Trubarg
JF-Expert Member
- Jan 8, 2020
- 4,261
- 6,908
Habari wadau. Kumekuwa na wimbi la wafanyakazi wa NHIF waliopo mahospitali kuwataka wazazi wabadilishe vitambulisho vya watoto kwakuwa picha zilizopo kwenye vitambulisho hazifanani na watoto kutokana na kubadilika.
Mimi hiki sikatai. Watoto wadogo wako katika hatua ya makuzi si jambo la kushangaza kuona mtoto akibadilika sura kila baada ya mwezi mmoja au kama si mwaka. Sasa sijafahamu kwanini hawa watu wanataka mtu abadilishe kadi kila sura inapobadilika, je hawajui kwamba hawa watoto wanakua. Kubadilisha kadi/ kitambukisho kinagharimu kiasi cha shilingi elfu ishirini. Kama mzazi ana mtoto zaidi ya mmoja inagharimu zaidi.
Nafahamu kwamba mzazi huwa anaulizwa details mbalimbali zinazohusu mtoto au mchangiaji kabla ya kadi au kitambulisho kutumika, lakini taarifa hizi kwao huwa bado hazitoshi wanasisitiza picha ya mtoto. Mimi nashauri badala ya kung'ang'ania mfumo tambuzi mmoja wa picha, wawekeze kwenye mifumo mingine ya utambuzi kama fingerprint scanner au scanner ya macho ambayo naamini ni za kudumu kuliko hii ya kusumbua wazazi kubadilisha vitambulisho mara kwa mara.
Mimi ndugu yangu mtoto wake mwenye mwaka mmoja alikataliwa kitambulisho cha mtoto wake kisa mtoto sura imebabadilika, huu ni uonevu wa hali ya juu.
Majibu ya NHIF, soma hapa - NHIF: Tutaanza kutambua Wanachama wetu kwa Kitambulisho cha NIDA