Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Ajira buana..​

Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, “hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa”

Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri..

Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele “Mama nakufwaaa!”

Mara yule Simba akamwambia “Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu!

Rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia!"

Chezea ajira wewe!!!

 

Mke na mume​

Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani?!
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa blender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi saa 11 jioni bila kumtaarifu mkewe.. Alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui, aliondoka na blender toka asubuhi
 

Jamaa aokota wallet yenye pesa..​

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akafungua radio akatafuta station iliyokuwa na kipindi cha wasikilizaji kupiga simu..

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 9, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…”

Mtangazaji:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe... kama ana kusikiliza akutafute kwa namba Gani!?

John: Hapana, asinitafute tafadhali.. mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipo…!!!
Noma sana.
 
FB_IMG_1662543434900.jpg
 

Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao..​

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari: Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!

Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?!!
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone

Mama akaenda na Bakari akaanza

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimyaaa

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie basi, ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama: kimyaaa
Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu
dah! Ni hatari sana hii
 

Jamaa na binamu yake​

Jamaa alikuwa na tabia ya kunyandua binamu yake….

Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.
Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisa chumbani kwake….

Akanyata taratiiibu, akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudi…

MJOMBA; Ebooo.. wee mshenzi umefata nini chumbani kwangu, tena uko uchi?!!!
JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka
MJOMBA; ndo uje uchi?
JAMAA; ndio kwa sababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi
 

Madhara ya kusinzia kwenye ibada​

Tukiwa kanisani majuzi, mdada mmoja alikuwa amesinzia , akaamka akasikia tu Pastor anasema:
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliyesimama..

Pastor akamwambia, wee dada endelea kusimama hivyo hivyo..,
Pastor: tumepata mmoja hadi sasa, huyo aliyesimama..

Pastor: Narudia kwa mara ya mwisho kwa ambaye hajaelewa..
” Kama wewe umewahi kumsaliti mwenza wako au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
we jamaa una talent ya uchekeshaji, hongera sana
 
Back
Top Bottom