Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Vituko vya Maisha ya Boarding, Tukumbushane Tuliosoma Huko

Enzi za skuli tumefanya utukutu mwingi sana. Sitasahau siku nimepenya dirisha la jikoni tukaiba pora (uji) kisha masufuria yakaoshwa usiku huo huo na kujazwa maji. Mpishi alikua mzee mmoja mhuni siku hiyo sijui alipata mama wapi kaenda kulala nayo huko mtaani. Hii siku naikumbuka na huwa nacheka sana. Wana tuliopiga hili tukio mkipita hapa mtakumbuka. [emoji28][emoji28][emoji28] Hapo form two.

Matokeo ya pre national yametoka mabovu mbaya ikabidi tuvunje kioo cha notice board tukachana matokeo.

Nakumbuka tuliwahi kuvamia canteen siku imetokea vurugu kwasababu mwenye canteen alikuwa anauza vitu ghali tukafanya kumkomoa. Wa dukani tulimwacha kwasababu alikua fair.

Mlinzi mnoko siku hiyo alipigwa vile vitofa vyakuchoma akakimbia lindo akakimbilia maporini.

Nakumbuka kuna jamaa alikuwa snitch anatusnitch kwa walimu siku moja umeme ulikatika jamaa wakaingia porini kuchuma upupu asee jamaa yupo bed kwake alichapwa upupu wa uso alivimba balaa. Sitaji majina maana kwenye kamati ya upupu nilikuwepo.

Nakumbuka machalii wa Dar walikuwa wanajiona wakishua sana mara blue band sijui Milo, Nido na mbwembwe basi machalii wa R tukawa tunaiba ma tranka yao tukishachukua kinachotufaa tunatupa jalala la shule.

Kuna day jamaa mmoja aliharisha kwenye chumba kimoja jirani na bweni asee tunaolala lile bweni wote tulishikishwa kile kinyesi na mwalimu wa discipline alikuwa mkali balaa (simtaji jina) [emoji28][emoji28]

Kipindi hiyo tunatoroka skuli kwenda sehemu fulani kula mihogo wengine kunywa banana na kuvuta bangi na fegi.

Matukio ni mengi sana nikiandika hapa naweza kujaza kitabu. Hapo ni o'level tu bado advance.

Clue: Manyigu na Madondola.. kama unajua hii utajua ni skuli gani na mwaka gani maana tuliacha legacy. Siku tunamaliza pepa uongozi wa shule ulipumua.
Manyigu madogo walivaa green. Waliiba halfcakes canteen. Wakamuibia mzee Jamaica uji wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Mzumbe sec,nikiwa kama DH committee (kamati ya bwalo) mzee pale skonga kila j2 ni pilau nyama mpaka leo hii,sasa mimi na wanakamati wenzangu ilikuwa lazima tuwahi bwaloni kutengeneza nyama choma,mpishi mkuu alitudekeza sana sitamsahau yule mzee,sasa kimbembe ilikuwa nikirudi Dom,mzee hupewi pumzi ni madongo hadi unajikuta unashiba mwenyew,
Utaitwa majina ya kifisadi mpaka msosi unakukinai.

Machalii ya MZ mnaboa mjue?.
Mkuu dash, nilikuwa Self reliance, kula salo sana, top layer, nimekaa fede sana, kwenda mongwe sana. Enzi za Njawa, [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale tulipopita Ndanda Boys High School kulikua na second master mnoko sana sasa ilikua ukienda kuchoma na kupiga bia ukimuina pale bar bas unawahi kumpa offer anatuliaa, maisha ya kucheza lizangati, kwenda kusomea mlimani, kusubiri watoto wa masasi girls na mtwara girls...Maisha yalikua kama chuo tofauti bumu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asalam Aleikhum

Katika Maisha ambayo siwezi kuyasahau ni maisha ya Boarding. Maisha ya Boarding noma aliimba Jay Mo, moja kati ya wasanii waasisi wa Bongo Flavor.

