasiojua kukisoma kiswahili?
 

wasiojua kusoma na kuandika pia wamejaa marekani
 
Jay-z na 50 Cent na wao wametoka kwenye mazingira magumu pia. Ila kuchukua Dola zao inabidi ufanye kazi.

Hili Jinga linatawanya ovyo. Eti ana ndege yake. Tulishawaona akina Pippen na ndege zao, leo wako hoi.

Kwa nini usikodishe au kuwa na ndege za ushirika? Sijui kama Jordan bado ana ndege yake.

Kununua ndege si ghali ila kuifanyia Check-Up na kupata vibali vya kuruka kila mwaka, hapo ndiyo hela zinakwisha.

 

Kweli kabisa.

Si kila bilionea ana ndege, wengi wanapanda hizi commercial ones. Jamaa hajui jinsi ya kumanage kipato chake. Yetu macho, ataishi kwa historia muda si mrefu.

Wapi kina mike tyson?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…