Vituko ubadilishaji wa vitambulisho vya ukaazi Zanzibar

Waunguja na Wapemba nje ya Muungano sijui hata kama wataweza kuishi pamoja bila kuvurugana

Kuna hawa masheha wana ubaguzi wa hali ya juu sana dhidi ya Wapemba, na huu ubaguzi una baraka zote za Serikali

Mkuu tatizo sio waunguja na Wapemba, Tatizo ni CCM. CCM ndio wanaouendesha huo ubaguzi.
 
Ukifika unaambiwa wewe ulishahama hilo eneo rudi ulipohamia.
Dai barua kutoka kwa Huyo anayekukatalia na aandike kwa nini anakataa kuupdate kitambulisho chako
Naomba uwaambie na wengine ...baada ya hapo nitawaambia cha kufanya
Pls njoo PM
 
How...mfano mm nimejiandikisha kata ya Vingunguti ila kwa sasa nimehamia kata ya Buyuni ....uchaguzi ukifanyika narudi Vingunguti kupiga kura na hakuna anayenizuia na hata kqma vitambulisho vitabadilishwa nitaendelea kubadilishia kata ya Vingunguti na shughuli zangu zote za uchaguzi nitazifanyia hapo

Mkuu hao masheha wanagoma kabisa kutoa izo barua, Wanakimbia kabisa kwnye majumba yao hizo siku za uandikishwaji.
 
Dai barua kutoka kwa Huyo anayekukatalia na aandike kwa nini anakataa kuupdate kitambulisho chako
Naomba uwaambie na wengine ...baada ya hapo nitawaambia cha kufanya
Pls njoo PM
Akashtaki.wilayani...

Au watakuwa na figisu na huyo sheha.. .

Mbona wengi tu wanapewa hizo barua?

Mkuu tuambie ni sheha wa wapi huyo...
 
Mkuu hao masheha wanagoma kabisa kutoa izo barua, Wanakimbia kabisa kwnye majumba yao hizo siku za uandikishwaji.
Muhimu ni kila mmoja kwenda kwa wakati wake.....kama atakimbia maana Yake watakuwa wamehama majumbani mwao? Ok nendeni kwenye mabaraza au mahakamani ...waitwe waje waeleze kwa sababu gani wanawakatalia mahakamani au barazani wakitoa hukumu ombeni nakala ya hukumu....kisha tufanye yetu
 
Huyo sheha ni kwamba haingiriki kabisa, Mimi nilihama mji mmoja kwenda mwingine ndani ya unguja hii hii lakini nilipaswa kwenda na barua ya sheha,
Kupata barua kwa sheha ni ngumu Sana, kwanza anahisi unataka kitambulisho cha ukazi au unatafuta kazi au unataka kupata passport ya kusafiria....
Hii nchi wanaiharibu wenyewe, hakuna wa kumsingizia

CCM ndio wanaoiharibu usitafute mwengine.
 
Ukijibaguwa.....ukashtukiwa .utabaguliwa tu!

Sio wewe ubague halafu usibaguliwe.

Kuna mengi sana hawayasemi hapa!

ugomvi huku si mpemba na muunguja ...ni mpemba kumtomtaka mbara !

Hamna jengine..hayo mengine ni wanazuga tu!

Ndio maana hapakai sawa...

Kila mtu hapo anafanya lake ugenini!

Waunguja wamechoka wallah!

Acha ubaguzi mkuu. unajidhihirisha kabisa halafu eti unatupia lawama wengine.
 
Ok vizuri....but what if atabadilishia pale pale alipojiandikishia?
Mimi pia nimeona haina haja ya kwenda kufuata hio barua ilhali unaweza kwenda siku ya kufuata barua ndo ukajiandikisha.Wazanzibari bwana kazi kwelikweli
 
Zanzibar hivi sasa imo kwenye harakati za kubadilisha vitambulisho vya ukaazi. Vitambulisho hivi ni muhimu sana kwa Wazanzibari wakaazi, kwani ndio nyenzo kuu ya kuendesha shughuli za kijamii na kisiasa kule visiwani. Bila kuwa na kitambulisho hicho maisha yanakuwa vigumu kuyaendea.

Nimesema hivi kwa sababu bila kuwa na kitambulisho hicho hata safari za ndani, yaani kati ya Unguja na Dar es Salaam pamoja na zile za kati ya Unguja na Pemba inakuwa vigumu. Ni vigumu kwani ili kupata tiketi unatakiwa kuwa na kitambulisho ama cha ukaazi, uraia, cha kupigia kura au leseni ya udereva.

Vitambulisho vyote hivi kwanza kuvipata kwake kuna uhusuiano mkubwa na kitambulisho cha ukaazi, ukiachilia mbali hichi cha uraia.

Ni bahati mbaya kwamba ubadilishaji wa vitambulisho hivi umeingizwa siasa. Nasema hivi kwani matayarisho ya uchaguzi mkuu yameanza chini kwa chini kwa kuweka miundo mbinu ya zoezi hilo. Hii ni pamoja na matayarisho ya uandikishaji wapiga kura. Utaratibu uliowekwa wa kubadilisha vitambulisho hivyo ni kwamba wahusika wanabadilisha pale walipovipatia mara kwanza (vikongwe vinavyobadilishwa).

Inapotokea mtu amehama anatakiwa achukue barua ya kule alikotoka na kuipeleka alikohamia ili sasa apewe barua ya kwenda kubadilisha kitambulisho. Katika hili ndio wenyewe wanapocheza mchezo huu wa kisiasa.

Masheha ambao ndio wanaotoa ruhusa ya kuandikishwa/kutokuandikishwa, wameweka daftari lao lenye orodha ya watu wanaotaka waandikishwe. Sheha anapokuwa na wasiwasi tu kwamba mtu sio MWENZAO anakwambia humo kwenye orodha yako na hivyo swala la kubadilishiwa kitambulisho chako ndio linaishia hapo.

Lakini ikumbukwe pia kwamba kama kitambulisho hakitobadilishwa ndio kusema kwamba mhusika hatopiga kura, hatopata tiketi ya kusafiria kati sehemu moja na nyengine kutoka visiwani, hatopata hata nafasi ya kuandikisha cheti cha kuzaliwa mtoto wake akiwa naye na mambo mengine mengi.

HII NDIO ZANZIBAR
Huko visiwani kuna mambo ya kilofà sana
 
Mkuu hili linafanyika ili usipate kuandikishwa kwani sheha atakwambia rudi huko ulikotoka na ukirudi huko unaambiwa nenda ulikohamia. Mradi usiandikwe tu
Mimi nakuleww mambo ya unguja na pemaba nayaelewa vizuri yaani binadamu wake hawapendani mpaka kufa.
 
Back
Top Bottom