Maisha ya Boarding ni moja kati ya maisha matamu lakini pia yenye changamoto nyingi. Kuna matukio na vimbwanga ambavyo vinatia chachandu katika Maisha ya Boarding.

Kuanzia kuingia shule ukiwa form 1 ni burudani tosha. Kwanza tuliitwa majina mengi sana, nyoka, Salamanda, njuka, soksi ya mlinzi n.k

Tulipigishwa simu chooni, tulichapwa mikanda usiku hasa tulipowasnitch watesaji kwa walimu. Aisee tuliooingia form 2 tukawa eti ma MP, na sisi ndio wababe dhidi ya Form 1...hataree.

Maisha ya Boarding bhana, tulikula ada, home walipojua ikawa msala wengine ilibidi kipindi cha kuchukua cheti tutafute hela kwa udi na uvumba ili tukakomboe ada tuliyokula.

Nakumbuka kipindi tunajiandaa kwenda shule baada ya likizo tulikuwa tunanunua mafuta ya kupikia na dagaa na viungo, tunachemsha huo mchanganyiko na tukifika shule duh.. hatari, kijiko kimoja cha mafuta kwa bakuli moja la maharage, waombaji sasa, weeeeengi, nyama ilikuwa mpaka ng'ombe wa shule augue.

Siku ya wali wengine ndio tulikuwa tunaoga hasa wale Tuliosoma maeneo yenye baridi. Kuna wakati tulikula ugali na sukari, sukari ni mboga wakuu sio mnashanga tena tamu kweli. Tukiandikiana barua na masela wetu wa shule nyingine, lazima ndani ya bahasha tuambatanishe punje mbili tatu za wali, watajuaje huwa tunakula wali.

Ukipoteza sahani usiwaze, kwa wali au uji utatumia ndoo unayoogea, kwa ugali utabeba mkononi na maharage utaweka kwenye kikombe chako cha uji.

Kuna wakati tulikuwa tunaenda jikoni kuiba upper layer au top layer pale msosi unapokaribia kuiva. Upper layer ni yale mafuta yanayoelea juu ya maharage, ukichanganya na maharage utamu wake sio wa nchi hii.

Kuoga haikuwa lazima. Boarding wengi ndipo walioojifunza kupiga Punyeto, a.k.a Puli. Nakumbuka kuna siku washikaji waliifanya mashindano nani atatoa wazungu haraka na mshindi alipatikana.

Kwa wapenda soka kulikuwa hamna namna unaweza kukosa Mechi za UEFA au za ligi za usiku. Kutoroka lazima, tukirudi tuna fegi mfukoni tukifika Shuleni tunampa mlinzi inakuwa sio kesi. Ikiwa zamu ya mlinzi mnoko tunatumia mbinu za kijasusi kuingia na kutoka eneo la shule.

Maisha ya boarding tulilima, tulifyeka, tulicheza. Kulikuwa na wasongo na wanafeli, halafu kulikuwa na wasongo na wanafaulu. Kubaki bwenini wakati wenzako wapo class ilikuwa kawaida sana, ila ukikutwa na bwana Pepsi shauri yako, yaani ni msala. Ila sisi wazoefu hatukukamatwa.

Muda wa prep a.k.a prepo hatukwenda class, tulisubiri usiku wa manane mtu atuamshe ndio tukasome hii ilikuwa sana sana wakati wa mitihani, tuliita msuli pepa.

Dah siku ya kuondoka school baada ya mitihani ya kitaifa kuisha ilikuwa very sad day. Wa mbeya walikwenda, wa Dar walikwenda, wa Morogoro walikwenda, wa Dodoma, wa Arusha. Kweli boarding school inakutanisha watu kutoka kila kona ya nchi.

I bet waliosoma day schools hawakupata hii informal education katika shule walizosoma.

