Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,209
- 1,635
Zanzibar hivi sasa imo kwenye harakati za kubadilisha vitambulisho vya ukaazi. Vitambulisho hivi ni muhimu sana kwa Wazanzibari wakaazi, kwani ndio nyenzo kuu ya kuendesha shughuli za kijamii na kisiasa kule visiwani. Bila kuwa na kitambulisho hicho maisha yanakuwa vigumu kuyaendea.
Nimesema hivi kwa sababu bila kuwa na kitambulisho hicho hata safari za ndani, yaani kati ya Unguja na Dar es Salaam pamoja na zile za kati ya Unguja na Pemba inakuwa vigumu. Ni vigumu kwani ili kupata tiketi unatakiwa kuwa na kitambulisho ama cha ukaazi, uraia, cha kupigia kura au leseni ya udereva.
Vitambulisho vyote hivi kwanza kuvipata kwake kuna uhusuiano mkubwa na kitambulisho cha ukaazi, ukiachilia mbali hichi cha uraia.
Ni bahati mbaya kwamba ubadilishaji wa vitambulisho hivi umeingizwa siasa. Nasema hivi kwani matayarisho ya uchaguzi mkuu yameanza chini kwa chini kwa kuweka miundo mbinu ya zoezi hilo. Hii ni pamoja na matayarisho ya uandikishaji wapiga kura. Utaratibu uliowekwa wa kubadilisha vitambulisho hivyo ni kwamba wahusika wanabadilisha pale walipovipatia mara kwanza (vikongwe vinavyobadilishwa).
Inapotokea mtu amehama anatakiwa achukue barua ya kule alikotoka na kuipeleka alikohamia ili sasa apewe barua ya kwenda kubadilisha kitambulisho. Katika hili ndio wenyewe wanapocheza mchezo huu wa kisiasa.
Masheha ambao ndio wanaotoa ruhusa ya kuandikishwa/kutokuandikishwa, wameweka daftari lao lenye orodha ya watu wanaotaka waandikishwe. Sheha anapokuwa na wasiwasi tu kwamba mtu sio MWENZAO anakwambia humo kwenye orodha yako na hivyo swala la kubadilishiwa kitambulisho chako ndio linaishia hapo.
Lakini ikumbukwe pia kwamba kama kitambulisho hakitobadilishwa ndio kusema kwamba mhusika hatopiga kura, hatopata tiketi ya kusafiria kati sehemu moja na nyengine kutoka visiwani, hatopata hata nafasi ya kuandikisha cheti cha kuzaliwa mtoto wake akiwa naye na mambo mengine mengi.
HII NDIO ZANZIBAR