Vituko ubadilishaji wa vitambulisho vya ukaazi Zanzibar

Hapa nilitaka tu kuongeza baadhi ya vitambulisho ambavyo vinakufanya upate ticket ya kusafiria wala sikuwa na nia nyingine tofauti na hiyo mkuu

Jamani mi sjaona hata umuimu wa kutumia ivyo vitambulisho ktk shul za safar za ndani uko zenj.

Pia mwenye kujua naombeni sana anijuze malengo ya ivyo vitambulisho vya mkaazi wa Zenj tafadhal.
 
Waunguja na Wapemba nje ya Muungano sijui hata kama wataweza kuishi pamoja bila kuvurugana

Kuna hawa masheha wana ubaguzi wa hali ya juu sana dhidi ya Wapemba, na huu ubaguzi una baraka zote za Serikali
Pana sababu...

Wengi wanaongea kushoto tu na wengine .wanajipambanua kwa upande mmoja tu... ila uhalisia huwa unakaliwa chini!

Mtenda akitendewa....
 
Mkuu hili linafanyika ili usipate kuandikishwa kwani sheha atakwambia rudi huko ulikotoka na ukirudi huko unaambiwa nenda ulikohamia. Mradi usiandikwe tu
Ukiona hivyo ujuwe una au pana walakini.lakini ni wengi tu wameandikishwa...bila shida!
 
Zanzibar hivi sasa imo kwenye harakati za kubadilisha vitambulisho vya ukaazi. Vitambulisho hivi ni muhimu sana kwa Wazanzibari wakaazi, kwani ndio nyenzo kuu ya kuendesha shughuli za kijamii na kisiasa kule visiwani. Bila kuwa na kitambulisho hicho maisha yanakuwa vigumu kuyaendea.

Nimesema hivi kwa sababu bila kuwa na kitambulisho hicho hata safari za ndani, yaani kati ya Unguja na Dar es Salaam pamoja na zile za kati ya Unguja na Pemba inakuwa vigumu. Ni vigumu kwani ili kupata tiketi unatakiwa kuwa na kitambulisho ama cha ukaazi, uraia, cha kupigia kura au leseni ya udereva.

Vitambulisho vyote hivi kwanza kuvipata kwake kuna uhusuiano mkubwa na kitambulisho cha ukaazi, ukiachilia mbali hichi cha uraia.

Ni bahati mbaya kwamba ubadilishaji wa vitambulisho hivi umeingizwa siasa. Nasema hivi kwani matayarisho ya uchaguzi mkuu yameanza chini kwa chini kwa kuweka miundo mbinu ya zoezi hilo. Hii ni pamoja na matayarisho ya uandikishaji wapiga kura. Utaratibu uliowekwa wa kubadilisha vitambulisho hivyo ni kwamba wahusika wanabadilisha pale walipovipatia mara kwanza (vikongwe vinavyobadilishwa).

Inapotokea mtu amehama anatakiwa achukue barua ya kule alikotoka na kuipeleka alikohamia ili sasa apewe barua ya kwenda kubadilisha kitambulisho. Katika hili ndio wenyewe wanapocheza mchezo huu wa kisiasa.

Masheha ambao ndio wanaotoa ruhusa ya kuandikishwa/kutokuandikishwa, wameweka daftari lao lenye orodha ya watu wanaotaka waandikishwe. Sheha anapokuwa na wasiwasi tu kwamba mtu sio MWENZAO anakwambia humo kwenye orodha yako na hivyo swala la kubadilishiwa kitambulisho chako ndio linaishia hapo.

Lakini ikumbukwe pia kwamba kama kitambulisho hakitobadilishwa ndio kusema kwamba mhusika hatopiga kura, hatopata tiketi ya kusafiria kati sehemu moja na nyengine kutoka visiwani, hatopata hata nafasi ya kuandikisha cheti cha kuzaliwa mtoto wake akiwa naye na mambo mengine mengi.

HII NDIO ZANZIBAR
Ukikosa hapo kituoni kwako nenda tu ofisi ya wilaya yako ukiwa na kitambulisho cha zamani cha uzanzibar na tanzania unalpia elf 5, unapewa, huko kwa sasa ni bure
 
Kuhusu kitambulisho cha kusafiria kutoka nje ya Unguja kwenda maeneo mengine hata cha kazi, nssf, zssf, na hata ukiwa huna kitambulisho chochote kinachotambulika Tanzania unaenda kwa Sheha anakuandikia barua inayokutsmbulisha eneo lako la ukaazi ambayo itakufanya upate tiketi ya kusafiria bila shida yoyote
Huyo sheha ni kwamba haingiriki kabisa, Mimi nilihama mji mmoja kwenda mwingine ndani ya unguja hii hii lakini nilipaswa kwenda na barua ya sheha,
Kupata barua kwa sheha ni ngumu Sana, kwanza anahisi unataka kitambulisho cha ukazi au unatafuta kazi au unataka kupata passport ya kusafiria....
Hii nchi wanaiharibu wenyewe, hakuna wa kumsingizia
 
Watu wanaweka hesabu sawa kwanza. Nadhani hata Bara nimesikia utaratibu wa kuhesabu wabiga kura umeanza, tuone utakapoishia
 
Huyo sheha ni kwamba haingiriki kabisa, Mimi nilihama mji mmoja kwenda mwingine ndani ya unguja hii hii lakini nilipaswa kwenda na barua ya sheha,
Kupata barua kwa sheha ni ngumu Sana, kwanza anahisi unataka kitambulisho cha ukazi au unatafuta kazi au unataka kupata passport ya kusafiria....
Hii nchi wanaiharibu wenyewe, hakuna wa kumsingizia
Kupata kitambulisho au pasport ni haki ya kila mwananchi na masheha wametoa sana hizo barua tena sana na wanaendelea kutoa.kama hataki nenda wilayani.... ......lakini hawakatai bure!

Kuna vitu vingi sana tu wameshtukia sasa hivi ndio maana watu wanalalamika ovyo!
Ila kipindi kile ilikuwa kimyaaa...
 
Ni ndogo lakini ni zaidi uijuavyo, ubaguzi sidhani kama utaisha
Ukijibaguwa.....ukashtukiwa .utabaguliwa tu!

Sio wewe ubague halafu usibaguliwe.

Kuna mengi sana hawayasemi hapa!

ugomvi huku si mpemba na muunguja ...ni mpemba kumtomtaka mbara !

Hamna jengine..hayo mengine ni wanazuga tu!

Ndio maana hapakai sawa...

Kila mtu hapo anafanya lake ugenini!

Waunguja wamechoka wallah!
 
Ukijibaguwa.....ukashtukiwa .utabaguliwa tu!

Sio wewe ubague halafu usibaguliwe.

Kuna mengi sana hawayasemi hapa!

ugomvi huku si mpemba na muunguja ...ni mpemba kumtomtaka mbara !

Hamna jengine..hayo mengine ni wanazuga tu!

Ndio maana hapakai sawa...

Kila mtu hapo anafanya lake ugenini!

Waunguja wamechoka wallah!
Naiona kama habari mpya!!
 
Hatutoi kwa vikaratasi. Unahaingaika nini kitambulisho cha mzanzibari?
Mkuu nilieleza awali kwamba hivi vitambulisho kama huna hata mtoto aliyezaliwa hapatiwi cheti cha kuzaliwa. Ingekuwa hivyo unavyosema wala sio tatizo.
 
Back
Top Bottom