Waliosoma maisha boarding tiririka your experience.
Kuna huyo jamaa alikua anatokea Bukoba alikua comedian cjapata kuona, tukifungua shule alikua anakuja na madaftari tuu Mambo ya sabuni, dawa ya meno na mazaga yote anapata hukohuko shule, nakumbuka tukiwa form6 watu wa Arts walitaka kumpiga aliposema HKL50 nisawa na PCM mmoja
 
Nilisahau Shamba dress. Jamani ila kwa kweli tulisoma boarding za Kayumba we are strong than ever. Shida ya maji sasa acha kabisa. O level nilisoma Rugambwa girls yaani kule maji tulikuwa tunafuata kwenye kijito fulani hivi kina mawe makubwa kabisa. Halafu sasa kule vyoo vilikuwa vinaziba, kuzibua sasa. Imagine mavi yanajaa hadi yanatokezea kwenye pavements. O My God sitaki kukumbuka.Ila namkumbuka sana mpishi Kaka hansi na Samaki wa mama nelly, jongwe, blue band. Vyoo vya Ihungo vilikuwa vichafu balaa.
Haahaa Ulipo itaja IHUNGO BOYS HIGH SCHOOL
Nikamkumbuka
"IKEMEFUNA"
Haahaa Boyz wa IHUNGO walikuaga wanaishobokea rugambwa wonderful enough mpk namaliza six siijui rugambwa ilipo? Nili ishia ku onyeshwaga kilima kile sikuwai kwenda...na sketi Zao nyekundu
 
Tuliosoma kibaha boys a.k.a wazee wa kuku tujuane hapa,haya maisha yenu mnayosimulia hapa kwa siye wazee wa KSS tunaona kama tamthilia vile😂😂😂
 
hehehe huu uzi ni hatwarii...watu mlikuwa mmepinda asee
olevel
- kulala bwenini wakati wa vipindi hasa baada ya muda wa break
-Me na team yangu ilikuwa mwiko kusikiliza mwalimu au kuingia kipindi cha hesabu hasa baada ya kuingia form 2 eti kisa tulikuwa hatumpendi matron ambaye ndo alikuwa mwalim wa hesabu. basi akiingia tunatoka au kama hatutatoka basi tunalala fofofo.
- kumpiga form one kidogo nifukuzwee

alevel
-kutoroka kwenda disco pub alberto halafu kaka boni tunamhonga buku
-kuiba nyama kwenye sahani za watu siku ya wali nyama
-kwenda changbay kununua chips kuku kila siku jion (hata kama hakuna hela basi tutaenda tu hata tupoteze muda na kuwachokoza waalim na viranja) na hakuna wa kututaja
-kutoroka kwenda arusha jumapili na na siku ya shopping
-kudanganya michango ya uongo kwa mzazi ili tu nisile ugali maharagwe
-siku ya mwisho kabisa nikamuuzia dada teddy godoro langu zuriiiii baba alininunulia saba saba kwa elfu 15, kufika home godoro liko wapi nkasema waliiba
Ulisoma Mawenzi Secondary ⁉️
 
Kufuta stamp kwa sponji iliyolowanishwa kwenye maji yenye sabuni.Ule mchanganyiko wa vitunguu,dagaa na mafuta uliokaangwa na pilipili umenikumbusha mbali, prepo mwisho saa nne usiku, ila nakumbuka wakati wa national exams tulikuwa tunakesha kwenye store moja, Maisha ya boarding kwa kweli ila ilikuwa hapana aisee. Sitaki wanangu wayaishi. Ninatamani siku moja nikatembelee na wanangu shule nilizosoma na niwaonyeshe shamba, viwanja vyenye nyasi tulivyofeka. Maana wao shuleni kwao hizo kazi zinafanywa na wafanyakazi.
Kama sio Maswa girls basi itakuwa Msalato....
 
Nilikutana na mchizi wangu baraka anapenda kuangalia video si mchezo, ikawa ni kutoroka kila night hakuna cha prepo wala nini tunazama kibanda umiza.

Cheki movie mpaka ngoma 6 inawekwa pilau aseeh, siku moja ma njagu wakatuotea kibanda umiza tunacheki pilau wakatudaka watu kama 8.

Hapo tukilala kituoni ni msala skuli, kufukuzwa nje nje ilibidi tuwaambie ukweli sie wanafunzi tuwape mkwanja fulani watuachie wakakubali ikawa pona pona yetu.

Matukio ni mengi sana, niliweka wali kwenye tranka mjinga fulani akalitingisha juu chini chini juu daaa! nguo zilitapakaa wali si kidogo
Nilikutana na mchizi wangu baraka anapenda kuangalia video si mchezo, ikawa ni kutoroka kila night hakuna cha prepo wala nini tunazama kibanda umiza.

Cheki movie mpaka ngoma 6 inawekwa pilau aseeh, siku moja ma njagu wakatuotea kibanda umiza tunacheki pilau wakatudaka watu kama 8.

Hapo tukilala kituoni ni msala skuli, kufukuzwa nje nje ilibidi tuwaambie ukweli sie wanafunzi tuwape mkwanja fulani watuachie wakakubali ikawa pona pona yetu.

Matukio ni mengi sana, niliweka wali kwenye tranka mjinga fulani akalitingisha juu chini chini juu daaa! nguo zilitapakaa wali si kidogo
Ahahaaaaa
 
Kupiga simu chooni, kuvuta mjani, kugonja walimu wa kikeni waliokuwa wakija field, kuuza biskuti, kuvunja makontena ya vilaza, watu tulikuwa na funguo zaidi ya 500 hizi ni za kupampu makufuli, wakati tuko shule, tunamiliki shamba bondeni, la nyanya na miwa, kupiga walimu wanoko mida ya prep, kutoroka usiku tunaenda mlima zinaa, kulala ktk mabweni ya wasichana na wasichana kujichanganya ktk mabweni ya masela, kuingia class na vi-bom, kupiga simu chooni, disko vumbi, kuwekeana mafuta ya taa ktk chakula, kuchambia godoro, kulamba sahani baada ya kula, kupiga passpot size,

Njuka mnyonge alibanduliwa au kunyonya rungu, kufunga mawe ktk mataulo kisha taa inazimwa dakika tano, muda wa kufunzana adabu, hii kila siku saa tano usiku, kupakana losheni, au kuvunjiwa yai ukilala kisha wanasingiziwa vibwengo, kuuza magodoro ya walioingia darasani wiki dume, godoro linabadilishwa na sahani ya wali maharage, mchaka mchaka saa kumi za usiku kisha mnafuata maji ya kuoga chini ya mlima..na mwisho tukachoma shule moto kisa hawakutupikia wali wiki mbili mfululizo

Nilikuwa waziri wa chakula, kampani yangu walijaziwa kuliko maadui zetu, sisi chakula tulikuwa tukiweka katika ndoo ya lita 20 watu watano, tulikuwa wanafunzi 1200 lakini nyama inapikwa kilo kumi na tano tuu, hapo waziri wa msosi nachoma kilo moja na ikiiva najaza kisado, wengine wanakunywa supu...tulibadilishana wali kwa penzi....pamoja na yote, darasani tulikuwa vizuri... mvua ikinyesha wote tulitoka nje uchi tukioga...kutokana na utukutu niliokuwa nao, pesa ya matumizi nilipewa buku na panadol tu, lakini nikirudi rikizo nilikuwa na zaidi ya laki tatu...
😁😁😁 we jamaa ulikua zaidi ya jambazi
Kuna kijana wako atakuja kupita umu 😀
 
Kanawa sec 2002-2005 wazee WA kudondoa nawakumbuka Sana walikuwa wananuita kamotion Luzugumo filbert,mnaku obeid,mandazi masangu,gungulugwa lukulu,Eliza jijongo,nuru Abbas mbua namtafuta Sana hadi Leo nikimpata anakuwa mchepuko wangu😂😂😂😂
 
Sitamsahau jamaa mmoja mbabe tukirripoti shulen mwezi wa january anapita bweni la form one anasema form one wana neti mpya na mashuka mapya mimi sinunui chochote naenda kuchukua vyao daaaaa
 
Back
Top Bottom